Wito tugomee kupanda ndege za emirates na qatar airways

WITO TUGOMEE KUPANDA NDEGE ZA EMIRATES NA QATAR AIRWAYS
QATAR NA UAE KULIPA GHARAMA ZOTE ZA MAUAJI YANAYOFANYWA NA CRUSADERS WA MAREKANI , UINGEREZA NA UFARANZA.
KISA WANAMCHUKIA GHADDAFI KWASABABU ALIKUA AKIWAMBIA UKWELI KWAMBA WAO NI PUPPETS WA WESTERN POWER.
Taarifa za uhakikaa ni kwamba serikali za kifalme za UAE na QATAR ambazo zenyewe sio za kidemokrasia ndizo zitabeba gharama zote za vita dhidi ya serikali halali ya Libya.Pia nchi hizo ndio pekee katika Arab league ,Jumuia ya Madikteta ya waarabu(ambayo Gadhafi alijitoa kuachana na unafiki wao lakini wakamlamba miguu kwani ingepoteza sifa ya kuwepo kwake)ambazo zimepeleka ndege za kivita kwa ajili ya kushiriki mauaji dhidi ya waislamu wenzao wa Libya.
Tangu mauaji hayo yaanze mamia ya watu ,wakiwemo wanawake na watoto wameuliwa.Idadi inayopita ya raia waliokufa kabla ya mashambulizi ya Crusaders hayajaanza.Sababu zilizotolewa na QATAR na UAE ati ni kuzuia mauaji yanayofanywa na majeshi ya serikali ya Libya.lakini cha kujiuliza Serikali ya Libya kweli inapambana na waandamanaji raia? Au inapambana na uasi uliobuniwa na Sarcorzy rais wa Ufaranza??
Jee waasi wa Bhengazi ni haki kupambana kwa niaba ya miji mengine ya Libya? Waasi hao pia wana bendera yao tofauti na bendera ya serikali ya Libya? Bendera wanayotumia wao ni kifalme aliyepinduliwa na jeshi la Libya wakiongozwa na Gadhafi …kwa hiyo QATAR NA UAE wanaona haya kwao ni sawa?
Mfalme huyu Idrissa aliyepinduliwa aliruhusu nchi yake iwe kibaraka wa Magharibi..wakati wa vita vya SUEZ Ufaransa na Uingereza waliruhusiwa kutumia base zao zilizokuwepo Libya kuipiga EYGPT….haya ndiyo yaliyosababisha wanajeshi wa Libya kumuondowa Kibaraka Mfalme pamoja na Bendera yake…..leo hawa waasi bila ya aibu wanabeba bendera ya puppet huyu na inajulikana kwamba Mfalme Idris alitoka Bhenghazi sasa kuna wachache waliokua wakifaidi kwa sababu waliokua wakifaidi kama zilivo falme za QATAR NA UAE ni familia zao na watoto wao kama hujawa AL MAKHTOUM AU BIN HAMAD AU NAHAYAN BASI HUWEZI KUPATA UWAZIRI , UBALOZI AU HATA MKUU WA TRAFIC.
Leo QATAR NA UAE wapo mbele kuwatetea wasi hawa wana peleka ndege zinaua raia wa Libya, nchi hizi zina kibri cha mali…na leo waasi wa Bhengazi wanawakamata na kuwaua raia WEUSI wa Libya….kwani hapo zamani mfalme wao aliwabagua na kuwatenga .Libya ni nchi yenye raia weusi karibu 45% .
Lakini serikali ya Libya imejitahid kuwaweka raia wote kuwa ni sawa.
Kuna kila dalili ndugu zetu weusi watabagulia na serikali inayotakiwa na QATAR NA UAE…
Hakuna nchi itayokaa kimya kuona waasi wanateka kambi za jeshi wanasaidiwa na maadui na MACRUSADERS basi ikakaa kimya …..ina wajibu wa kulinda usalama wa mipaka ya nchi na raia wake….kama inavofanya serikali ya Libya…
Kabla ya waasi hawajateka kambi za jeshi Ghaddafi hakutumia ndege kuwapiga wandamanaji..alitumia mabomu yamachozi kama police wa London walivofanya juzi….lakini walipo chukua silaha tena nzito kuharibu miji na mali za serikali Nayo serikali ilibidi itumie silaha kuweka hali ya usalama, QATAR NA UAE nao wangefanya kama alivofanya Ghaddafi…
Kwa vile wanatumiwa dhidi ya waislam wenzao na kwa vile Libya ilikua ni afrika zaidi kuliko Uarabu…..Waafrika na Watanzania tuoneshe kuchukizwa kwa nchi hizi mbili kutumiwa dhidi ya walibya kwa maslahi ya nchi za Magharibi….
Kwa kuanzia tusipande ndege zao na tujizuie kwenda UAE kwa ajili ya biashara…kma ni bishara nendeni China..
TUSUSIE KUPANDA NDEGE ZA UAE NA QATAR KUANZIA SASA HII ..KILA MTU AMWAMBIE MWENZAKE ..MISIKITINI…KOTE ..KWENYE FACEBOOK…..HAWA JAMAA HAWATUSAIDII CHOCHOTE …AFADHALI GHADDAFI……TUONESHE KWAMBA WANACHOFANYA SIO SAHIHI WANATIA AIBU UTU WAO…
TUSUSIE
mbona hujasema tususie misikiti,fwedha ,tende,mazulia yatokayo huko yakhe
 
mama yangu zile totozi taaamu niache kisa??? hujasafiri nini mkuu maana ungesema tuacge kukwea yale mapipa maana zile totozi ni nouma
 
haki ya nani, dini hii ya mwamedi inaharibu sana watu, inawaumiza moyo bureee, inawabadilisha hadi akili wanakuwa kama mandondocha? sasa hii issue ya libya wameshatangaza kuwa wale wanaopigana na gadafi ni ma crusaders kwasababu tu gadafi alishawahi kuwajengea msikiti hapa dodoma? wamareani wangekuwa wamewajengea huo msikiti, wangesema gadafi ndo crusader...hahaha. akili zingine kama matope haki ya nani!
 
Na wala hajasema yeye binafsi anapanda/anasafiri na hizi ndege mara ngapi kwa mwaka.


Unaweza kuta mtoa mada hata usafiri wenyewe haujui... sasa nimeamua rasmi lazima nipande hizo ndege!!!:A S-key:
 
hao uea na qatar maendeleo yao yapo juu ie aljazira, dubai ndo mji wa kibiashara,, ndo mana hawaungi mkono mambo ya kipumbavu ya akina gadafi,,utaendelea kufa na kijiba cha roho ndege zao 2tapanda
 
Mie napanda Lufthansa na KLM tu, sipandi hizo Qatar ndege za bei rahisi...

natania bwana, tusipopanda Emirates na qatar patakalika??

tutabanana hapo hapo kajambanani ndani ya emirates.
 
Gadaff kasaidia kipi Africa mpaka nimuunge mkono?
jitu limeua raia wake halifai kabisa

viva france, thanks GOD for making sarkozy presidaa as he kicked da ball at right time on right direction.
 
Hebu pendekeza basi mashirika mbadala ya ndege yasiyo na chembechembe za macrusader ili tusafirie na dhamira safi.

mashirika yapo ila nauli yao unakuta ni mara tatu ya emirates na qatar, si bora uje nazo bongo hizo dola za kupandia KLM, lufthansa etc. ugawie maskini?
 
Huyu Macos sijui wa wapi huyu, tunashindwa kususia vodacom ya mafisadi tunakwenda kususia mashirika ya kigeni yanayofanya safari za kigeni??

kweli watu wengine priorities zero!!

Ntapanda na ntaenda nazo kama nauli ni cheap
 
Gadaff kasaidia kipi Africa mpaka nimuunge mkono?
jitu limeua raia wake halifai kabisa

viva france, thanks GOD for making sarkozy presidaa as he kicked da ball at right time on right direction.
dah... powder balaa aisee
 
.HAWA JAMAA HAWATUSAIDII CHOCHOTE …AFADHALI GHADDAFI……TUONESHE KWAMBA WANACHOFANYA SIO SAHIHI WANATIA AIBU UTU WAO…[/B]
TUSUSIE

Watu wengine bana, yaani akili zenu zinawaza misaada tu hata kama anaewapa misaada anafanya vitu kinyume na haki za binaadamu

Huu ndio unafiki mwalimu alikuwa hautaki wa kuinama kufumbia macho ukanywagaji wa haki za binadamu kwa mgongo wa misaada

Kwa hiyo hayo mamisikiti aliyojenga kama wa hapa Dodoma kwa kuwa ni mikubwa na mandhari ya kupendeza ndo mnaona bora akandamize watu wake lakini aendelee kuwepo maadam tu mtapata misikiti yenye mabango ya ufadhili wa "Ghadaffi Foundation"

Ikitokea nafasi ya kupanda ndege nitakata za UAE na Qatar kwa kuwa hakuna unafiki, hata kama mtu anatoa misaada, mbele ya haki za watu NO
 
Maneno yako yana ukweli. Hata hivyo binafsi bado sijawasahau WALIBYA jinsi walivyo kuwa dhidi yetu wakati wa vita vya Kagera wakitupiga kwa kushirikiana na Idd Amini Dada. Iweje leo nigome kupanda madege ya Emirates kisa kuwa unga mkono maadui zetu? Itakuwa ngumu bro.
 
mbona hujasema tususie misikiti,fwedha ,tende,mazulia yatokayo huko yakhe


Mfia nchi hapa nakugongea thanks maana misaada yake naona mamisikiti tu

Dom hapa kashusha bonge la sikiti la kufufuka mtu............

wanawasiwasi wa kukosa tende, halua na mazulia ya misikitini na misikiti yenyewe kutoka Libya
 
Nafikiri mtoa mada hafahamu analoongea amekurupuka. The future sasa hivi ni Emirates, hakuna shirika lolote la ndege hivi sasa ulimwenguni ambalo ni kubwa haliweweseki kutokana na mbinu za Emirates. Kwa taarifa yako shirika hili limeingiza ndege mpya mwaka huu 30+ ku-add up fleet yao ambayo tayari ina ndege 80 + siongelei ndege ambazo Watanzania wengi wanazifahamu naongelea new planes za uhakika sio mitumba ya ndege.

Emirates wataendelea kutoa huduma za nauli rahisi kuliko shirika lolote hata kama Watanzania wote wanaosafiri watasusia ndege zao, vile vile lazima ujue jamaa wamejiandaa hivi sasa wanakwenda kila kona ya ulimwengu via Dubai.

Cha kusikitisha sisi Tanzania tumewapa more rights kuja kutua kwetu wakati hatuna ndege za kwenda kutua kwao, tumewakumbatia mafisadi wetu hapa nyumbani ambao wanajitajirisha wao na makuwadi wao wa nje. Wanaua kila kitu ambacho taifa hili lingetegemea katika kuona maisha ya wananchi wake yanakuwa bora.
 
Nasikia pia kuna baadhi ya waislam wamesusia kunywa Coca Cola na maji ya Kilimanjaro sababu zinazalishwa na kafri, wanakunywa Pepsi na maji ya Azam!
 
Ndege hazina makosa bana labda useme kiusalama maana hivi sasa zitakuwa target
 
Juzi nilikua nasafiri sikupanda hizo ndege, nimewachukia sana hawa vilaza..mwisho wa siku Afrika itabaki imara...NAMUOMBEA NJAA OBAMA HAPATI TENA URAIS...jALUO HOVYO KABISA YULE TENA AKIJA MITAA YANGU TARIME LAZIMA NIMTOE MKUKU
wewe unafikiri republican wangekuwa madarakani huyo mjomba gaddafi angekuwepo pale sa ivi? wangekuwa washamnyoa kitambooooooooo
 
Back
Top Bottom