Wivu, Ngono vilivyopelekea kuuawa kwa Travis Alexender

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
3,995
2,000
In every murder, there is a motive... Huu ni msemo wenye ukweli 99%. Ni mara chache kutokea mauaji yalitokea tu bila lengo.

m2.jpg


Tarehe 4, mwezi 6, 2008, Kijana mtanashati kabisa aliyekuwa kama afisa mauzo wa kampuni ya Bima aliyejulikana ama Travis Alexender aliuawa kwa kuchomwa chomwa na kuchinjwa kisha mwili wake kutelekezwa bafuni katika nyumba yake iliyopo kwenye mji wa Mesa, huko Arizona (kwa wale amabo hamjui Arizona iko wapi, ngoja niwasaidie iko kwa Trump).

Mwili wake ulibaki bafuni pasipogunduliwa na mtu yoyote kwa siku tano. Kuonyesha kwamba muaji alikuwa kadhamiria na hasira sana, mwili wake ulikuwa una majeraha 27 ya kisu, na ulikuwa na tundu la risasi kkichwani, huku ukiwa umichinjwa kuanzia sikio moja kuelekea shingoni mpaka kwenye sikio la upande mwingine. Eneo tukio lilipotendeka lilikuwa halitamaniki kwa damu ilivyokuwa imetapakaa. Baada ya mwezi, polisi walimkamata aliyekuwa mpenzi wake wakaachana, Huyu hakuwa mwingine bali mwanadada pisi kali (angalizo hajalingana na Uwoya) kwa jina anajulikana kama Jodi Arias.

Arias alidai ya kwamba alimuua Alexender kama njia ya kujikinga. Mahakama hikukubariana na utetezi wake hivyo alikutwa nahatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2013.

Na mimi mtafisiri wenu Nafaka, leo nitakuletea kisa chote cha tukio zima mpaka Arias kuamua kumuua mpenzi wake waliyekuwa tayari wameachana.

Jodi Arias ni nani?
m1.jpg


Arias alizaliwa mwaka 1980 kwenye mji wa Salinas, huko California. Baba yake alijulikana kama Bill Arias na mama yake akijulikana kama Sandy Arias. Arias ana dada wa kufikia, na dada mwingine ambaye ni dada yake kabisa pamoja na kaka wawili. Arias aliacha shule akiwa high schoo, ila baadae alifanya General Educational Development Test (GED). Muda wake mwingi alitumia kuzunguka zunguka sehemu mbali mbali. Pia alijihusisha kimahusiano na wanaume mbali mbali na kuhama toka dhehebu moja kwenda dhehebu nyingine.

Katika mahojiano ya makachero na mama yake, alidai mtoto wake alikuwa kawaida tu kama watoto wengine, japo kuna kipindi alidai kwamba mwanae alikuwa na matatizo ya akili yajulikanayo kama bipolar disorder. Baba yake pia alidai kwamba mtoto wao alikuwa msiri sana na hakuwa muwazi na akiwa na umri wa miaka 14 kuna kipindi waligundua kuwa anaotesha bangi kwenye bustani yao (dogo kumbe alikuwa anauelewa mmea).

Pia Jodi mwenyewe wakati akijitetea mahakamani alidai wazazi wake walikuwa siyo wazazi bora kwani walimnyanyasa kiakili, kihisia na kimwili.

Kukutana kwa Jodi na Travis
jodi.jpg


Ilikuwa mwezi wa 9, mwaka 2006 ambapo Arias alikuwa na Alexender kwa mara ya kwanza. Alexender alikuwa ni mmoja kati ya wazungumzaji kwenye Kongamano lililoandaliwa na kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi kwa wakati huo iliyojulikana kama, Pre-Paid Legal Services, huko Las vegas.

Kwa kipindi hicho Arias alikuwa akijihusisha na upigaji picha huku akiishi California, wakati Alexender yeye alikuwa akiishi Arizona. Haikuchukua muda hawa wawili kuwa karibu na kuanzisha mahusiano ya kimapenzi. Ndani ya muda mfupi toka walipokutana, Arias, allimbwaga mpenzi wake wa muda mrefu aliyekuwa akiishi naye. Hawa wawili, walianzisha mahusiano ya mbali (kwa kingereza eti uwa wanasema long distance relationship). Kumbukumbu zinaonyesha ya kwamba katika kipindi hicho, walibadilishana emails zipatazo 82,000. Arias anadai kwamba walifanya ngono na Alexender wiki ya kwanza tu toka walipokutana, japokuwa ngono kabla ya ndoa haikubailiki katika imani Ya Alexender, Kanisa la Mormon.

Mwezi wa 11, mwaka huo huo wa 2006, Arias aliamua kubadili imani yake na kuwa muumini wa Mormonism, ili awe sawa na mpenzi wake. Alexender alimbatiza mpenzi wake. Mahusiano yao yalikuwa kingono zaidi, na rafiki zake Alexender wanadai Arias alikuwa na wivu sana. Wapenzi hawa waliachana baada ya miezi mitano tu, ila waliendelea kushiriki ngono na kuwasiliana. Arias alikasirishwa sana alipofahamu ya kwamba Alexender ameanza kujihusisha kimapenzi na mdada mwingine. Inasemekana Arias hasira zake zilimpelekea kufanya matendo mengi ya ajabu, kama kutoboa matairi ya gari la Alexender. Pia alihack akaunti za mitandao ya kijamii za Alexender. Inasemekana, kutokana na mambo Arias aliyokuwa akimtendea Alexender, ipo siku aliwahi kumwambia rafiki yake wa karibu kuwa, asishangae akija kusikia kuwa kauwa na Arias.

Kufikia mwezi wa 6 mwaka 2008, Alexender alikuwa kachoshwa na matendo ya Arias hivyo aliamua kumwambia waache kuonana wala kuwasiliana, anataka aondoke kabisa kwenye maisha yake.

Kuuawa kwa Alexender
travis.jpg


Siku kadhaa abla ya kuawa kwa Alexender, ilikuwa ni tarehe 28 mwezi wa 5, mwaka 2008 bunduki iliporwa kutoka kwenye makazi ya babu na bibi yake Arias. Arias alikuwa akiishi huko kwa kipindi hicho. Hiyo bunduki ndiyo ilikuja kutumika kumuua Alexender.

Alexender alikuwa amepanga kusafiri na Arias kwenye shughuli zake huko Mexico, ila alibadili uamuzi huo na kuamua kuwa atasafiri na mdada mwingine. Tarehe 2, mwezi wa 6, 2008 Arias alikodi gari kutoka katika kampuni ya kukodisha magari ijulikanayo kama Budget rent-a-Car yenye makao yake huko Redding, California. Arias aliendesha gari hizo mpaka Mesa, Arizona kuoanana na Alexender. Tarehe 4, mwezi 6, wawili hao walifanya mapenzi wakiwa kwenye bafu liliko kweye nyumba ya Alexender. Ushahidi wa kufanyika tendo hili polisi waliupata kwenye picha walizojipiga kwenye kamera iliyokuwa kwenye mashini ya kufulia nguo.

Rafiki zake Alexender ndio waligundua mwili wake siku chache baadae baada ya kutomuona wala kupokea simu zao kwa siku kadhaa. Mwili wake ulikuwa na majeraha mengi ulikuwa ushaanza kuoza. Alexender alikuwa kapigwa risasi ya kichwa, na kuchomwa chomwa mara 27, kisha shingo yake kuchinjwa. Kamera iliyosadikika ilikuwa ya Arias, ilikutwa ikiwa imedumbuizwa kwenye mashini ya kufulia nguo ikiwa kwenye maji mle mle bafuni. Polisi waliweza kupata picha zilizomo kwenye memory card, na ziliweza kumuoneysha alexender na matukio ya kabla ya kuawa kwake na pia kuna picha zilizoonyesha mwili ukiwa umelala pembeni ya siki la bafuni ukiwa umetapakaa damu.

Polisi walimkamata Arias kama mhusika wa mauaji tarehe 15, mwezi wa 7 mwaka 2008. Wakamfungulia mashitaka.

Kesi juu ya Arias

Kati ya mambo ambayo yalitawala kwenye kesi hiyo ni juu ya wawili hawa kuwa waumini wa dhehebu la Mormon, lakini kulikuwa na zile picha zilizoonyesha wanafanya ngono, na nyingine Arias akiwa analiwa kinyume na maumbile na Alexender. Wakili mtetezi alidai Arias alimuua Alexender katika harakati ya kujitetea maana uhai wake ulikuwa hatarini. Wakili alidai Alexender alimbamiza arias kwenye sakafu huko bafuni, ambapo walipambana sana. Akadai kama Arias asingepambana basi angekufa yeye.

Arias pamoja na wakili wake walijaribu kuonyesha kwamba Alexender alikuwa akimtumia Arias wka ajili ya ngono tu na alikuwa akimuumiza kihisia, kimwili na kaikili. Wakili wake Arias alienda mbali zaidi mpaka kumleta mpenzi wa zamani wa Alexender, aliyejulikana kama Lisa Andrews Daidone kama shahidi, ambapo naye alidai ya kwamba alikuwa akihisi kuwa Alexender anamtumia kingono kwenye uhusiano wao.

Mahakama haikukubaliana na utetezi huu. Mwaka 2013 mwezi wa tano, Arias alipatikana na hatia ya mauaji. Mahakama ilishindwa kukubariana kama ahukumiwe kunyongwa, ikiwa ina maana Arias ilipaswa kesi yake isikilizwe tena kuanzia mwaka 2014. Mwaa 2015, baada ya kesi ya kusikilizwa tena bado mahakama ilishindwa kukubaliana kama anyongwe au laa, hivyo waliamua kuondoa uwezekano wa kunyongwa na kumhukumu kifingo cha maisha bila uwezekano wowote wa kuachiwa. Baada ya hukumu yake, Arias alionekana kujutia alichofanya akidai kama kungekuwa na namana ya kurudisha wakati nyuma asingefanya alichofanya.

Over..............................
 

Petluk

Member
Sep 11, 2017
97
125
Story zako nzur sana unazimaliza, sio zile story za nitarud badae. Hongera sana mkuu
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
53,423
2,000
Wazungu wanaua kikatili sana, naamini kabisa shetani ni ndugu yao wa damu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom