Wito wa Maandamano makubwa kulaani Serikali kushindwa kuleta maji ya uhakika kwa miaka 60

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,090
Hivi hii serikali ya CCM iko madarakani kwa Uhalali upi?

Miaka 60 ya Uhuru imepiga marktime na kufanya mambo mengi yasiyo ya maana na kuacha mengi ya maana.

1. Hivi Wakati Serikali ya CCM inavumilia ufisadi wa EPA , Rada Meremeta, Kagoda, Richmondi Ndege ya Rais, hizo pesa zisingeweza kusaidia kuondoa kero ya maji kwa wananchi?

2. Hivi ma V8, Mamisafara makubwa, maposho manene wanayolipana yasingeweza kisaidia kuondoa shida ya maji kwa wananchi?

3. Wanakimbiza Mwenge, Wanalipa wastaafu hadi asilimia 80% ya mishahara ya viongozi walioko madarakani, hizo pesa zisingeweza kuondoa kero ya maji ya wananchi?

4. Tumezunguukwa na maziwa makubwa, tuna mito mikubwa, tuna bahari. Hizi serikali za CCM toka mwaka 1961 zimeshindwaje kutatua kero ya maji kwa wananchi?

5. Wanafanya mamiradi makubwa kabla ya kusolve matatizo ya maji, wanajenga uwanja wa ndege Chato, Daraja la kupita baharini Dar, Wakati wananchi hawana maji

6. Wanawalipa Syimbion, shilingi bilioni 300 kwa mkataba wa kihuni ulioingiwa tena kiujanjaujanja wakati mkataba wa awali ulikuwa umeshaisha!

7. Walihonga watu waunge mkono juhudi, ili majimbo yao yawe wazi kisha zitumike pesa za umma kurudia tena chaguzi. Mapesa haya ya wananchi yangesaidia kuondoa kero ya maji

8. Wanatumia mabilioni kulipa wabunge hewa, waliobungeni kinyume cha katiba. Hizo pesa zingesaidia kuondoa kero ya maji

Kwa hakika Watanzania tumechoka na Ujinga, Ukosefu wa maono, Ubinafsi na kukosewa heshima na serikali hii ya CCM.

Wametufikisha katika hatua sasa ya kutufanya tuamke, tusimame, tupambane nayo kwa hali na mali, kwa jasho na machozi kwa kuwa sasa imegeuka kuwa serikali dhalimu, isiyotosheleza haja zetu!

Sasa tunatangaza kuanza maandamano yasiyo na kikomo, kuitaka serikali hii ilete maji, kama haitoleta maji tutayafuata kwa Mawaziri, wao hawakosi maji

Kama haitoleta maji tutayafuata Ikulu, huko nasikia yako mengi hayakatiki.

Haiwezekani tukaendekeza upumbavu huu

Kama hamuwezi kutatua shida ya maji ondokeni, Tokeni madarakani. Hamna legitimacy tena ya kuitwa serikali au viongozi.

Serikali gani nyinyi, hamuwezi chochote. Nyambaafu!

Failure wakubwa nyinyi!.
 
Kabla ya kuwaza hayo
Jiulize wewe kama mwananchi unafursa ya kuanzisha kampuni kubwa ya kusambaza maji mijini na vijijini je umefanya hivyo au your talent is for waste haya matatizo ya maji ni fursa sie wamiliki wa visima vidogo tunaouzia watu maji tunatamani shida iendelee na pia tunatamani kutambulika ili tupate mikopo mikubwa tusambaze maji kwa watu wengi ikiwezekana mji mzima hii ndio maana ya kuwa mwananchi serikali ituweke sera na kubadili sheria za kuzibeba mamlaka mbalimbali za maji inazomiliki kama vile kwenye mitandao ya simu na redio iweke uwanja sawa iseme ruksa watu binafsi kusambaza maji safi ila kampuni zisajiliwe na zilipe kodi tumalize hili tatizo kwa watanzania ndani ya mwaka maji yatasambaaa kila kijiji.
 
Kabla ya kuwaza hayo
Jiulize wewe kama mwananchi unafursa ya kuanzisha kampuni kubwa ya kusambaza maji mijini na vijijini je umefanya hivyo au your talent...
Umetoa mawazo mazuri lakini huoni bado serikali ni ya kishenzi kila mwaka mambo ni zimamoto? Kwanini hawaondoi kero kila mwaka sababu ni zilezike za kijima.

Mimi pia ni mmojawapo ninapiga pesa kwangu kwa kuwa nina kisima na nimefunga mashine ya kufanya desalination, lakini watu wanaumia kwelikweli.
 
Utachapwa kipigo cha mbwa koko, jaribu uone. Acheni ulimbukeni. CCM haihusiki na mambo ya maji maana kila kona ya dunia kuna uhaba wa maji na mvua
 
Tuandamane kisa kwenu hakuna maji?

Bora walau ungesema sukari ipo juu hii hata mimi ninayekaa pembezon mwa vijito ningeshawishi watu.
 
Back
Top Bottom