Elections 2010 Wito wa kukamatwa kwa mnajimu

MWANA WA UFALME

JF-Expert Member
Sep 10, 2010
578
144
Yule mnajimu aliyetishia nchi nzima kwamba uchaguzi utaahirishwa na kwamba kuna mgombea atakufa anahitaji kukamatwa mara moja kwa tuhuma za uchochezi na kutishia watu.

Alichokifanya ni mauaji ya maneno au kisaikolojia na hivyo watu kama hawa hawapasi kuachiwa hivi hivi maana ni hatari kwa amani, haki na ustawi wa taifa.
 
Yaani rasilimali za umma zitumike kumkamata mjinga mjinga kama huyo? You cant legislate stupidity. Just let him be
 
Huyo mnajimu anapanda chati kwa makosa ya waandishi wa habari na watanzania wanaomuamini au kumpa nafasi kwa njia moja au nyengine.


Ingekuwa amepuuzwa hata tungejua amesema nini?
 
si k2 cha ajabu kwa ma rais wengi waafrika kuaini wanajimu. hata mkwere ni muumini sana wa hayo mambo ya shiriki. ndo mana alitumiwa ulinzi wa majini na hajaanguka tena. pia jamaa haja kamatwa kwa kutishia demokrasia. ikulu ikasema ana haki ya kutoamaoni yake. shida tu hapo ikulu.
Tokeni leo.
 
Camera zimmulike atakapokua anaenda kupiga kura.

Isije akawa bado anaamini uchaguzi umeairishwa.

Itakua aliomba kwa mungu wake mgombea uraisi afe ili azidi kupata wateja na apate coverage kwenye vyombo vya habari,,lakini Mungu wa Kweli akaingilia kati.
 


Hivi si kuna mgombea urais anayeitwa Mziray? Labda alichanganya.
 
Leo mnajim ameadhirika kwani uchaguzi ni mbele kwa mbele; anawalia hela hao wajinga wakwere wanaomuamini na majini yake!!
 
Jamni huyo ni mchumia tumbo tu! Na mkwere alijua kumtumia vyema sana kuwatishia CCM wenzie kwamba atakaye mpinga atakufa na wote wakatitia kama viwavi! Ni wa kupuuza tu wala hana lolote!
 
Bwana wa majeshi ameshinda vita. Utabiri wa Sheikh Yahaya ni kuwa uchaguzi utaahirishwa na baadae Kikwete atashinda. Kwa kuwa haikutokea maana yake kila alichotabiri kimeenda tofauti hivyo Kikwete ameshindwa uchaguzi...... simple mathematics.... logic .....
Kwa heri baba Kikwete nenda Goba kapumzike kwa Amani ila uache kumwamini huyo Sheikh Yahaya
 
si k2 cha ajabu kwa ma rais wengi waafrika kuaini wanajimu. hata mkwere ni muumini sana wa hayo mambo ya shiriki. ndo mana alitumiwa ulinzi wa majini na hajaanguka tena. pia jamaa haja kamatwa kwa kutishia demokrasia. ikulu ikasema ana haki ya kutoamaoni yake. shida tu hapo ikulu.
Tokeni leo.
Walitaka kuanza kutuletea mambo yale ya pweza paul, ila tunamshukuru Mungu ameshamwondoa huyu mdudu waliyekuwa wanamtumia.
 
Kweli,inawezekana ndumba zake zilimwonyesha jina la mziray,yeye akajua ni yule mgombea.alishindwa kutafsiri,kumbe mziray kocha!!!
 
Huyu ni tapeli tu. Hatuwezi kumjumuisha tapeli katika level kubwa kama hii. Maruhani yake apeleke huko huko kwenye familia yake. Hapa anatafuta tu namna ya kufanywa moja ya mafundi wa mgombea atakayeshinda. Ni mabo ya kiswahili swahili. Taifa letu kwa kuwa limianzishwa katika misingi ya imani za huyu jamaa sasa tunavuna tulichopanda. Mambo ya kifimbo n.k. Ushenzi tu. Chagueni watu wenye imani za sayansi na siyo umafyoso
 
Back
Top Bottom