Wito wa kunga mkono vuguvuvu la "mapinduzi ya kizalendo " kuanza tarehe 19/02/2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito wa kunga mkono vuguvuvu la "mapinduzi ya kizalendo " kuanza tarehe 19/02/2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by saggy, Feb 16, 2011.

 1. s

  saggy Senior Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  WAKATI NI SASA HAKUNA KUNGOJA!!!!

  Mimi nasema hawa WATOKE ni WAONGO na wametusaliti wananchi na wamekalia maneno tu,nasema Watupishe watokee,nimechoka ,Dunia nzima imechoka na SISI TANZANIA Kwanini TUNALALA UZINGIZI ,Mabadiliko ya Katiba sawa lakini ni kifungu gani cha Katiba ya sasa kinawaruhusu kula Rushwa,kuingia Mikataba Mibovu na etc.Thats why nasema hatutangoja kuandikwa katiba Mpya iandikwe ndipo tufanye mapinduzi,WAKATI NI SASA

  Dawa yao ni Kuwaondoa madarakani kwa Maandamano makubwa kama walivyofanya Wenzetu,leo nasema nimechoka na ,how LONG WE WILL WAIT? Tungoje katiba kuandikwa lini?

  1.Watoto zaidi ya 250,000 walipata daraja la IV na 0 kwenye Mitihani yao ya Kidato cha nne mwaka huu kutokana na kupata Elimu duni kwenye shule za kata wangoje mapaka lini?

  2.Mamilioni ya Vijana wasio na AJIRA Wanaolala na hawajua maisha yao yatakuwaje nao wangoje mpaka Katiba iandikwe?

  3.Wakulima wasio na masoko ya uhakika na Pembejeo za kilimo,wakifa kwa kukosa hduma muhimu vijijini kama Afya,Elimu na Maji wangoje mpaka lini?

  4. Maelfu ya akina mama zetu waja wazito wanaokufa kwa kukosa Huduma bora za Afya wakati wa Kujifungua wangoje mpaka lini?

  5.Walimu ,wahadhiri wa Vyuo vikuu wanaolipwa mishahara midogo,mazingira duni ya kazi na mdai yao kutolipwa kwa muda mrefu wangoje mapaka lini?

  6.Mgao wa umeme unaondelea sasa uliosababisha Mfumuko wa Bei na kupunguza uzalishaji wa Taifa na kutuingiza kwenye umasikini mkubwa,Viwanda zaidi ya 50 kuelekea kufungwa na hivyo kutonesha donda ndugu la ukosefu wa Ajira,tungoje Katiba mpya kuandikwa hata lini ili haya yapate ufumbuzi,hata lini?

  7.Wanafunzi wa Vyo vya Elimu ya Juu wanaoteseka na kuhangaika kwakuwa Pesa ya kujikimu haitoshi na mazingira magumu ya kusomea na hawana uhakika wakimaliza watapata Ajira au la Wangoje mpaka lini?

  8.Polisi,askari magereza wanaoishi maisha ya dhiki ,hawana makazi bora ya kuishi,angalia pale Misimbazi na kwingineko Tanzania,angalia mishahara yao,wao wanajua wanapataje,nao wangoje mpaka lini kuendelea kuteseka?

  9.Wachimbaji wadogo wanaofukuzwa kwenye Migodi ndani ya Ardhi yao Tanzania na kupiga myayo jirani huku wakishuhudia ndege zikipaa na kushuka kwenye migodi yao na kuondoka na mali yao wangoje mpaka lini?

  10.Tungoje Tume huru ya Uchaguzi ndipo MAGEUZI yafanyike,hatutangoja hata siku moja.


  Nasema tarehe 19/02/2011 ndio mwanzo wa vuguvugu la Mapinduzi ya kulikomboa Taifa letu,leo mataifa ya Kiarabu wameamka na kudais Ukombozi sisi Watanzania tunalala USINGIZI kama kumeridhika na matatizo haya yote?


  Maandamano kuanza katika Mikoa ya Dar es salaam,Mwanza,Arusha,Kigoma,Mbeya na Mara kwa kuanzia na baadaye nchi nzima kwa mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani.


  Mapinduzi haya si chama fulani ni ya WAZALENDO WA TANZANIA.

  Sime wote,sisi ndio Dola,vyombo vyetu vya Dola hakikisheni mnakuwepo kwakuwa na ninyi nia WAZALENDO WA TANZANIA.


  SHIME WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYOTE KATIKA MIKOA NILIYOTAJA,NATUMAINI SISI NDIO CHACHU YA MAGEUZI YA TANZANIA


  WAKATI NI SASA,HAKUNA KUNGOJA!!!
   
 2. s

  saggy Senior Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa Tarehe na maudhui vimebadilika na itakuwa Tarehe 9/07/2011

  Maudhui ni yala yale PLUS Mgao wa Umeme

  Yataanzia Viwanja vya Maonyesho ya Sabasaba Nchi Nzima na kwa Dar es salaam yataanzia pale Saba saba kwenye Banda la Wizara ya Nishati na Madini kila siku Jioni saa kumi na kuzunguka Mabanda yote.Tusibebe silaha yoyote please ni maandamano ya amani,Tarehe 7/07/2011 kutakuwa na maandamano Mkubwa zaidi Nchi nzima na hakutakuwa na Sherehe za Sabasaba kama ilivyozoeleka Miaka yote,hili halitafanyika kama hatua za haraka za kupunguza makali ya mgao zitachukuliwa kabla ya Tarehe 9/07/2011. Na kama hatua hazitachukuliwa Mandamano Makubwa yatafanyika siku ya tarehe 9/12/2011 ili kusherekea Uhuru wa TAIFA letu na kuwasilisha malalamiko yetu
   
 3. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bado ni ndoto, altenative hii bado saana.
   
Loading...