Wito wangu kwa Serikali. Matuta yaondolewe na Barabara zilizopakwa Lami ziwekwe Lami

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Nimekuwa nikipigia sana kelele suala la kuwa na barabara ambazo zimepakwa lami na baadaye kuja wekewa matuta Serikali iziangalie.

Ni mwaka wa tatu huu napata changamoto kila napowaza kununua gari za chini zenye speed.

Ukiangalia barabara nyingi za hapa TZ ni kama barabara za lami.ila watu flani wanapaka lami kwenye barabara na kufanya zionekane kama za lami.hii imesababisha watu wengi kupendelea kununua gari SUV kuliko Saloon.

Serikali pia iangalie uwezekano wa kuondoa matuta barabarani. Yanaharibu sana gari zilizo chini.ziwekwe alama zinazostahili barabarani na camera pia. Mtu asipozitii alama apigwe faini ya 500,000.

Haina haja ya kuharibu umaana wa barabara za lami kwa kuweka matuta sababu tu eti kuna watu hawazingatii alama za barabarani. Mimi nina Int DL. Duniani kote alama zinafahamika ni zile zile. Why muweke matuta tena barabarani? Si sahihi.

Pia serikali ihakikishe hawa wakandarasi watengeneze barabara za lami kweli kweli na si kupaka lami barabarani.siku mbili tu kuna kuwa na mashimo na viraka. Kwa kweli natamani sana niendeshe magari yenye speed ambayo pia yanakuwa chini sana but kwa haya matuta sidhani kama ntaweza fika popote.

Au nilazimike kuwa natembea na winch nikifika kwenye tuta gari inabebwa kuvushwa niendelee na safari.
 
Upo sawa kabisa bwana kidukulilo, kuna maeneo mengi waliyoweka matuta hazina alama yoyote kuonyesha kama mbele kuna tuta, halafu unaweza kuendesha kwenye barabara ya lami mara ukanyage shimo mara ukutane na barabara yenye mawimbi yaani lami imebonyea, sasa kwa sisi tuliobahatika kwenda nchi zilizoendelea ukilinganisha lami yao na hii iliyopakwa kwenye barabara zetu unabaki kusikitika tu...
 
Ila kwakwel matuta barabaran yanazingua aseeee.... Watu tunataka twende 140 to 160
 
Uwepo wa matuta ni ushahidi kwamba jamii yetu haija staarabika. Physical measure kusuluhisha jambo la kutumia akili. Ngoja madaktari wa Mirembe waje watujuze tuko kwenye stage gani ya maradhi ya akili
 
Yanaharibu sana gari zilizo chini.ziwekwe alama zinazostahili barabarani na camera pia.
Yanaharibu hata barabara zenyewe, yanaigharimu nchi kuagiza spare nyingi nje ya nchi, yanaongeza matumizi ya mafuta, yanasababisha ajali nyingi, huwapa shida kubwa abiria wanaokaa viti vya nyuma ya mabasi,
 
Kwa hiyo unaendesha FUSO dunia nzima

Back
Top Bottom