Wito: Wassira Jiuzulu kwa hiari

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Waziri wa mahusiano na uratibu katika ofisi ya Rais aliwahi kulitangazia taifa kuwa milango ya Ikulu imefungwa na kamwe Wapinzani hawatakuwa tena na nafasi ya kukutana na Rais , na hii ilikuwa mara tu baada ya mabadiliko ya sheria ya mabadiliko ya katiba yaliyokuwa yamepitishwa kibabe na kihuni Bungeni,

Mara baada ya Rais kurejea tarehe 04.10.2013 akihutubia taifa aliomba kukutana na viongozi wa vyama vyenye hoja ambavyo ni Chadema, CUF na NCCR Mageuzi, hii ilikuwa jibu au pigo kubwa kisiasa kwa Waziri Wassira ambaye alishafunga milango ya Ikulu , huku akijua wazi kuwa wajibu wake ulikuwa ni kudumisha mahusiano baina ya ofisi ya Rais na wadau wengine nchini, hakutimiza wajibu wake huo wa kuratibu na kudumisha mahusiano.

Kikwete , ameomba kukutana na viongozi hao tarehe 15.10.2013 Ikulu, ile ile ambayo Wassira alisema milango imefungwa,
hivyo, kutokana na mtiririko huo wa matukio Hayo anapaswa kujiuzulu kwa hiari au Rais amfukuze kazi mara moja maana ameshindwa kutimiza wajibu wake wa kudumisha mahusiano.

Ninatoa wito, kwa Wassira kujiuzulu mara moja kwa ajili ya kulinda heshima yake , asisubiri mpaka afukuzwe kazi na Rais , aidha, kama Rais anataka kuwepo kwa katiba bora ya watanzania , anapaswa kumwajibisha Wassira pamoja na waziri wa sheria na katiba kutokana na matamko yao waliyoyatoa .

Jisomee makala hii.

MINYUKANO KATIKA JAMII
Ukitaka kuboresha uhusiano, usimtumie Wassira
Msomaji RaiaToleo la 287
27 Mar 2013
SAFU hii iliwahi kuandika na kushauri kuwa Serikali ikitaka kudanganya umma juu ya jambo fulani, isimtumie Kamanda Suleiman Kova wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam.

Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hakumjalia kipawa cha kuficha jambo la hila. Anapotoa taarifa kwa umma hujikuta akiongea huku kama anasikiliza kitu kingine masikioni mwake au akijaribu kukumbuka alivyoagizwa aseme.

Matokeo yake, mtiririko wa taarifa yake hupata dosari zinazowafanya wasikilizaji watilie shaka taarifa yake. Kova si mesenja mzuri wa kupeleka taarifa za kupika maana macho yake na mwili wake humsaliti anapoanza kufanya hivyo.

Tulimwona wakati wa sakata la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Steven Ulimboka na hata majuzi wakati wa sakata la polisi kukimbia na fuko la fedha walilowanyang'anya majambazi maeneo ya Kariakoo.

Yupo mtu mwingine wa namna hiyo katika serikali yetu. Huyo ni Waziri wa Uratibu wa Mahusiano Ikulu, Stephen Wassira. Wiki hii alijitokeza katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV.

Imekuwa ni kawaida yake kukimbia huku na huko kushughulikia minyukano mbalimbali ya kijamii. Kujitokeza kwake mara kwa mara kunaashiria mambo makuu mawili. Kwanza, ama serikali ina upungufu mkubwa wa watu wa kushughulikia mitafaruku katika jamii na kwa hiyo kumwona yeye ndiye ana nafuu. Hili limeonekana hata katika medani za siasa pia ambapo CCM imelazimika kuwatumia mawaziri wachache sana, wale wale kila mahali katika kuhutubia mikutano ya hadhara.

Pili, kwamba mzee Wassira ni wajibu wake kushughulikia mahusiano na kwa hiyo ni yeye anayepaswa kutokea kila mahali kutoa maelezo na msimamo wa serikali kuhusiana na mitafaruku hiyo. Kwa mtizamo wangu na wa wengi, ambao nimewasikia wakizungumza, nadhani ni sahihi kusema, mzee Wassira anatengeneza mitafaruku zaidi kuliko kuitatua. Uwezo wake wa kutengeneza mitafaruku ni mkubwa kuliko uwezo wake wa kuiibua na kuichochea iende kwa kasi zaidi. Nitaeleza.

Awali ya yote niseme wazi kuwa kimsingi, kuunda Wizara hii katika serikali hii kulizua maswali mengi. Mantiki iliyotumika kuona na kuamua kuwa kuna haja ya kuwa na wizara inayoratibu mahusiano katika Taifa ina kasoro kubwa.

Kasoro mbili ziko wazi. Kwanza, kuunda taasisi au chombo cha kushughulikia migogoro ni sawa na kuweka uwezekano wa kutengeneza migogoro zaidi ikiwa iliyopo haitoshi au hailipi. Hulka ya mwanadamu ukimuundia kitengo cha kushughulikia tatizo, huwa ni kuunda tatizo ili kitengo hicho kipate kazi ya kufanya.

Tukichunguza kwa makini tunaweza kugundua kuwa mzee Wassira amekuwa anatengeneza migogoro ili apate kazi ya kufanya. Anaweza kuwa anafanya hivyo kwa kujua au kutojua kwake. Mtindo wake, haiba na misimamo yake vinakuza (escalate) migogoro badala ya kuipunguza. Hii ni kwa sababu, yeye binafsi ni mkereketwa (Zealot) wa misimamo fulani na anapenda misimamo hiyo ikubalike na wote wote anaoshughulika nao.

Katika hali ya ombwe la uongozi lililopo, mtu kama Wassira ambaye ni mwepesi wa kubandika (impose) mawazo yake kwa haraka, ni rahisi sana kwa yeye kuonekana ndiye anafaa kwenda maeneo yenye migogoro kutoa maelezo na msimamo wa serikali. Serikali isipoligundua hili, itapoteza muda mwingi na raslimali kushughulikia migogoro isiyokwisha.

Pili, mojawapo ya dhamana (role and responsibilities) za wateule wa rais katika serikali ngazi zote ni kutatua migogoro, kuboresha mahusiano na hata kutengeneza mahusiano mapya katika maeneo yao ya kazi. Pale ambapo wateule hao hawawezi kuifanya kazi hii vizuri, kuna maofisa uhusiano wanaoshughulikia suala hili.

Kwa uamuzi wa serikali kuunda wizara inayoshugulikia mahusiano kwa njia ya kuratibisha au kutatua migogoro pale inapojitokeza, ni sawa na kuwaambia wateule wengine waachane na wajibu huu ambao umo katika mikataba yao. Ni maoni yangu kuwa, kuibuka kwa mitafaruku na minyukano mingi ya kijamii katika Taifa kwa sasa ni matokeo ya utekelezaji wa sera hii inayopungukiwa na umakini wa kimantiki. Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamebakia kumsubiri Wassira alete suluhisho la mitafaruku inayojitokeza katika maeneo yao.

Hata pale baadhi ya watendaji wanapojitokeza na kutafuta suluhu ya mitafaruku ya kijamii, wanakuwa hawana uhakika kama hawatagongana na mzee Wassira na matokeo yake walio wengi wanaamua kuacha au kuwaambia watu kuwa wasubiri jibu kutoka Ikulu.

Katika kipindi cha dakika 45 wiki hii, mzee Wassira alikiri wazi kuwa serikali imekuwa inachelewa mno kushughulikia matatizo na kusababisha yapanuke kiasi cha kutishia amani na mshikamano wa watanzania. Jibu lake na maelezo yake kuhusu uchelewaji wa serikali, vinathibitisha kile ninachokijadili na kile kinachoimbwa na wengi kuhusu ombwe la uongozi katika serikali.

Tatizo jingine kubwa la mzee Wassira anaposhughulikia mitafaruku ya kijamii ni kuchanganya haki na hila. Nimefikia kushawishika kuamini kuwa pengine hii ndiyo sifa kuu iliyomfanya mteuzi wake amteue kushika wadhifa huu wa wizara kiraka katika serikali.

Mzee Wassira anapotafuta suluhu ya mitafaruku daima anatafuta kushinda. Hii si sifa nzuri kwa mtu anayetafuta kusuluhisha migogoro. Anapohisi anaweza kuonekana ameshindwa, hujiona mdhaifu na mnyonge, na hii humfanya kuamua kutumia mbinu chafu ili kufikia ushindi wake.

Katika mahojiano yake ya dakika 45 alitamka kuwa Rais alikutana na viongozi wa dini Machi 7, 2013 Ikulu ya Dar es Salaam. Lakini wiki iliyopita vyombo kadhaa viliripoti kuwa Wassira aliwahadaa baadhi ya viongozi wa dini kuwa wanahitajika Ikulu na kuwa maaskofu wengi walikuwa tayari wamefika lakini viongozi hao walipofika walijikuta wako peke yao.

Aidha, ni Waziri huyu huyu Wassira aliyepata kusema mwaka jana kuwa chama fulani kitasambaratika hivi karibuni. Katika mahojiano yake na kipindi cha dakika 45, mzee Wassira akajikuta anang'ang'ania kuzungumzia suala la kukamatwa kwa kiongozi wa chama hicho cha upinzani kana kwamba alikuwa na undani wa kukamatwa na ukweli wa sakata zima. Lakini mzee Wassira alipotakiwa kueleza wimbi la utekaji wa watu wakiwamo waandishi wa habari, alikwepa sana swali hilo na kushikilia kuongelea suala lililo mahakamani.

Mzee Wassira anachanganya mambo. Pale anapohisi kushindwa jambo yeye binafsi anadhani ni serikali imeshindwa na kwa hiyo analazimika kutumia hila ili kupata ushindi wa muda na wa bandia usioleta suluhu yoyote. Anapaswa aelewe kuwa udhaifu wa Wassira si udhaifu wa serikali maana serikali si mali yake. Hata pale serikali ya wananchi inapokuwa tayari kukiri kushindwa, Wassira asione nongwa.

Kimsingi, mzee Wassira anapaswa kufikia sasa awe ameishatambua kuwa mitafaruku mikubwa ya kijamii kwa sasa ni katika makundi ya kisiasa, kidini na kiuchumi. Makundi haya ndiyo wadau wakuu wa wizara yake. Misimamo yake binafsi inayokinzana na mitizamo ya makundi haya ndiyo chanzo kikubwa cha kukuza (si kuanzisha) migogoro.

Mzee Wassira anawezaje kukaa meza moja na chama cha CHADEMA ikiwa tayari anaamini chama hicho ni cha kigaidi, cha vurugu na cha kikabila? Anawezaje kukaa na CUF ikiwa anaamini chama hicho ni cha kidini, ni cha uamsho na kiana harakati? Anawezaje kukaa na viongozi wa kiislamu ikiwa anaamini kuwa waislamu ndio wamechoma makanisa na ndio wameua mapadre?

Anawezaje kukaa na kuaminiwa na viongozi wa kikristo ikiwa yeye anaamini tayari kuwa wakristo hawana haki ya kuchinja vitoweo? Tabia yake ya kuja mezani akiwa na majibu tayari kwa mitafaruku inayojitokeza, haiwezi kuboresha mahusiano anayolenga kuyaratibu.

Yeye ni kikwazo tayari kwa makundi anayolenga kuyapatanisha na ni kikwazo pia kwa watendaji serikalini wanaomwona kama mtu asiye na kazi na kuishia kuwaingilia kwenye majukumu yao.

- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/ukitaka-kuboresha-uhusiano-usimtumie-wassira#sthash.SnOr7twi.dpuf
 
Kwangu sioni kosa la Wassira kama wapinzani wasingetoka Bungeni. Wasira alisema vile kwa kuamini kuwa kila kitu kimeenda sawa na masuala yote yataishia bungeni. ila kwa vile wabunge wa upinzani hawajitambui na wamekaa kishari shari, Rais hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuwaita viongozi hao Ikulu
 
Kimsingi CHADEMA ndo wametengeneza mazingira ya kwenda kunywa Juice pale Ikulu
 
wasira sawa na mjane tu ana jipya kule bunda watu wamekosa maendeleo coz yeye
 
Kwangu sioni kosa la Wassira kama wapinzani wasingetoka Bungeni. Wasira alisema vile kwa kuamini kuwa kila kitu kimeenda sawa na masuala yote yataishia bungeni. ila kwa vile wabunge wa upinzani hawajitambui na wamekaa kishari shari, Rais hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuwaita viongozi hao Ikulu
Na hapo ndio kuna hoja yangu , kuwa kama Wassira alisema vile kwa kuona kuwa kila kitu kilienda sawa Bungeni , anapaswa kujiuzulu ili kulinda heshima yake na hadji yake mbele ya jamii.
 
Tuwaache hawa wafu wazikane mpaka siku yao ya mwisho. Wasitupotezee muda kwa umbumbu na uchimvi wao.
 
siku moja Selina kombani aliwahi sema katiba mpya ni hoja ya wapinzani na hiyo haikuwa kwenye ilani yao, kikwete akamuhumbua katiba ikajadiriaka na sasa mswada na sasa wasira ansema ikulu milango imefungwa kikwete kama kawa kamuumbua milango ikafunguka, sasa hawaoni kuwa rais kapitia CCm tu ila nayeye ni CHADEMA damu damu. Kwenye vitu vya kitaifa kama hivi namshukuru kikwete kwakweli anasikiliza hoja na si malipo kama walivya akina wasira na book 7 ya Lumumba.

IKULU ni ofisi ya UMMA na wali siyo ya CCM wala CHADEMA wasira anatakiwa kujifunza hilo.
 
Waziri wa mahusiano na uratibu katika ofisi ya Rais aliwahi kulitangazia taifa kuwa milango ya Ikulu imefungwa na kamwe Wapinzani hawatakuwa tena na nafasi ya kukutana na Rais , na hii ilikuwa mara tu baada ya mabadiliko ya sheria ya mabadiliko ya katiba yaliyokuwa yamepitishwa kibabe na kihuni Bungeni,

Mara baada ya Rais kurejea tarehe 04.10.2013 akihutubia taifa aliomba kukutana na viongozi wa vyama vyenye hoja ambavyo ni Chadema, CUF na NCCR Mageuzi, hii ilikuwa jibu au pigo kubwa kisiasa kwa Waziri Wassira ambaye alishafunga milango ya Ikulu , huku akijua wazi kuwa wajibu wake ulikuwa ni kudumisha mahusiano baina ya ofisi ya Rais na wadau wengine nchini, hakutimiza wajibu wake huo wa kuratibu na kudumisha mahusiano.

Kikwete , ameomba kukutana na viongozi hao tarehe 15.10.2013 Ikulu, ile ile ambayo Wassira alisema milango imefungwa,
hivyo, kutokana na mtiririko huo wa matukio Hayo anapaswa kujiuzulu kwa hiari au Rais amfukuze kazi mara moja maana ameshindwa kutimiza wajibu wake wa kudumisha mahusiano.

Ninatoa wito, kwa Wassira kujiuzulu mara moja kwa ajili ya kulinda heshima yake , asisubiri mpaka afukuzwe kazi na Rais , aidha, kama Rais anataka kuwepo kwa katiba bora ya watanzania , anapaswa kumwajibisha Wassira pamoja na waziri wa sheria na katiba kutokana na matamko yao waliyoyatoa .

Wewe ukisema vijana wenzako wasije kwenu, baba yako anakufukuza nyumbani?
 
siku moja Selina kombani aliwahi sema katiba mpya ni hoja ya wapinzani na hiyo haikuwa kwenye ilani yao, kikwete akamuhumbua katiba ikajadiriaka na sasa mswada na sasa wasira ansema ikulu milango imefungwa kikwete kama kawa kamuumbua milango ikafunguka, sasa hawaoni kuwa rais kapitia CCm tu ila nayeye ni CHADEMA damu damu. Kwenye vitu vya kitaifa kama hivi namshukuru kikwete kwakweli anasikiliza hoja na si malipo kama walivya akina wasira na book 7 ya Lumumba.

IKULU ni ofisi ya UMMA na wali siyo ya CCM wala CHADEMA wasira anatakiwa kujifunza hilo.

ongelea pembeni, unatutemea mate.
 
Kumbu kumbu zangu sijawahi kusikia wasira akisema haya ila mnyika ndiyo anayedai hivyo huu nao ni upotoshaji mkubwa sana.
 
Kimsingi CHADEMA ndo wametengeneza mazingira ya kwenda kunywa Juice pale Ikulu
wengine kama Mbowe, Lipumba hawana ata ndoto ya kuingia ikulu why wakiona upenyo wa kupiga picha za kumbukumbu wanakwenda. kweli upinzani bado sana.
 
Kuna kitu kimewaathiri viongozi we2, labda ni hiki;
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1381399579088.jpg
    uploadfromtaptalk1381399579088.jpg
    15.7 KB · Views: 98
Kimsingi CHADEMA ndo wametengeneza mazingira ya kwenda kunywa Juice pale Ikulu
Watu wenye akili ndogo utawajua tu, yaani mnaona juice ni kitu cha maana saaaana. Si ajabu na wewe ni kiongozi mkubwa serikalini lakini mawazo yako hata mtoto wa Form IV anayaona ya kipuuzi. Tuongozwe na kauli hii: "Taifa kwanza, Vyama baadae."
 
Hivi Ikulu ni mali ya nani? Kama ni ya watanzania wote , hakuna ubaya , ila kama Ikulu ni ya Wassira afunge milango au ajiuzulu kulinda heshima yake .

Mbatia na Lipumba walikuwa hawajanywa Juice, wacha nao wafaidi, Wasira alisema alionya Katiba kutopatikana na kwenye maandamano, na ndicho kilichofanyika kosa lake nini?
 
Kumbu kumbu zangu sijawahi kusikia wasira akisema haya ila mnyika ndiyo anayedai hivyo huu nao ni upotoshaji mkubwa sana.
Jipe muda wa kusoma, kwani nukuu za kauli hii zipo , na hata Wassira alipokuwa kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV aliongelea kauli hizi.........Mnyika anatoka wapi hapo?
 
Back
Top Bottom