iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Kutokana na hali ilivyo,natoa wito kwa vyama vya siasa,vyama vya kiraia,NGO pamoja na mtu mmoja mmoja.
Ianze kampeni ya mwaka mmoja kupiga kelele katika jumuiya za kimataifa pamoja na taasisi zake kama UN,Benki ya Dunia,IMF,nchi moja moja wafadhili,balozi zote,Amnesty International na taasisi zote zinazofadhili bajeti
Tuwasihi waache kufadhili bajeti kabisa na kuleta misaada yoyote kwa kuwa inawezekana misaada hiyo,mikopo hiyo,ndiyo inawapa nguvu hawa jamaa kuendelea kufanya wanayofanya sasa,wanajua kuna mahali hela zitakuja tu!
Na sisi tuwaambie wafadhili,hela zao zinatuumiza,zinawafanya hawa watu waache kuwajibika,mpaka wanasema hata ije meli moja ni sawa tu,nina imani tukipiga kampeni kubwa,wale jamaa walioenda clouds watajua kuwa wanaelekea kuanguka,wale wa ROMA na Ben,watashinikizwa mpaka kieleweke.
Mambo ya kutumia hela(labda na za wafadhili)kumpa lipumba yatakwisha
Hata bunge na mahakama zitaheshimiwa na sio kupewa bajeti za nipe nikupe.
Mikutano ya kisasa itaheshimiwa na kuruhusiwa,kamata kamata ya viongozi itakwisha
Nadhani hii kampeni itasaidia na ni vizuri ianze mara moja kabla hali haijaharibika,mpaka sasa ni dhahiri bunge limeshindwa kuidhibiti serikali kuhusu matukio yanayoendelea
Na upande wa mahakama,ni kama kaimu jaji mkuu kategeshewa,hajathibitishwa kazini,na hakuna sababu,hivyo naye tunamuona hayuko Uhuru kufanya maamuzi sawasawa mpaka athibitishwe kazini
Kilichobaki ni kuongea na jumuiya za kimataifa tu,hapo awali iliwezekana,hata sasa inawezekana