Wito tugomee kupanda ndege za emirates na qatar airways | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito tugomee kupanda ndege za emirates na qatar airways

Discussion in 'International Forum' started by Macos, Mar 31, 2011.

 1. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  WITO TUGOMEE KUPANDA NDEGE ZA EMIRATES NA QATAR AIRWAYS
  QATAR NA UAE KULIPA GHARAMA ZOTE ZA MAUAJI YANAYOFANYWA NA CRUSADERS WA MAREKANI , UINGEREZA NA UFARANZA.
  KISA WANAMCHUKIA GHADDAFI KWASABABU ALIKUA AKIWAMBIA UKWELI KWAMBA WAO NI PUPPETS WA WESTERN POWER.
  Taarifa za uhakikaa ni kwamba serikali za kifalme za UAE na QATAR ambazo zenyewe sio za kidemokrasia ndizo zitabeba gharama zote za vita dhidi ya serikali halali ya Libya.Pia nchi hizo ndio pekee katika Arab league ,Jumuia ya Madikteta ya waarabu(ambayo Gadhafi alijitoa kuachana na unafiki wao lakini wakamlamba miguu kwani ingepoteza sifa ya kuwepo kwake)ambazo zimepeleka ndege za kivita kwa ajili ya kushiriki mauaji dhidi ya waislamu wenzao wa Libya.
  Tangu mauaji hayo yaanze mamia ya watu ,wakiwemo wanawake na watoto wameuliwa.Idadi inayopita ya raia waliokufa kabla ya mashambulizi ya Crusaders hayajaanza.Sababu zilizotolewa na QATAR na UAE ati ni kuzuia mauaji yanayofanywa na majeshi ya serikali ya Libya.lakini cha kujiuliza Serikali ya Libya kweli inapambana na waandamanaji raia? Au inapambana na uasi uliobuniwa na Sarcorzy rais wa Ufaranza??
  Jee waasi wa Bhengazi ni haki kupambana kwa niaba ya miji mengine ya Libya? Waasi hao pia wana bendera yao tofauti na bendera ya serikali ya Libya? Bendera wanayotumia wao ni kifalme aliyepinduliwa na jeshi la Libya wakiongozwa na Gadhafi …kwa hiyo QATAR NA UAE wanaona haya kwao ni sawa?
  Mfalme huyu Idrissa aliyepinduliwa aliruhusu nchi yake iwe kibaraka wa Magharibi..wakati wa vita vya SUEZ Ufaransa na Uingereza waliruhusiwa kutumia base zao zilizokuwepo Libya kuipiga EYGPT….haya ndiyo yaliyosababisha wanajeshi wa Libya kumuondowa Kibaraka Mfalme pamoja na Bendera yake…..leo hawa waasi bila ya aibu wanabeba bendera ya puppet huyu na inajulikana kwamba Mfalme Idris alitoka Bhenghazi sasa kuna wachache waliokua wakifaidi kwa sababu waliokua wakifaidi kama zilivo falme za QATAR NA UAE ni familia zao na watoto wao kama hujawa AL MAKHTOUM AU BIN HAMAD AU NAHAYAN BASI HUWEZI KUPATA UWAZIRI , UBALOZI AU HATA MKUU WA TRAFIC.
  Leo QATAR NA UAE wapo mbele kuwatetea wasi hawa wana peleka ndege zinaua raia wa Libya, nchi hizi zina kibri cha mali…na leo waasi wa Bhengazi wanawakamata na kuwaua raia WEUSI wa Libya….kwani hapo zamani mfalme wao aliwabagua na kuwatenga .Libya ni nchi yenye raia weusi karibu 45% .
  Lakini serikali ya Libya imejitahid kuwaweka raia wote kuwa ni sawa.
  Kuna kila dalili ndugu zetu weusi watabagulia na serikali inayotakiwa na QATAR NA UAE…
  Hakuna nchi itayokaa kimya kuona waasi wanateka kambi za jeshi wanasaidiwa na maadui na MACRUSADERS basi ikakaa kimya …..ina wajibu wa kulinda usalama wa mipaka ya nchi na raia wake….kama inavofanya serikali ya Libya…
  Kabla ya waasi hawajateka kambi za jeshi Ghaddafi hakutumia ndege kuwapiga wandamanaji..alitumia mabomu yamachozi kama police wa London walivofanya juzi….lakini walipo chukua silaha tena nzito kuharibu miji na mali za serikali Nayo serikali ilibidi itumie silaha kuweka hali ya usalama, QATAR NA UAE nao wangefanya kama alivofanya Ghaddafi…
  Kwa vile wanatumiwa dhidi ya waislam wenzao na kwa vile Libya ilikua ni afrika zaidi kuliko Uarabu…..Waafrika na Watanzania tuoneshe kuchukizwa kwa nchi hizi mbili kutumiwa dhidi ya walibya kwa maslahi ya nchi za Magharibi….
  Kwa kuanzia tusipande ndege zao na tujizuie kwenda UAE kwa ajili ya biashara…kma ni bishara nendeni China..
  TUSUSIE KUPANDA NDEGE ZA UAE NA QATAR KUANZIA SASA HII ..KILA MTU AMWAMBIE MWENZAKE ..MISIKITINI…KOTE ..KWENYE FACEBOOK…..HAWA JAMAA HAWATUSAIDII CHOCHOTE …AFADHALI GHADDAFI……TUONESHE KWAMBA WANACHOFANYA SIO SAHIHI WANATIA AIBU UTU WAO…
  TUSUSIE
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Poleni sana waislam wa Tanzania maana inaonyesha muna uchungu kuliko hata walibya wenyewe..
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Sijawahi safiri na hizi ndege ila naanza rasmi sasa :love::love::love:
   
 4. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  susia kimpango wako mazee,wacha siye wengine tuendelee kufaidika na hizo huduma
   
 5. m

  matambo JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  bahati mbaya mimi sipandi ndege
  ningewagomea kabisa
   
 6. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Nina ticket ya kusafiri July na Emirates, ngoja niangalie utaratibu kama huwa wanarudisha chenji nile kona shirika lingine :rip:
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  susia mwenyewe bana.....ukisusa wenzio twala......pesa ya kupanda BA na KLM sina
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Badala ya kususia simuende mkamsaidie...kawajengea misikiti leo anapigwa mnasusia kupanda ndege tu...
   
 9. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Juzi nilikua nasafiri sikupanda hizo ndege, nimewachukia sana hawa vilaza..mwisho wa siku Afrika itabaki imara...NAMUOMBEA NJAA OBAMA HAPATI TENA URAIS...jALUO HOVYO KABISA YULE TENA AKIJA MITAA YANGU TARIME LAZIMA NIMTOE MKUKU
   
 10. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sasa unashauri watu wapande ndege za shirika gani? Gulf Air (dala dala la uarabuni), Egypt Air au Yemenia?

  By the way una valid point lakini umeharibu kila kitu ulipoingiza mambo ya sijui crusaders and whatnot, mwisho wa siku asilimia kubwa ya vitu unatakavyotumia be it ndege, computer, simu etc ni kutoka kwa hao hao crusaders.
   
 11. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kwamba mimi nitazipanda sana tena nimegundua ni bei rahisi kuliko nilozizoea KLM... mleta sredi susia mwenyewe!!!!:love::love: Emirates!!
   
 12. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ...nimekuelewa nitapanda Air France, BA na BA!!
   
 13. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tatizo kubwa sasa ni juu ya hali ya usalama wa ndege hizo.

  Kumbuka Col. Qadaffi alivyoisambaratisha Lockorbie...
   
 14. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi naunga mkono kuanzia leo sipandi ndege, nadunda na mguu nikichoka ngamia tu!!! :A S-coffee:
   
 15. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Hebu pendekeza basi mashirika mbadala ya ndege yasiyo na chembechembe za macrusader ili tusafirie na dhamira safi.
   
 16. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapo sasa!
   
 17. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  ..MR..Utakuwa hujakosea, kama Qatar Airways wanakwambia ni 5 star airline naomba uamini. KLM na BA hawafikii kabisa hata chembe kwa huduma za QR. Usimuige mtoa mada

  ..Haswaa!
  Kwi kwi kwi! Sure. QR huwa wananilaza kwenye hoteli kali sana, siwezi kuwamwaga.

  Yes! Naona unakwepa trip ya Dar-London-Dubai, umeamua kuchukua mkata wa Dar-Dubai directly. Hongera sana.
   
 18. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  air tanzania!
   
 19. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  kama ndio hivyo bac inauma sana
   
 20. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Ah wapi hiyo haiwezekani tutazidi kupanda tu hizo ndege za UAE na QATAR tena kwa raha zetu,toka lini Libya wamewahi kutuunga mkono kwa ajili ya matatizo yetu ?
   
Loading...