Wito: Mabenki yanayokopesha kuweni macho na hali iliyosababishwa na serikali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito: Mabenki yanayokopesha kuweni macho na hali iliyosababishwa na serikali.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgt software, Jul 28, 2011.

 1. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,727
  Likes Received: 1,635
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa naanza kwa kutoa shukrani ziwaendee mabenki yaliyotayari kuwakopesha wanyonge na kuwalaani wanaowatenga wanyonge kuwa hawana vigezo kuwa na mkopo.
  Serikali ndiyo iliyozalisha ukosefu wa ajira kwa kutoandaa mbinu za kuwakomboa vijana, ikiwa ni kuwapatia elimu ya kutosha pamoja kuandaa mazingira mazuri ya kujitegemea.
  Kwa kupitia Bank vijana wengi walianza kujishughuli hasa kwenye biashara, uunzi, useremala, ushonaji, gereji uchomeleaji, salooni n.k
  Ikiwa umeme ndio chanzo kikuu cha kuendesha shughuli hizi na kwa bahati mbaya sana shughuli hizi hazikwepi umeme, kwa ufupi ajira ndio zimepotea, hivyo mabenk yote yaliyotoa mikopo midogo midogo au mikubwa wajaribu kuwatembelea wateja wao wajionee mateso wanayoyapata wajasirimiamali waachane na kuuza mali za wateja wao kwani wao wameshaanguka kiuchumi.
  Fikilia wewe umepewa mkopo kupitia hati ya nyumba ya kakayako ili kukidhi vigezo, umeanzisha mradi mkubwa wa duka la nguo, umekodi kairakoo maduka ya katikati, umeme ndio huo hakuna kabisa, nani ataenda kwenye giza kununua nguo?
  Tunashukru ndugu zetu wachina kama vile walijua maana wameingiza generator la kudumu kwa miezi miwili ambazo huziuza kuanza laki moja na nusu mpaka laki tatu angalau wanatumulikia kidogo tuuze nguo mbili, angalia gharama za mafuta generator dogo hutumia 15,000/= kwa siku badala ya sh. 1,500.00 kuwasha taa, lile likishawashwa halina kipimo , hivyo halina bajeti yamatumizi.
  Tena nilikuwa nawaomba na hawa TRA wajipe likizo ya miezi mitatu kwani wanakamua ng'ombe ambaye serikali imekula majani yake kwa kushindwa kutatua tatizo sugu.
   
Loading...