WITO: Watanzania Tumwombee rais Kikwete

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Ni wazi Rais Kikwete anakabiliwa na kazi ngumu hivi sasa haswa kwa mambo mawili makubwa;

KWANZA, Ni kuunda Upya kabisa Cabnet, (au labda kuikarabati), Kazi ambayo naamini si rahisi kwake kutokana na ukweli kuwa amefanya hivyo mara tatu bila matokmeo ya kuridhisha.

PILI, Safari ya uandikwaji wa Katiba Mpya inaanza. Safari itakua na ugumu wa aina yake haswa tukikumbuka kwa mfano suala la Muundo wa serikali ama MOJA, MBILI au TATU lilivyo mvutano Nchini.

Ndg zangu Rais huyu anaongoza Nchi na si familia yake. Na nchi ni yetu sote pamoja na Wewe!
Hatuna budi kila mmoja wetu kwa imani yake, Tumuombee awe na Busara na Hekima Pamoja na wanaomsaidia na kumshauri ili aweze kutupitisha salama katika Mambo haya,

"TOGETHER WE SHALL STAND"
 
Mkuu umeongea mambo ya msingi sana mungu amlinde rais wetu na adumu zaidi.
 
Alishasema Urais ni wa kwake yeye na Familia yake, kwa hiyo ajiombee mwenyewe na Familia yake..
Kuhusu Cabinet ni uzembe wake mwenyewe kuteua "washikaji" wanaomuangusha kila siku.
Kuhusu Katiba mpya ni wajibu wake kama Rais kuhakikisha tunaipata, na kama hawezi basi apishe wanaoweza watuongoze katika hilo.
 
Amezidi kwa uzururaji. Akiacha hilo utakuwa mwanzo mzuri.
 
Alishasema Urais ni wa kwake yeye na Familia yake, kwa hiyo ajiombee mwenyewe na Familia yake..
Kuhusu Cabinet ni uzembe wake mwenyewe kuteua "washikaji" wanaomuangusha kila siku.
Kuhusu Katiba mpya ni wajibu wake kama Rais kuhakikisha tunaipata, na kama hawezi basi apishe wanaoweza watuongoze katika hilo.

***like***
 
Ni kweli watanzania tumwombee rais aweze kuwashinda wasimtakia mema hasa wale walio ktk chama chake cha CCM!
 
Yupo sheikh Ilonga. wakutane Moro. akishindwa amtafute Lusekelo yupo hapo hapo Dar.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom