Nyami2010
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 227
- 50
Wasalaam wanaJF
WITO: 2015 tunahitaji kuwa na akina Mhe. Mnyika 15, akina Mhe. Janauary 15, akina Mhe Tundu Lissu 20 ili Tanzania yetu ifikapo 2025 tuwe na uchumi angalau kama ule wa Botswana! Tanzania tuna kila kitu, jamani!
Tutafikaje hapo: Vijana na wasomi, chonde chonde kila mmoja kwa nafasi na wakati wake tuanze harakati na mipango ya kujitokeza kwa wingi ifikapo 2015 ili Taifa hili tusiendelee kuwaachia watu wasio na huruma. Ndugu zangu, siasa ni kila kitu hapa kwetu Tanzania. Uchumi ni siasa, Michezo ni siasa, Afya ni siasa, Kilimo ni siasa, n.k, n.k.
Tunahitaji kuwa na MODEL au njia inayoweza kutuunganisha vijana na wasomi wote nchini na walioko nje ya nchi ili 2015 tuikomboe Tanzania!
Tukiendelea kusema siasa ni mchezo mchafu na haifai, tutaendelea kuwa na watu wabovu wanaofanya maamuzi, wanasinzia bungeni, hawajali na mwisho wa siku maamuzi yao ndiyo mustakabari wa Taifa!
Tujitokeze wote bila kujali tunapitia chama gani, muhimu ni vijana na wasomi tujipange kulikomboa taifa kupitia ballot box 2015!
Ninawasilisha na mbarikiwe sana!