Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,442
- 113,452
Wanabodi,
Japo JF ni an open public forum kwa wote, mtu ukiwa na ujumbe wako fulani ambao ni muhimu, unataka kumfikishia mlengwa au walengwa fulani, ukiutuma ujumbe huo kupitia jf, unamfikia mlengwa kwa haraka zaidi na kwa urahisi zaidi, hivyo hili ni bandiko, kwa ajili ya kufikisha ujumbe fulani kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Waziri wa Kilimo, na Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuhusu umuhimu wa Chakula kwa binadamu, hivyo siku ya Chakula Dunani, ipewe umuhimu unaostahili.
Kwavile wote tunaamini Mungu, tunaamini tumeumbwa na Mungu, na kupatiwa zawadi ya uhai kwa kupuliziwa pumzi ya uzima,
Kutokana na umuhimu wa siku hii, serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro, ikaamua kulichagua eneo la Pasua, kuwa ndilo eneo stahiki la kufanyia maandhimisho hayo, na maonyesho hayo, hivyo mimi nami, kama Mtanzania mwingine yoyote, niko Mkoani Kilimanjaro, kuwaletea, kila kinachoendelea kwenye viwanja hivi vya Pasua.
Hapo katika viwanja vya Pasua, pamoja na mambo mengine yote, pia Chanjo ya Corona inatolewa bure.
Sasa imetokea tuu kama zali, maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani mkoani Kilimanjaro, yamepata bahati ya mtende, ku concide ya ziara ya mtu mmoja muhimu, kufanya ziara ya kiserikali mkoani Kilimanjaro. Kwa vile ziara zote za kiserikali ni ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndio huratibu kwa kushirikiana na wizara husika, mgeni atembelee wapi na wapi, na kumpangia siku ya kuzungumza na wananchi. Sasa kwa vile ugeni huu ume coincide na Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, sasa kufuatia umuhimu wa Chakula kwa binadamu na kwa nchi yetu, hili ni ombi langu kwa serikali ya Mkoa, kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, na Wizara ya Mifugo, mleteni mgeni huyu viwanja vya Pasua. Tena ningekuwa mimi ndio RC wa Kilimanjaro, ile siku ya mgeni wetu kuzungumza na wana Moshi, ningempangia azungumzie viwanja vya Pasua, ili pia wana Moshi na wana Kilimanjaro, wajitokeze kwa wingi, sio tuu kumsikiliza mgeni wetu akizungumza na wana Moshi na wana Kilimanjaro, bali pia atahamasisha, wana Moshi na Wana Kilimanjaro, kujitokeza kwa wingi, kuchanja.
Hivyo huu ni wito wangu kwa RC wa Kilimanjaro, Waziri wa Kilimo na Waziri wa Mifugo, kufuatia umuhimu wa chakula kwa uhai wa binaadamu na viumbe wote, ambapo baada ya umuhimu wa Mungu aliyetuumba, na pumzi ya uhai tunayoivuta, chakula ndicho kitu muhimu kuliko vitu vingine vyote, hivyo kwa niaba ya wana Pasua, tunawaomba, P'se mpitisheni mgeni wetu na kwenye viwanja vya Pasua, hata asipozungumza chochote, angalau atupungie tuu mkono, na sisi tumpungie kumjulisha tuko pamoja nae.
Ni Hayo Tuu.
Paskali, Pasua, Moshi, Kilimanjaro.

- Hivyo kitu muhimu nambari moja kwa binaadamu ni Mungu, The Almighty God, The Father, The Creator, who created us, and everything.
- Kitu muhimu nambari mbili ni hewa, pumzi, uhai, the air that we breathe
- Na kitu muhimu nambari tatu ni chakula, the food that we eat, to live, to survive.