Kuetekeleza Agizo la Mh Waziri Mkuu kwa vitendo kama mwananchi wa kawaida namuomba Waziri na Katibu Mkuu mwenye mamlaka azifutilie mbali posho za Nyumba, Umeme, Simu na Maji kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Idara katika Wizara, Mikoa na Halmashauri.
Kwa ufupi Posho hizi zilizobatizwa jina la Utility zinaweka tabaka baina ya watumishi wa Umma, inasikitisha na Kushangaza Wakuu wa Idara na Viongozi mbalimbali wa Kisiasa ambao wengi wao mishahara yao inaanzia 3,700,000/= hadi 5,500,000/= kulipwa tena posho za nyumba, umeme, maji na simu ilihali mishahara yao ni mikubwa na inajitosheleza.
Posho ambazo viongozi hawa hupata kila mwezi kwa ajili ya nyumba, umeme, maji na simu ni Tsh 975,000/= ambapo posho tu wanayopokea inazidi mshahara wa afisa wa kawaida mwenye degree anayelipwa TSH 710,000/= kwa mwezi hapo hujaweka makato ya kodi, bima ya afya na mifuko ya jamii.
Mh Waziri Mkuu kama tunataka kuleta usawa katika watumishi wa umma anza nahii posho ya 975,000/= ambayo hata Mh Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndugu hapi analamba kila mwezi nje ya mshahara wake.