Wito wangu kwa vijana juu ya uhuru na uzalendo na mwelekeo wa taifa letu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito wangu kwa vijana juu ya uhuru na uzalendo na mwelekeo wa taifa letu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shayu, Nov 7, 2011.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu, dada na kaka zangu. Naandika nakala hii kutokana na dhamira yangu ya kizalendo juu ya taifa langu na watu wake kwa ujumla.

  Nikiwa mzalendo na raia wa taifa hili. Nina wajibu wa kutoa maoni yangu kuhusu mwelekeo na mustakabali wa taifa letu.
  Mimi sio maarufu miongoni mwa watu wa taifa hili. Lakini naamini mawazo yangu yanaweza kuleta mchango mkubwa kwa taifa hili au kuonya kuhusu mwelekeo ambao tunaelekea kama taifa. Taifa lolote lile hujengwa na watu kutokana na jitihada zao za pamoja katika kujiletea maendeleo yao wenyewe, wakitumia fikra zao katika kujikomboa na kutawala mazingira.

  Hatuwezi kuendelea kama hatutalipenda taifa hili na kujitolea kwa dhati kabisa katika kuliendeleza kwa faida ya vizazi vyetu. Ni ukweli usiopingika binadamu hawezi kufanikiwa katika jambo lolote lile isipokuwa kwanza kutia juhudi na kupenda jambo analolifanya. Ni ukweli usiopingika kabisa kiini cha watu kuishi katika taifa ni umoja bila umoja hakuna taifa. Lazima tuwe tumekusanywa na lengo ambalo sisi kama taifa lazima tulifanikishe. Ikiwa kila mmoja wetu akitia juhudi katika kufanya kazi na katika kufikiri kwa ajili ya manufaa ya taifa tutapiga hatua. Taifa hata siku moja haliwezi kujengwa katika misingi ya ubinafsi ni kinyume na uasilia wa watu kuishi kama taifa na ni kiashiria cha kuporomoka kwa utaifa na madhara yake ni vita na uharibifu.

  Ni Aibu kwa viongozi wetu kusaka uongozi hadi kwa waganga wa kienyeji. Mtu kama huyu hafai kuongoza wananchi, ni mbinafsi na mroho, anataka uongozi kwa faida zake binafsi na anasa.Kiongozi wa kweli ni yule anaye organize watu kutumikia taifa lao wenyewe, sio yule anayetumia nafasi hiyo kujinufaisha na kuishi maisha ya anasa wakati watu wake wakiteseka.

  Tumekuwa taifa lisilokuwa na mwelekeo, wananchi hawajui wanapoelekea, ni nini mission ya taifa? tumekuwa watu wa binafsi na wenye choyo.

  Ubinafsi huondoa mantiki ya watu kuishi katika taifa, kama taifa ni lazima tujue, nini kimetuunganisha na wapi tunataka kuelekea, Kujumuika kwetu kwa pamoja ni ili tuwe na maisha mazuri kuliko haya tuliyo nayo, ili tuishi kwa amani, undugu na upendo, ili kulinda taifa letu dhidi ya maadui wa kigeni.

  Haki za kila mmoja wetu ni muhimu ili kujenga taifa lenye umoja. Tuna taifa ambalo watu wake hawajui wajibu wao kwa nchi yao wenyewe , hii ni hali ya hatari sana. Ni lazima tujenge taifa ambalo vijana watajua wajibu wao kwa taifa, hili ni jambo muhimu sana.

  Taifa huvunjika na kusambaratika kabisa, Tusifikiri kwamba Tutataishi milelele katika nchi hii kama hatukujenga misingi ya umoja na mshikamano wetu. Ni lazima tufikirie upya juu ya ujenzi wa taifa letu na mustakabali wetu kama taifa. Ufisadi hutugawa lakini haki utuleta pamoja, ni ukweli pia taifa lisilo kuwa na malengo ya pamoja watu wake ufikiria ubinafsi, sio utaifa na mwelekeo wa taifa. Ni muhimu kwetu kuamini katika taifa hili, Jukumu la kiongozi yeyote yule makini katika hali tuliyonayo sasa ni kuziondoa akili za watu katika ubinafsi na kuzileta katika utaifa. Watu lazima wajue taifa lao linapoelekea na wanaamini nini kama taifa.

  Taifa imara hujengwa katika umoja na mshikamano wa watu wake na sisi watu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, tulioamua kuwa taifa, tutambue hilo, uwepo wa taifa hili unategemea sana maamuzi yetu tunayoyafanya. Kwahiyo umakini mkubwa unahitajika tunapoongelea masuala yanayohusu taifa letu. Taifa ni kitu ambacho kinavunjika na kusambaratika ili tuendelee kuwa pamoja inabidi umakini mkubwa. Nchi haijiendeshi yenyewe bali huendeshwa na busara za watu wake na viongozi wao. Aina ya taifa hutegemea sana aina ya viongozi tulionao, Ubora au ubovu wa taifa lolote hutegemea busara na akili za viongozi wa taifa hilo. Uchu na tamaa zitatugawa, ni sawa sawa na kukata tawi ulio kalia, tutalisambaratisha taifa hili alafu tuanze kulaumiana. kila mtu anajua hali ilivyo tete ya taifa letu, Watu wachache wanatikisa nchi kwaajili ya ubinafsi wao na kutishia amani shauri ya ufisadi.


  Ninachoona sasa katika taifa letu ni mgawanyiko, wa dhahiri kabisa unaotukana na ubinafsi, ufisadi, utafutaji umaarufu wa kijinga, uwekaji pesa mbele kuliko maslahi ya taifa hasa katika yale mambo ya msingi yanayo tuleta pamoja. tumekuwa wabomoaji wa taifa na sio wajenzi, Vyombo vya habari ambavyo vingetumika kama tool ya kujenga utaifa vimekuwa vyombo vya kisiasa vinavotumiwa kufanya propaganda kwa maslahi ya magenge, Kumekuwa na uhuni mkubwa unaendelea katika taifa letu, Waliopewa dhamana wanaacha kufuatilia mambo ya msingi na kufuata starehe na anasa.

  Kuanguka na kunyanyuka kwa tawala yeyote ile kunategemea sana misingi ya kimaadili na kinidhamu ya taifa hilo, pasipo nidhamu taifa lolote halitoweza kupiga hatua ya kimaendeleo.

  Taifa lisilokuwa na nidhamu ni kama mbegu zilizomwagwa shambani bila mpangilio. haliwezi kuzalisha chochote, mimea itaota na kufa. Utakuwa na watu upande mmoja wanajenga taifa na upande mwingine wanaiba kile tunachokijenga. utakuwa na viongozi wasiowajibika na wafanyakazi wanaofika kazini saa tatu, utakuwa na wabunge wanaochaguliwa vijijini na kuja mjini kustarehe badala ya kuishi na wananchi na kujua matatizo yao na kuyatatua kwa pamoja. Tutakuwa na taifa lisilokuwa na mpangilio wala heshima.

  Hatutaweza kujenga taifa la watu wanaojitolea kwa dhati kwaajili ya ujenzi wa taifa lao wenyewe. Tutazaa watu wabinafsi na mantiki yote ya sisi kuishi kama taifa itafutika, kutokana na huu ufisadi na ubinafsi utatupelekea tupigane vita na taifa tulilolijenga litafutika kabisa. Ni lazima kila mmoja wetu katika taifa hili ajue ana jukumu la dhati kabisa katika ujenzi wa taifa hili, kwasababu majaliwa ya taifa hili ni majaliwa ya kila mmoja .

  Elimu na sheria vina nafasi kubwa sana katika kujenga maadili ya jamii, katika mwelekeo tunaoutaka na katika kubadilisha tabia za watu. ili kujenga raia wema na kuunda taswira ya taifa tunalolihitaji, kulinda utaratibu na muundo mzima wa taifa. Pasipo sheria hatuwezi kuwa na kitu kinachoitwa taifa. ni kama yai na gamba lake.Taifa lisilotii utawala wa sheria kunauwezekano mkubwa taifa hilo likasambaratika. sheria ndizo zinazolinda taifa. Ni jukumu la kila raia kuzitii, Kwani tumejiwekea sisi wenyewe kama mwongozo wetu, zinalinda haki za kila mmoja wetu na mahusiano yetu kama binadamu. Tumeunda mahakama, bunge, polisi nk Lengo letu ni kujenga jamii bora yenye nidhamu na utaratibu, amani yetu itakuwepo ikiwa vyombo hivi vitafanya kazi yake kikamilifu na kwa uaminifu na kwa mashirikiano bila kuangalia vyama bali vikisukumwa na uzalendo na hamu ya kuona taifa hili likiendelea, lazima tutambue sisi ni watu wamoja na lazima tuwe na malengo kama taifa.

  Ni jukumu letu kila mtanzania mzalendo kuamua na kujenga roho ya uzalendo ndani yake na kujifunza kutokana na utumwa waliopitia mababu zetu. Lazima tujiulize ni nini tunajivunia kama taifa? ni kitu gani tunachoweza kusema mbele ya mataifa mengine na kujivunia ? wakati umefika kwa taifa hili kuacha kuendelea kuishi bila malengo, lazima tujitoleee nafsi zetu na maisha yetu kwa ajili ya ukombozi wa taifa hili. Mimi kila wakati naamini kama tutahangaika kwa pamoja, kama tutakuwa wazalendo kwa kulipenda taifa letu na kulitumikia tutafanikiwa, sijaona popote duniani watu walipokuwa na lugha moja na nia moja walifeli katika harakati zao.

  Ni lazima tufanye harakati za ukombozi wa taifa hili. Lazima tutangaze vita, vita ya kulinyanyua taifa hili dhidi ya maadui aliosema mwalimu nyerere, kufikiria uvumbuzi na kuacha kuwa watu wa mizaha na kufuata mambo ya kijinga tuwe wamoja na tujenge taifa letu kwa nguvu moja. Udhaifu wetu unatokana na kutokuwa wamoja kwetu, Umoja katika malengo ndio njia na mkombozi sahihi wa taifa letu. Umaskini wetu unatokana na udhaifu wa viongozi wetu, Ufisadi, ujinga na kutokjitolea kwetu kwa dhati kwaajili ya taifa letu.Naandika leo hii kwenu kama wito wa uzalendo na uhuru. wenye lengo la kuleta mapinduzi. Mapinduzi sio kutoa serikali moja na kuiweka nyingine, mapinduzi ni kuondoa mfumo mzima na kuuweka mwingine. Mfumo wa ufisadi, fitna, ubinafsi choyo na kila takataka. Tujenge nchi yetu katika umoja , uzalendo na kujitolea ili kujenga taifa imara na tishio.

  Tuna wito sasa hivi, wito wa kizalendo utakaopelekea taifa letu kujitegemea. Tunatukanwa kwasababu hatutaka kujitegemea na hili liwe fundisho kwetu tuwe na machungu ya kujitegemea kama taifa ili tuwe na uhuru, ili tuheshimiwe, Hakuna mtu atakaye kuheshimu kama wewe ni ombaomba tutatoka kwa donor mmoja hadi mwingine lakini hakuna hatakaye tuheshimu. Vijana wa taifa hili natumia wakati wangu kuamsha hisia zenu ndani yenu za kizalendo ili mpate mwanga na kulipenda taifa hili nakulitumikia ili kuleta heshima, naongea na nyinyi kwasababu nyinyi ndio wenye nguvu, nyinyi ndio mtakaoleta mapinduzi ya kweli katika taifa letu. Serikali yeyote isiyokuwa na malengo ya kujitegemea kwa taifa letu, isiyokuwa na malengo ya kuleta watu pamoja, isiyokuwa na malengo ya kutumikia wananchi haina budi kutoka madarakani, ili tulete heshima kwa taifa letu. Watu wazalendo wenye hamu ya kuleta maendeleo kwa taifa hili wapo na wenye uchu wa dhati kabisa kwa maendeleo ya taifa. Lazima tujue mwelekeo wa taifa hili na baadae yetu.

  Mapambano yangu sio dhidi ya chama chochote au kikundi chochote cha watu, Mapambano yangu dhidi ya mfumo wa uovu wa rushwa na ufisadi unaoangamiza taifa na umoja wetu, Mapambano yangu ni dhidi ya ubinafsi, ili kuleta umoja na mshikamano wa watu wa taifa hili, ili kuleta mwelekeo na dira kwa taifa letu, ili kuunganisha juhudi katika ukombozi, ili kuleta uzalendo na uhuru wa kweli wenye kujitegemea............Aluta continua!
   
 2. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  ''Aim must be the well being of our country''
   
 3. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  ''
  A house divided within itself can not stand''
   
Loading...