Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,319
- 72,742
Wakuu,
Mwanadamu akifanya juhudi zake zote na kushindwa huwa anamkabidhi Mwenyezi Mungu swala hilo na kumuomba atende kwa kadri atakavyoona inafaa.Sisi raia wa nchi hii ni wajibu wetu kuihoji na kuisimamia serikali yetu tuliyoiweka madarakani na kwa utaratib.
Watu milioni 45 au 50 hatuwezi fanya hivyo kwa pamoja ndio ukawepo utaratibu wakupata wabunge kadhaa watuwakilishe kwenda kukubali mambo mazuri ya serikali na kukataa kabisa mambo ya hovyo ya serikali kwa niaba yetu.Bahati mbaya kuna kundi kubwa la wawakilishi wetu karibia 70% wao wapo pale hata hayo ya hovyo wanayatetea na wameamua pia kupambana na wachache wanaotusemea kupinga hayo mabaya.Hii ni dalili ya pepo mchafu kuwepo ndani ya bunge na ndio maana hilo kundi kubwa halijitambui kabisa.
Wito kwa viongozi wa dini, wadau wengine humu JF na wananchi kuandaa maombi maalum kwa ajili ya wabunge wetu ili ufahamu uwarudie na wajue wanapaswa kututetea na mienendo hii ya serikali ambayo inaashiria magumu kwetu na vizazi vyetu.
Pia Mungu awatie nguvu wale wachache watuteteao lakini wanakumbana na kufedheheshwa, kunyanyaswa, kufukuzwa hata kunyimwa posho eti kwa vile hawaridhiki na anayewadhalilisha, ili nao wasijisikie kama yatima.