Wito wa dua na maombi maalum ya kitaifa kwa rais”

mkuchun

Member
Apr 21, 2013
9
45

Wito wangu kwa waTanzania, tuzidishe maombi kwa Raisi wetu. Lakini maombi ya namna gani? Sio maombi yoyote tu? Maombi mahsusi juu ya mtakatifu sana ni kama yale aliyoomba Mfalme Suleiman, Mungu AMPE HEKIMA! Hekima ya kuona kwamba KATIBA MPYA ndiyo dawa na matatizo hayo yanayolikumba taifa. Hekima ya maono na mafunuo juu KATIBA MPYA(siyo ya toleo la Chenge,.,aaah lile la Warioba).,..Hekima ya kuwaongoza watu! Watu waongozwe kwa taratibu na sharia na KATIBA.


Tunahitaji KATIBA MPYA ITAKAYO WAWEKA WATU WOTE CHINI YA SHERIA. Tunahitaji utwala bora na uongozi unaofwata sharia na sio uongozi wa mtakatifu mmoja unotolewa kwa sauti za hisia za uchungu wa mali ya umma, au ukali au vitisho au hasira . Katiba itakayo wahesabu binadamu wote sawa. Katiba isiyobagua watu! Katiba inayomtia hatiani mhujumu uchumi hata kama ni matakatifu sana(ALIYESTAAFU) au awe kondoo wa kafara kama alivyosema Prof. Tibaijuka na wengineo.


Katika siku hizi chache kumekuwa na mvumo wa washangiliaji wengi. Wengine hata wamefanya maandamano ya pongezi kwa mtakatifu sana. Na wengine wamediriki kusema eti matakatifu aongezewe muda wa kutawala mpaka miaka 20. Kama alivyosema mtu mmoja mahali flani, SIDHANI KAMA NI MUDA MWAFAKA KUMSHANGILIA MTAKATIFU SANA KWA AJILI YA KUKAMATWA KWA HARBINDER SINGH SETH NA JAMES RUGEMALILA!!!! Badala ya kushangilia, tunapaswa kujiuliza ni kwa nini wamekamatwa wafanya biashara waliochotewa mabilioni ya Tegeta Escrow lakini wameachwa mawaziri na maafisa wa serikali walioruhusu uchotwaji wa fedha hizo, au wote waliopata mgawo wa fedha hizo.


Tunatakiwa kuhoji ni kwanini mtandao wote wa mafisadi waliogawana hizo pesa usiunganishwe hapo? KWA NINI KWA NINI SIMBA TRUST hasemwi? Kwanza wamezipeleka wapi? Mafano 1.6 bn kwa Prof. Tibaijuka…zimeshaisha? Au walizitumia kwa kumpigia kampeni mtakatifu sana. Watu hawa wote wakamatwe na hela zirudishwe kwanza.

Tunapaswa pia kuhoji ni kwa nini anaelekea kukwepa watu baadhi lakini wengine anawakaba koo? ?? (“Double standard” inaonekana kuwa tabia yake: kumbuka la vyeti vya Bashite, Kikula na Paramagamba,…. Issue ya Lugumi…, n.k). Viashiria hivi vinamfanya mtu mwenye mawazo mapana kuwa na shaka juu Ya DHAMIRA yake halisi. Ndo maana ninahimiza maombi kwa mtakatifu sana.

Mchana mwema!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom