Wivu katika mahusiano ya Ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wivu katika mahusiano ya Ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Unazo!, Jul 17, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,755
  Likes Received: 2,345
  Trophy Points: 280
  Wakuu nimekua nikifuatilia maada nyingi za ndoa na upenzi humu kwenye jamvi nikaja gundua kuwa yaote yatokeayo ndani ya mahusiano hayo ni wivu wa mmoja wao kutomwamini mwenzie au kutokuwa karibu na mwenzi wake iwe kwenye ndoa au huko kwenye upande mwingine.

  Wakuu naombeni nisaidie nani anastahili kuwa na wivu kwa mwenzie?Mwanamke au mwanaume?na ni wivu gani mzuri wa upande wa mwanamke au mwanamume.?

  Na kama nitakuwa natumia neno wivu kwa tafsiri toafuti na niliyomaanisha kwenye maelezo ya mwanzo;Je nini maana ya wivu?Nini Faida na hasara za wivu?

  Labda hili likikijibiwa tutakuwa tumemsaidia mwanajamii one na wengine tunaoazinshia thread zenye muingiliano wa mahusiano.

  Wakuu nawasilisha.
   
 2. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  wivu kwenye mapenzi ni muhimu, lakini wivu wa kiasi usipitilize hadi ukawa kero,
  Wivu ni kutaka uliye naye awe wako peke yako, na ukimpenda mtu lazima umuonee wivi.
  Na wivu ukizidi sana hata mambo madogomadogo yatakuwa yanakusumbua sana, ambayo ni ya kawaida. mpende mwonee wivu kiasi basi.
   
 3. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,755
  Likes Received: 2,345
  Trophy Points: 280
  kipimo chake cha wivu wa kiasi ndo hapo chacha!!!!!!!!!!
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Wivu haukosekani kwenye mahusiano ila kiwango chake kinatofautiana. Mwanamke/mwanaume wote tunakuwa na wivu kutokana na kwamba wao ni wapenzi hivyo hupendi penzi mnaloshare na kila kitu ndani yake likaamia kwa mtu mwingine ilhali unampenda huyo mpenzi na bado ni wapenzi..Unataka umiliki lile pendo na upewe wewe peke yako siyo kuona kuna 'wagombea wenza' wamekuzunguka.

  NB: Wivu ukizidi ni mbaya na kipimo chake ni vitendo mtu afanyavyo akiwa na wivu wa hali ya juu kama kumpiga mwenza wake ukihisi ana uhusiano wa mashaka, kusababisha ugomvi na anaohisi wanamuibia mwandani wako, kuchunguzana kupita maelezo(kama vile unaishi na mpelelezi)..
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Wivu muhimu bwana!
   
 6. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Tutofautishe kati ya upendo na wivu. Upendo ni ridhio la moyo kwamba sasa umefika na hakuna pengine tena. Alama za upendo wa watu wawili hawa ni nyingi: kujali, kuhudumia mwingine, kujito kwa ajili yake, kusamehe yakitokea makosa, uaminifu, nk.

  Wivu si dalili ya upendo. Wivu ni kitu hasi siyo chanya. Wivu ni dalili ya KUTOKUMWAMINI mwenzako wa ndoa. Mwenye wivu anakuwa na wasiwasi kwamba wenzake wanamwibia, anakosa raha, ananyong'onyea, anakuwa na hasira, anakuwa hajiamini na haamini kwamba "chombo" ni chake tu! Huu ni ugonjwa mbaya ndiyo maana wenye wivu wanapigana ngewe, wanauana, wanakunywa sumu na kujinyonga.

  Mtu anayempenda mwenzake hapaswi kuwa na wivu kwa vile anamwamini mwenzake. Mkipendana lazima muaminiane na kutokumtlia mwingine mashaka kwamba wanamnyemelea vibaka na mafisadi wa mapenzi. Kumbe kati ya watu hao wawili hapapaswi kuwepo wivu. Wivu daima ni negative concept.
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Usipite kiasi
   
 8. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,755
  Likes Received: 2,345
  Trophy Points: 280

  Nashukuru sana kwa kuweka wazi kwamba wivu ninegative concept ya mwenzi wako.

  jamani hapa ndo nachanganyikiwa wengine wanasema kama huna wivu na mwenzio basi hakuna upendo.
  Mbona kunamchanganyiko wa uelewa? Am total confused
   
 9. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wivu ni mapenzi
  wivu ni kiama
  wivu ni kuchanganyikiwa
  wivu ni kukosa amani
  wivu ni karaha
  wivu ni kukosa uhaminifu
  wivu ni donda ndugu
  wivu ni kihoro
  wivu ni kupenda kupita kiasi
  wivu ni ajali ya mapenzi
  wivu ni kifo cha mapenzi
  wivu ni balaa katika mapenzi
  wivu ni presha za ghafla na kudumu

  NB: Angalia zilizo-positive na zilizo-negative then uta-conclude mwenyewe wivu una faida au hasara

  Ushuhuda/Experience
  Binafsi nilikuwa na bado nina wivu na nimeshakosana hadi kuachana kwa kile kinachoitwa wivu na wapenzi kama watatu hivi kama sikosei

  Funzo/Fundisho
  Sasa hivi niko kwenye process ya kuondoka uko kwenye kuwa na wivu na niko kwenye stage ya tatu bado stage nyingne tatu nafikiri nitazimaliza kabla ya kuingia kwenye ndoa so i think that ndoa yangu itakuja kuwa na amani sana.

  Tahadhari
  Unapokuwa na wivu ni lazima tu utagundua kitu ambacho sio sahihi kwa mpenzio kutokana na kumfuatilia kwa kila analolifanya iwe nyumbani ama kazini ama kwenye sherehe

  Present Situational analysis ya wivu
  Simu zimekuwa chanzo kikubwa cha kufanya mapenzi yaingiliwe na wivu. Kabla hujaniuliza kivipi fanya uchunguzi wako binafsi

  Asanteni
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,066
  Trophy Points: 280
  Wivu = f(ubinafsi, woga, kutojiamini, x,y,z)
   
 11. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,755
  Likes Received: 2,345
  Trophy Points: 280

  kwa kweli nashukuru sana!!kumbe katika yote yanayomtokea ndugu yangu mwanajamiione atakuwa amepata jibu karibia kila kitu alichokuwa anataka tumshauri na wengine wengi ambao wamekuwakuwa wakianzishwa thread zinazoonyesha matatizo katika mahusino.

  Hivyo basi kwa kumalizia tu ni kwamba wivu ukitumia katika negative side kama ilivyoainisha hapo juu ndoa haitakuwa na amani kamwe nami nimejifunza kwa kuwa nilikuwa na mapungufu makubwa sana kwa sababu unakuta na mind hata mambo madogo na nispojibiwa tu naanza kulalama kuwa nadharauriwa kwa kweli from this time leo naenda kumtoa out mtu wangu ili niweze kuliconcile yaliyokuwepo.

  That is place to air out now and then human problem katika level zote.

  Big up guys.

  Mwanajamiione please not something from this thread na hii nilianzisha mahususi kwa ajili yako na nimefurahi guys with experience na tremendouly outstanding wameweza kusema ukweli juu ya hili suala na ndo chanzo yote yatokeayo katika hatua zote uzijuazo za mahusiano kuanzia level y ubf/ugf na hata ndoa.

  So be happy kwa kuwa sababu ni hizo za wivu usiokuwa wa maana kama alivyosema Mkapa.
   
 12. ocade

  ocade Member

  #12
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 26, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  wivu ni muhimu sana, na bnila wivu zi kwamba humoeni mwenzako, vivu ndi unaonyesha unamoenda na kumjali mwenzako kiasi gani,

  huu upendo wa kikaka kakaaa tuu si huo unaongelewa hapa, hapa unaongelewa upendo wa kimahusiano ya kimapenzi,


  so wivu ni muhimu na wivu ni kipimo cha mapenzi, tena mapenzi ya ukweli!

  uliza kila mtu atakueleza hayo ndugu yangu!
   
 13. Daud omar

  Daud omar JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2014
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,467
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Aggggrr mim niliwacha kitambo hayo mambo yalinifanya nikose raha sana, eti mtu anakuonesha wivu na wasi wasi kibao juu yako alafu yeye ndio wa kwanza unamshika anakusaliti, kwhyo siku hizi hizo presha staki tena, mpaka kuna mwengine anananiulize eti bebe hiv wew hauna wivu mim nina wasi wasi na mapenz yako, nikamwambia tupa kule wew kama unanpenda basi utaniepusha na maswala yanayoleta wivu
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2014
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Dah, wivu mbaya sana. Unakufanya unaumizwa hata na jambo dogo tu, siutaki kabisa.
   
 15. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2014
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  hmm yaanii ni balaa...mnagombana kwa vitu visivyo na kichwa wala miguu..
   
 16. Nanaa

  Nanaa JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2014
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 5,909
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nina mpango wa kumuacha mtu kwa sababu ya wivu, kila nikiongea naw hanielewi....yani hadi nakonda. simu yangu inakaguliwa kuanzia call logs hadi phonebook, siruhusiwi kwenda hata sokoni, nikikutana na mkaka niliyesoma nae au jirani yangu nikimsalimia tu basi nikila kona vibao...eti namdharau nachekeana na wanaume mbele yake.
  Nikisafiri naulizwa nimekaa na nani, nikisema mbaba au mkaka basi nitakoma, manake nikichlewa kujibu sms basi nlikuwa natongozwa.
  Yani nahisi mateso hadi upendo wangu kwake umetumbukia nyongo. Nalazimika kuwa muongo ili mambo yaende mfano nikienda sokoni namwambia nalala.
  Kwanza hapa nilipo nina mihasira sijaenda kucheck mechi manake nimepigwa stop kwenda uwanjani.
  Am gonna break up with somebody...am tired oooh.
   
 17. Himidini

  Himidini JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2014
  Joined: May 8, 2013
  Messages: 5,570
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 145
  ^^
  Pole Kim nana
  ^^
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Nanaa

  Nanaa JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2014
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 5,909
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...