Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Ukiwa na mtu akakuambia habari za mtu aliyekuwa naye kabla au aliyefikiria kuwa naye ila ukawa husikii wivu hasa huyo mtu mwingine anapokuwa karibu au unapomuona jua humpendi mwenzio. Na ukiwa na mtu mkaachana, akakuacha au ukamuacha halafu ukimuona na mtu mwingine husikii wivu tambua kuwa ulikuwa humpendi mwenzako. Wivu ni kipimo thabiti cha mapenzi. Tahadhari: Wivu ukizidi husababisha kifo. Ushauri: Maumivu yatokanayo na wivu yakizidi muone daktari. Kwa leo ni hayo tu kutoka kwenye Tafakuri za Alfajiri za Kompanero.
---
"Penzi Kitovu cha Uzembe" - Ngoswe
---
"Penzi Kitovu cha Uzembe" - Ngoswe