Wito: Waziri Jafo tumeona maelekezo ya Geita na Mpanda ni maamuzi mazuri, Temeke je?

Kupitia vyombo vya habari kwa siku za hivi karibuni tumeona Mh Jafo akimsimamisha Mkurugenzi wa Geita kupisha uchunguzi na pia ametoa maelekezo kama hayo kwa Halmashauri ya Mpanda.

Lakini Mh. Jafo watu wengi wanajiuliza kuna lile Gari la Mkurugenzi wa Temeke ambalo limenunuliwa 400M mwaka 2019 na pia inasemekana kanunua magari aina ya Tata ya kubebea watumishi ambayo nayo wanadai ni mabovu tunaiwekaje hii? Mh chukua hatua kali Mh Raisi anakuamini sana.
Na magari 9 aina ya landcruiser VXR V8 ya serikali yaliyopakwa rangi ya kijani wakati wa kampeni yapo wapi sasa ? Nani aliyatoa? Naye awajibishwe.
 
Kwa ujumla TAMISEMI kumeoza, Morogoro barabara mpya tu ni mashimo kwa kwenda mbele. Hata soko jipya halifanani na thamani ya fedha iliyotumika kulijenga. Jafo inabidi akaze buti ili atoboe 5yrs.
Buti lipi la kukaza Ila wadanyika mmekuwa waBwege mpaka mnakera!

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Huyu DED madiwani wa manispaa ya Temeke wanalalamikia kutumia ubabe kwa walimshutumu kununua magari ya kifahari ya pesa nyingi kwa kutumia ubabe bila kuwashirikisha sawa. Kama haya yana ukweli na hajatumbuliwa hadi sasa, nani anamkingia kifua?
Rais wetu mpendwa JPM tupia jicho lako kali mahali hapa.
Ungejua huyo unaemuomba akusaidie kuwa ndio tatizo lenyewe wala usingeandika huu ujinga

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Uzi umegeuka wa kupigia chapuo makada, ooh January anafaa ooh Makondakta anafaa,
Wote watoto wa baba mmoja, tusidanganyike na maigizo!

Hata aingie nani mfumo uliopo ndiyo unaotoa mianya yote hiyo!

Nchi inahitaji mfumo imara siyo mtu!

Everyday is Saturday........................... :cool:
 
Back
Top Bottom