Wito: Posho za nyumba, umeme, maji na simu kwa mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa zifutwe

Ndiyo maana wana viburi vya kila siku kutuimbia wimbo kuwa tujiajiri, wakati wenyewe wenye uwezo wa kupata hata mtaji wa m50 hawasubutu kujiajiri!
Usiahau kumtaja mwenye hati miliki ya hilo ulosema maana ni nukuu.
 
Mawazo ya kimasikini yanazidi kushamiri awamu hii, nadhani ni kwa vile rais anaupenda umasikini na kuupigia debe na kudai yeye ni rais wa masikini na anawapenda masikini basi kila mtu anadhani umasikini ni sifa na anataka awe masikini.

Watu masikini wana wivu sana hawataki kuona mtu anafaidi,wao wanataka kila mtu awe kama wao,wakisikia flani anafaidi hivi roho inawauma sana.

Haya ya kutaka sijui nini kuondolewe,itafika hatua mtataka hata rais asiishi ikulu na aaipewe ulinzi maana ni gharama.

Heri uwe masikini lakini uwe na mawazo ya kitajiri kama mimi kuliko kua masikini na mawazo ya kimasikini kama mtoa mada, mawazo ya kimasikini ni mabaya sana.

Hii inatokana na rais kupandikiza mawazo ya kimasikini kwa watu na kuona kila aliefanikiwa ni fisadi au kila anaeishi vizuri ni mwizi. Hii nchi bwana.
Nimegundua wewe unafurahia wazo la waziri mkuu kwa wengine ila wewe lisikuguse au sivyo.
 
Kuetekeleza Agizo la Mh Waziri Mkuu kwa vitendo kama mwananchi wa kawaida namuomba Waziri na Katibu Mkuu mwenye mamlaka azifutilie mbali posho za Nyumba, Umeme, Simu na Maji kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Idara katika Wizara, Mikoa na Halmashauri.

Kwa ufupi Posho hizi zilizobatizwa jina la Utility zinaweka tabaka baina ya watumishi wa Umma, inasikitisha na Kushangaza Wakuu wa Idara na Viongozi mbalimbali wa Kisiasa ambao wengi wao mishahara yao inaanzia 3,700,000/= hadi 5,500,000/= kulipwa tena posho za nyumba, umeme, maji na simu ilihali mishahara yao ni mikubwa na inajitosheleza.

Posho ambazo viongozi hawa hupata kila mwezi kwa ajili ya nyumba, umeme, maji na simu ni Tsh 975,000/= ambapo posho tu wanayopokea inazidi mshahara wa afisa wa kawaida mwenye degree anayelipwa TSH 710,000/= kwa mwezi hapo hujaweka makato ya kodi, bima ya afya na mifuko ya jamii.

Mh Waziri Mkuu kama tunataka kuleta usawa katika watumishi wa umma anza nahii posho ya 975,000/= ambayo hata Mh Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndugu hapi analamba kila mwezi nje ya mshahara wake.
kwa mfano, mikoa 26,kila mkoa wilaya 4= wakurugenzi 104
wale wa manispaa na majiji =26
Jumla 130
Posho zao 975,000x130 =126,750,000.

Aaaah kumbe bado ni vijisent tu sawa na zile wanazopokea kila siku wale jamaa wa ile kashfa ya umeme
Acha wapewe tu,lakini huku chini waongeze japo hiyo mishahara.
 
Watu hao hawalipwi hayo kwa hisani, wanalipwa hayo kutokana na kazi na hatari zinazoambatana na hiyo kazi.

Nasema ni mawazo ya kimasikini maana masikini ndio anaona mwenzake anafaidi basi wafanane,huyu alietoa mada anaona hao wakurugenzi na madc sijui nani wanafaidi sana waondolewe hizo huduma wawe sawa na yeye.

Mtu ni katibu mkuu,yeye ndie mtendaji na msimamizi mkuu wa mambo ya wizara kuanzia watumishi,fedha nk,unataka alipwe laki saba bila marupurupu afanane na wewe unaefunsisha huko nyampulukano sec school,haiwezekani.

Lazima muelewe, watu hawalipwi mishahara wao na hawapewi hizo huduma wao, inalipwa huduma wanayoitoa,inalipwa kazi wanayoifanya,usione mbona Mkuu wa wilaya Flani bwana flani analipwa hiki na hiki, hapana, halipwi bwana flani, inalipwa kazi anayoifanya bwana flani.

Haya ni mawazo ya kimasikini. Kama mawazo ya kimasikini hayatatutoka tuna safari ndefu ya maendeleo. Kwa nini usifight kua kama yeye ulipwe hizo badala yake unataka yeye awe kama wewe?
Sijawahi ona mawazo pumbavu kama haya tangu niingie jamii forum.
 
Hii kitu nimewahi kuhoji mara kibao, iweje mtu unalipwa mshahara mkubwa ila wanapata huduma nyingine bure? Halafu unakuta anayelipwa kidogo ndio anajigharamia vitu vyote
Watumishi wa uma wanatakiwa kuwa na bunge lao,sio hilo la kulala na la gizani.
 
Mawazo ya kimasikini yanazidi kushamiri awamu hii, nadhani ni kwa vile rais anaupenda umasikini na kuupigia debe na kudai yeye ni rais wa masikini na anawapenda masikini basi kila mtu anadhani umasikini ni sifa na anataka awe masikini.

Watu masikini wana wivu sana hawataki kuona mtu anafaidi,wao wanataka kila mtu awe kama wao,wakisikia flani anafaidi hivi roho inawauma sana.

Haya ya kutaka sijui nini kuondolewe,itafika hatua mtataka hata rais asiishi ikulu na aaipewe ulinzi maana ni gharama.

Heri uwe masikini lakini uwe na mawazo ya kitajiri kama mimi kuliko kua masikini na mawazo ya kimasikini kama mtoa mada, mawazo ya kimasikini ni mabaya sana.

Hii inatokana na rais kupandikiza mawazo ya kimasikini kwa watu na kuona kila aliefanikiwa ni fisadi au kila anaeishi vizuri ni mwizi. Hii nchi bwana.
SIJU KAMA AKI YAKO INA AKIL
 
Oneni aibu basi wanajeshi.. Polisi.. Magereza posho wanyimwe ili daily watukabe na kutupiga roba... Naunga mkono hoja Kwa posho ya President..PM..Mawaziri.. Makatibu wakuu... Wabunge na mashirika ya umma...
 
Watu hao hawalipwi hayo kwa hisani, wanalipwa hayo kutokana na kazi na hatari zinazoambatana na hiyo kazi.

Nasema ni mawazo ya kimasikini maana masikini ndio anaona mwenzake anafaidi basi wafanane,huyu alietoa mada anaona hao wakurugenzi na madc sijui nani wanafaidi sana waondolewe hizo huduma wawe sawa na yeye.

Mtu ni katibu mkuu,yeye ndie mtendaji na msimamizi mkuu wa mambo ya wizara kuanzia watumishi,fedha nk,unataka alipwe laki saba bila marupurupu afanane na wewe unaefunsisha huko nyampulukano sec school,haiwezekani.

Lazima muelewe, watu hawalipwi mishahara wao na hawapewi hizo huduma wao, inalipwa huduma wanayoitoa,inalipwa kazi wanayoifanya,usione mbona Mkuu wa wilaya Flani bwana flani analipwa hiki na hiki, hapana, halipwi bwana flani, inalipwa kazi anayoifanya bwana flani.

Haya ni mawazo ya kimasikini. Kama mawazo ya kimasikini hayatatutoka tuna safari ndefu ya maendeleo. Kwa nini usifight kua kama yeye ulipwe hizo badala yake unataka yeye awe kama wewe?
Baba yako yumo kati ya wanaofurahia mateso ya wengine walio wengi,huna haja ya kulaaniwa bali ipo siku kivuri chako kitakukimbia.
 
Jamani siasa tamu kumbe vitu vingi tu wanalipiwa next time nachukua kadi kwenye chama cha hashimu rungwe.
 
Naunga mkono hoja, kusiwe na discrimination, kama kwingine zimefutwa basi kote zifutwe tu maana hamna namna!
Halafu hata ukienda dukan kununua unga, mangi yeye hajui nani anapokea 710,000 au 5,500,000 wote munalipa sawasawa
 
Hawawezi kukubaliano na hilo mkuu, kisu kwenye mfupa nani anataka
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom