Wito wa mpito kwa DPP: Wakili aliyemwandaa ACP Kingai aondolewe jopo la Mashtaka la akina Mbowe

Siku zote ukweli ni mfupi na uongo ni mrefu.na hii serikali isiposoma alama za nyakati hii kesi itawaweka pabaya sana uko mbele.Zama zimebadilika.
 
Stupid, sentensi hiyo ina maana maelezo yale are cooked by Kingai and not extracted from the suspect. Stupid hujui lolote
Sasa wewe unayejua sheria mbona unahamaki na kutukana! Kwa mwenendo huu wa kutukana badala ya hoja ni kwamba ushindi wako unategemea hisani ya jaji na maagizo yaliyoandaliwa toka juu.
 
... exactly! You have nailed it! Na ndio maana mkamataji hatakiwi kuwa mchukua maelezo! One of the biggest mistakes ever!
Credibility of the witness tainted with lies; an impatial Judge will right away arrive at that conclusion and the whole lot will be expanged from record
 
Anajificha kwa wanawake huko, na kuwajaza ujina wake, ili tukilitimua liseme .. kina mama tukatae mfumo Dume.
Mtamtimua wapi ?!!!

Yaanj ninyi CHADEMA mumtimue mwenyekiti wa CCM ?!!!Khaaaa 😲😲🤣🤣🤣

Endelea kuota juani.....

#SiempreJMT
 
Means maelezo Yale aliyatunga mwenyewe from his head or cooked from his head ànd not from the suspect. Do you mean that?
Halafu pia alijichanganya sana pale wakili msomi Mtobesya alipomchanganya na vifungu vya sheria kisha akamuuliza kuwa alichukua maelezo kwa mujibu wa vifungu vya sheria au alitumia tu uzoefu, halafu ACP Kingai akajichanganya na kusema kuwa alitumia tu uzoefu kwa sababu alishajua kama akisema kuwa alitumia kifungu cha sheria ataambiwa akitaje wakati hakijui.

Kisha wakili msomi Mtobesya akakaa chini fasta kwa sababu alishajua kuwa amemaliza jambo lake vizuri.
 
Mkitaka kutunga uongo ni lazima waongo wote mkusanyike pamoja sehemu moja, hamuwezi kutunga uongo kwa kutumia simu ambazo nazo zimechanganyikiwa kwa uongo wa kila aina na ni kila siku.
Madawa ya kulevya yameingizwa ili kukazia uwezo wa kukata miti kuanzia Dar mpaka Mbeya, kwani bila bangi hauwezi hata kufika Kimara.
Yaani hiki ni kituko cha mwaka. Unakata miti ili kuzuia njia! Kigai kweli hana akili huyu.
 
Sema manjagu wajanja wakitaka kukutoa sadaka wanakutoa kwenye hizi kesi...huyo jamaa hana uwezo wa kusimama kutoa ushahidi kwa kesi za janja janja amelitia aibu Taifa...
 
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi. Sikwenda pale kwa minajiri ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Nilikwenda kufuatilia mambo ya mwanangu anayesoma pale Law School of Tanzania. Kwakuwa nilimaliza kilichonipeleka mapema na niliwaona hata marafiki zangu wakijumuika kuhudhuria kesi ya akina Mbowe, niliamua kujumuika nao. Ni katika viunga hivyohivyo vya Law School of Tanzania.

Jana, upande wa Mashtaka (Jamhuri) ilianza kuleta mashahidi. Shahidi wa kwanza, na nilishajua na kumtegemea, akawa ni ACP Ramadhani Kingai ambaye kwasasa ni RPC wa Kinondoni. Kama shahidi wa kwanza na wa muhimu wa Jamhuri, Kingai alieleza mengi kwenye kesi ya msingi na hata kwenye kesi ndogo iliyoibuka baada ya mapingamizi yaliyotolewa na upande wa Utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili Msomi Kibatala.

Katika uga wa kisheria, shahidi yeyote huandaliwa na Wakili anayemleta mahakamani. Kuandaliwa si kufundishwa cha kusema ila ni kuunda mtiririko na mueleweko wa ushahidi wa shahidi husika. Pia, maadalizi hujumuisha upembuzi wa kipi cha kuanza; kipi cha kumalizia; kipi cha kusemwa na kipi cha kutokusema mahakamani kwenye kesi husika. Hata ACP Kingai aliandaliwa na Wakili au Mawakili wa Jopo la Mashtaka.

Kuna mambo ya wazi kabisa ambayo yameleta mkanganyiko badala ya muunganiko kwenye ushahidi wa Kingai. Mkanganyiko usio na tija. Kuhusu mtiririko wa matukio; kilichotokea na kilichofanyika na polisi. Nitatoa mifano michache kwakuwa mambo yenye mkanganyiko yalikuwa mengi mno. Kwanza, Kingai hakutaja kwenye ushahidi wake kuhusu watuhumiwa kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni. Aliishia kusema walifikishwa Central Dar. Kwanini hakuandaliwa kuhusu hilo?

Pili, Kingai amesema kuwa watuhumiwa walikutwa na bastola moja na risasi tatu. Ni tofauti na Hati ya Mashtaka inayotaja risasi moja. Tatu, amezungumzia watuhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya. Kwanini hakuandaliwa kuacha kuzungumzia kitu kisicho sehemu ya mashtaka ya akina Mbowe? Nne, Kingai amesema kuwa alipokuwa akiongoza timu ya upelelezi na ukamataji alikuwa Regional Criminal Officer (RCO) wa Arusha. Hakuandaliwa kueleza kwanini alifanyia kazi mikoa ya wengine kwenye ma-RCO na askari wengine?

Au Kingai naye alikuwa Sabaya wa pili? Tena, Kingai ameeleza kuwa kuna mashahidi walichukuliwa maelezo yao Moshi. Hapohapo akasema watuhumiwa walichukuliwa maelezo yao Dar es Salaam kwakuwa ndiko jalada lilipokuwa limefunguliwa. Kwanini wahusika wa jambo moja watofautishwe mahali pa kuchukuliwa maelezo yao? Hapa pia hakuandaliwa vyema. Kingai amefanya kadiri ya uwezo wake kuelezea. Lakini, hakuandaliwa vyema.

Halafu, kama mkamataji hakupaswa kushiriki kwenye kuwachukua maelezo washtakiwa. Hivi Wakili aliyemwandaa hakulijua hata hilo? Maana Kingai amekuwa akirudiarudia mahakamani kuwa aliwachukua maelezo washtakiwa ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewakamata. Kufanya hivyo si kuandika stori yake mwenyewe anayetaka wengine waiamini na kumpongeza kwa uandishi wa stori tamu kuwahusu washtakiwa?

DPP Mwakitalu, chukua hatua mapema. Ondoa Wakili au Mawakili waliomuandaa Kingai. Kama Kingai amejikanyaga vile, watakaofuata wataanika madudu mapya na yakutisha zaidi.

Chief Hangaya, nasi tuanze kampeni chamani?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Ahsante Mzee Vuta ni kuvute. Hiyo Kesi imeandaliwa na Serikali ya Chama tawala. Je huko Chamani hii ndio Sera na Ilani yenu ya Uchaguzi kubambika watu Kesi, na Kuvielekeza vyombo vya Dola kuwaisaidia?

Au ndio utekelezaji ya yule aliyesema "Tutatumia Dola Kubaki Madarakani"?
 
Mijadala ya great thinkers nakushauri uwe unasoma tu bila kuchangia kitu. Maana hapo ndipo unapochemka kuuficha ujinga wako....

Yani hata logic ndogo tu kwenye hoja ya jamaa hujaielewa? Kwani shuleni ulienda kusomea ujinga?
Anatafuta ute UZI. Mjinga sana anajiona anachangia uharo baada ya kusoma hoja zenye afya.
 
Sasa wewe unayejua sheria mbona unahamaki na kutukana! Kwa mwenendo huu wa kutukana badala ya hoja ni kwamba ushindi wako unategemea hisani ya jaji na maagizo yaliyoandaliwa toka juu.
Nani kasema anajua Sheria. This is common sense, instinctive. You use your intuition man!
 
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi. Sikwenda pale kwa minajiri ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Nilikwenda kufuatilia mambo ya mwanangu anayesoma pale Law School of Tanzania. Kwakuwa nilimaliza kilichonipeleka mapema na niliwaona hata marafiki zangu wakijumuika kuhudhuria kesi ya akina Mbowe, niliamua kujumuika nao. Ni katika viunga hivyohivyo vya Law School of Tanzania.

Jana, upande wa Mashtaka (Jamhuri) ilianza kuleta mashahidi. Shahidi wa kwanza, na nilishajua na kumtegemea, akawa ni ACP Ramadhani Kingai ambaye kwasasa ni RPC wa Kinondoni. Kama shahidi wa kwanza na wa muhimu wa Jamhuri, Kingai alieleza mengi kwenye kesi ya msingi na hata kwenye kesi ndogo iliyoibuka baada ya mapingamizi yaliyotolewa na upande wa Utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili Msomi Kibatala.

Katika uga wa kisheria, shahidi yeyote huandaliwa na Wakili anayemleta mahakamani. Kuandaliwa si kufundishwa cha kusema ila ni kuunda mtiririko na mueleweko wa ushahidi wa shahidi husika. Pia, maadalizi hujumuisha upembuzi wa kipi cha kuanza; kipi cha kumalizia; kipi cha kusemwa na kipi cha kutokusema mahakamani kwenye kesi husika. Hata ACP Kingai aliandaliwa na Wakili au Mawakili wa Jopo la Mashtaka.

Kuna mambo ya wazi kabisa ambayo yameleta mkanganyiko badala ya muunganiko kwenye ushahidi wa Kingai. Mkanganyiko usio na tija. Kuhusu mtiririko wa matukio; kilichotokea na kilichofanyika na polisi. Nitatoa mifano michache kwakuwa mambo yenye mkanganyiko yalikuwa mengi mno. Kwanza, Kingai hakutaja kwenye ushahidi wake kuhusu watuhumiwa kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni. Aliishia kusema walifikishwa Central Dar. Kwanini hakuandaliwa kuhusu hilo?

Pili, Kingai amesema kuwa watuhumiwa walikutwa na bastola moja na risasi tatu. Ni tofauti na Hati ya Mashtaka inayotaja risasi moja. Tatu, amezungumzia watuhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya. Kwanini hakuandaliwa kuacha kuzungumzia kitu kisicho sehemu ya mashtaka ya akina Mbowe? Nne, Kingai amesema kuwa alipokuwa akiongoza timu ya upelelezi na ukamataji alikuwa Regional Criminal Officer (RCO) wa Arusha. Hakuandaliwa kueleza kwanini alifanyia kazi mikoa ya wengine kwenye ma-RCO na askari wengine?

Au Kingai naye alikuwa Sabaya wa pili? Tena, Kingai ameeleza kuwa kuna mashahidi walichukuliwa maelezo yao Moshi. Hapohapo akasema watuhumiwa walichukuliwa maelezo yao Dar es Salaam kwakuwa ndiko jalada lilipokuwa limefunguliwa. Kwanini wahusika wa jambo moja watofautishwe mahali pa kuchukuliwa maelezo yao? Hapa pia hakuandaliwa vyema. Kingai amefanya kadiri ya uwezo wake kuelezea. Lakini, hakuandaliwa vyema.

Halafu, kama mkamataji hakupaswa kushiriki kwenye kuwachukua maelezo washtakiwa. Hivi Wakili aliyemwandaa hakulijua hata hilo? Maana Kingai amekuwa akirudiarudia mahakamani kuwa aliwachukua maelezo washtakiwa ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewakamata. Kufanya hivyo si kuandika stori yake mwenyewe anayetaka wengine waiamini na kumpongeza kwa uandishi wa stori tamu kuwahusu washtakiwa?

DPP Mwakitalu, chukua hatua mapema. Ondoa Wakili au Mawakili waliomuandaa Kingai. Kama Kingai amejikanyaga vile, watakaofuata wataanika madudu mapya na yakutisha zaidi.

Chief Hangaya, nasi tuanze kampeni chamani?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Shida ni kwamba, uongo mmoja huitaji uwongo kumi kuulinda usijulikane... na hayo mauwongo kuna nayo kila mmoja huitaji kumi mengine.. HAPO NDO PENYE KAZI KUBWA
 
Back
Top Bottom