Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Feb 2, 2012.

 1. P

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 22,220
  Likes Received: 10,308
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Kitendo kilichofanywa na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai, hakiwezi kuachwa hivi hivi, hivyo natoa wito kwa wabunge wetu, wenye mapenzi mema na taifa hili, kuanzisha vuguvugu la kuzifumua kananuni zote zinazompa spika/ naibu spika mwanya wa kuliendesha bunge kwa udikteta kadri nafsi zao zinavyoona inafaa!

  Hakuna ubishi kuwa Mhe. Makinda kama spika, kuna wakati analiendesha bunge kidikteta ila udikteta wa Makinda unatokana na mazingira na hulka.

  Mazingira ni kwa vile kaupata uspika kutokana na jinsia yake na sio kutokana na uwezo hivyo to prove she is able lazima aonyeshe uwezo.

  Kwa upande wa hulka yeye Mama Makinda ni emotional na hot tempered lady hivyo anakuwa easly provoked hivyo kupandisha hasira kirahisi na kutoa maamuzi ya kidikteta huku akiyatetea kwa hoja japo nyingine ni dhaifu!.

  Ila huyu Naibu Spika Mhe. Job Ndungai yeye ni mtu mtulivu, makini na mtaratibu sana ila ndie dikteta mbaya zaidi kuliko Mama makinda kama alivyo simba mwenda kimya!.

  Hili nimelishuhudia leo bungeni wakati akiizima hoja ya dharura ya kuujadili mgomo wa madaktari kwa dharura iliyoibuliwa na wabunge wawili akiwemo Mhe. JJ Mnyika.

  Hoja imeombwa kwa kifungu no. 47 ambapo Dugai akaizima hivi hivi juu kwa kwa juu kwa macho makavu kabisa bila hata blink ya jicho kuwa hoja hiyo haikuungwa mkono!. Kitendo tuu cha kuibuliwa na wageshimiwa wabunge wawili kwa mpigo ni kuungwa mkono tosha, alitaka mpaka iungwe mkono na wabunge wangapi!.

  Hivi seriousness ya mgomo wa madaktari inahitaji uungwaji wa mkono wa aina gani kuonyesha ni dharura!.

  Mhe. Ndugai na smilling face yake ndio type ya wale ambao wana ku stab on your face infront huku anasmile as if nothing happened, wakati kwa kawaida stab hufanywa on your back!.

  Wabunge wetu hakikisheni mnajenga hoja ya kubadili kanuni ili kuzuia madikteta wa type ya Ndugai na Mama Makinda wasiabuse powers vested on them na kanuni!.

  Kwa yanayotekea bungeni sasa, yananifanya nimkumbuke sana Spika Sitta, kulikuwa hakuna ujinga ujinga kama huu tunaoushudia sasa.

  Paskali
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 34,644
  Likes Received: 11,570
  Trophy Points: 280
  labda kapewa maelezo toka juu?
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Pasco nakubalina na wewe kabisa. Sikuamini hata chembe kama Ndugai anaweza kusema aliyosema. Watanzania ni kama tuko yatima. wawakilishi wametugeuka. Cha kuhuzunisha ni pale Ndugai alipokubali kwamba hoja iliyotolewa kweli ina ya msingi na ina maslahi kwa wananchi, sasa kwa nini akatae isijadiliwe? Mimi nadhani Spika ameshatoa maelekezo mgomo wa madaktari usijadiliwe. Hatuna bunge maana bunge la Makinda liko chini ya serikali. Spika na naibu wake wamekuwa wasemaji wa serikali.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,701
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  walishaambiwa hao mkuu wasijadili suala la mgomo wa madaktari kwa sababu upo mikononi mwa raisi kwa sasa!
   
 5. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,216
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndio maanake, yaani kile kitendo sijakifurahia hata kidogo.
   
 6. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye red ndio unapokosea, wabunge wanawatumikia waliowapatia posho ya siku 200,000/=.
   
 7. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 5,614
  Likes Received: 1,109
  Trophy Points: 280
  Hilo litawezekana iwapo wabunge wa CCM wataamua kukaidi maagizo wanayopewa na chama kwa maslahi ya chama
   
 8. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,163
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Katika hili nakuunga mkono Pasco bunge kwa sasa linaendeshwa kitemi na udikteta unaoongozwa na Makinda na mwenzie Ndungai. Bunge letu limepoteza mwelekeo sio tena bunge la kumtetea mwananchi, inasikitisha kuona kwa sasa hatuna tena watetezi. Imenitia hasira sana
   
 9. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,708
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  wao haiwagusi kwani wakiumwa wanakwenda apollo ingekuwa madaktari wa apollo wamegoma ungeona kelele zake wangeongea hadi mapovu ya watoke mdomoni lakini kwa sababu muhimbili ni ya walala hoi wao kwao ni uchafu haiwagusi hivyo kuizima ni kawaida, ila wakumbuke one day yes watajua kuwa watanzania ni watu waina gani..... kwani kwa mbali naona makundi yanasogea kuipinga serikali yetu midundo ya ngoma na sauti za walala hoi wasiokuwa na matumaini na serikali yao inakuja wako kwambaliiiiii.....
   
 10. nanchi

  nanchi Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nimelitafakari hili suala la mgomo wa madaktari na kile kinachoendelea ndani ya serikal na uongozi wa juu wa bunge,ni dhahiri serikali inaonyesha kuwa ni mpango wa kutupunguza watanzania tulio zaid ml 45 angalau kufikia ml 20 wakiamini ndio idadi wanayoweza kuimudu.ni hatari kwa taifa na inasikitisha sana ndugu zangu.ila hili ni bomu likifikia kulipuka litalipuka tu.
   
 11. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wataanzisha vuguvugu wapi? bado bunge lina watu wale wale akina Juma Nkamia wataunga mkono hoja?
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,467
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Tunaiondoaje SERIKALI Bungeni? Ukiondoa Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar wengine wote waliobaki kwenye CABINET ni WABUNGE au sehemu ya Bunge. KATIBA yetu ya JMT imetufikisha hapa. Mbaya zaidi SPIKA ni mjumbe wa CC ya CCM. Katika hali kama hii BUNGE litabaki kuwa hivo lilivo hadi tupate katiba mpya yenye akili.
   
 13. MLATIE

  MLATIE Senior Member

  #13
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 170
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  linatakiwa lilipuke sio lita maana tumechoka
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 8,559
  Likes Received: 2,166
  Trophy Points: 280
  Jamani rais wetu ni mtaalmu wa mazishi na kutembelea wagonjwa , hivyo huu mgomo una maslahi kwani wanapokufa watu wengi atakuwa anaitumia vema taaluma yake.
   
 15. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 11,367
  Likes Received: 2,784
  Trophy Points: 280
  Vyema mzee.
  Kwa katiba hii inayotumika, ni vigumu sana kwa wabunge kubadili kanuni hizo kama anavyoshauri mzee Pasco.
   
 16. m

  mtolewa Senior Member

  #16
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu tatizo sio kanuni,makinda,ndugai au ccm hapa tuwe wakweli tu wabunge wengine wote wa cdm waliokuwa bungeni leo isipokuwa mnyika ambaye alianzisha hoja hawakusimama kuunga mkono hoja.wabunge wa cdm tuna mkataba nao sisi wanyonge kwa nini hawkuunga mkono? naomba majibu kutoka kwa hawa ambao niliwaona wakiwa bungeni.l.nyerere,sugu,mdee,kahigi.wengine akina lema ,wenje,msigwa,zito,arthi na silinde sikumbuki kuwaona bungeni leo.mnyika,ukiwa kama kiongozi wao toa taarifa na hatua watakazochukuliwa,wamekiabisha chma na kusaliti maslahi ya wanyonge.
   
 17. t

  taranda Member

  #17
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona makamba jr alivoibua ishu ya mafuta kwa mtindo wa dharura hakuna wabunge waliosmama na palepale mjadala ukaanza. Hii ya leo ni usanii mtupu
   
 18. W

  We know next JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa ukweli, Naibu spika nadhani alikuwa tayari kabisa kulifanya jambo hili lizungumzwe. Lakini kwa vile taratibu hazikufuatwa za wabunge kusimama na kuunga mkono, ndiyo maana akasema hivyo. Lakini pia ikubukwe kuwa, wabunge wote wa CCM wameshapigwa stop kuliongelea hilo mpaka Serikali yao iliyoshindwa kazi itoe tamko. Lakini kama ulimsikiliza Ndugai, mwishoni alisema, Misri ambako wabunge walikuwa likizo, jana mara baada ya kutokea mauaji ya watu zaidi ya 75 ktk uwanja wa mpira, Bunge limeitwa kwa ajili ya kuja kudiscuss issue hiyo tu. Nadhani alikuwa anaonyesha wazi kuto kukubaliana na wakubwa wake. Lakini akasema mpaka kesho kama Serikali haijatoa taarifa, ataliwasha bungeni kesho.
   
 19. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,837
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 0
  Wabunge njaa unategemea wajadiri jinsi wapiga kura wao wanavyo jinyea mahospitalini kwa kukosa huduma thubutu
   
 20. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 8,559
  Likes Received: 2,166
  Trophy Points: 280
  Pasco usitegemee wabunge hawa hawa wanaolilia posho na wameongezewa hadi 200,000/- watatia neno.Hawa wanafikiri kwa kutumia matumbo mkuu.
   
Loading...