Wito wa maandamano na mkutano wa chadema kwa wakazi wa dsm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito wa maandamano na mkutano wa chadema kwa wakazi wa dsm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, May 25, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Napenda kuwajulisha kuwa kutakuwa na maandamano kutoka sehemu na vitongaji mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam na kuishia katika viwanja vya JANGWANI, siku ya Jumamosi, Tarehe 26 Mei, 2012. Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar, kutoka katika matawi yao mbalimbali wataandamana kuelekea katika viwanja vya Jangwani. Wanatakiwa kufika katika viwanja hivyo saa NANE mchana ambapo shughuli rasmi zitaanza katika viwanja hivyo.

  Maandamano hayo na Mkutano huo una malengo makubwa mawili:

  1) Kuzindua kampeni ya Kitaifa ya Movement for change

  2) Kutoa muelekeo wa mchakato wa katiba

  Pia kutakuwa na malengo mengine yatakayoendana malengo makubwa hayo mawili kama vile Vua gamba Vaa Gwanda. n.k.

  Ombi: Tunawaomba wote muhudhurie bila kukosa na mshiriki katika kuleta mabadiliko na ukombozi wa mara ya pili ambao ndio njia pekee ya kututoa hapa tulipo. Aidha tunaomba mfikishe salaam hizi kwa yoyote yule mpenda mabadiliko, maendeleo, ustawi na amani. Karibuni wote. Hii ni fursa yetu wana Darisalama, kuonyesha kuwa kweli sasa tunaleta ukombozi wa mara ya pili.

  Mkutano huu utahudhuriwa na viongozi wote wa kitaifa na viongozi wengine waandamizi. Vyombo vya habari navyo vitakuwepo ikiwa ni pamoja na kurushwa kwa tukio hili moja kwa moja yaani live. Lakini ni muhimu kuhudhurie ili tuweze kukikomboa kizazi hiki na kizazi kijacho kutokana na uzembe, ufisadi, rushwa na kukosekana uwajibikaji.

  Nawashukuru sana na karibuni sana kesho.

  Imetolewa na Selemani Rehani
   
Loading...