sunshine1
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 539
- 290
Nianzie kwa kumshukru Mungu kwa ajili yakumjalia kila mmoja wetu afya njema hadi hivi leo.
Pia nimshukuru Mungu kwa kulilinda taifa letu na kutupa hali ya utulivu bila kujali tunapitia katika changamoto zipi.
Na mwisho niwashukuru wamiliki na waendeshaji wa JF kwakututengenezea namna yakuweza kujadili mambo mbali mbali nakubadilishana mawazo kuhusu mambo mbali mbali yanayotugusa kama individuals na kama taifa.
Sasa nisipoteze muda niende kwenye mada husika ni wito gani hasa na kwanini ni wito.
Wito wangu unahusu vifo vya kila leo vya watanzania wenzetu ndani ya taifa
Ni siku chache tu zilizopita nadhani wengi wetu tutakuwa tumesikia taarifa zakusikitisha za kifo cha mtanzania mwenzetu somebody Kamukara (RIP) aliyeuawa na majambazi wakihitaji kumpora fedha. Sina taarifa sana kama walifanikiwa kumpora fedha au lah na wala kwangu fedha siyo mada hasa. Mada yangu ni je vifo hivi haviwezi kuzuilika? Wapo watakaojiuliza why naandika baada ya kifo hiki? Niweke wazi mapema kuwa sikuwahi kumfahamu huyo bwana ila kifo chake kimenikumbusha matukio mengi na vifo vingi vinavyofanana na hiki vilivyokwisha kutokea huko nyuma na ikanipelekea kujiuliza hivi tutaendelea kusema RIP mpaka lini? Je vifo hivi haviwezi kuzuilika? Jibu la wazi nikuwa inawezekana tukiweka nia katika kufanya hivyo. Kutokana na tarifa zisizo rasmi ni kuwa Kamukara aliuawa baada yakuwa amechukua fedha bank ili aende kununua vigae vya nyumba yake Nabaki Africa. Ni wazi kuwa kuna uwezekano wapo waliofahamu plan zake vizuri na wakahamua kumfuatilia au kutoa taarifa kwa waliomfuatilia nakupelekea kifo chake. Sasa point yangu inakuja je hakukuwa na uwezekano wakutumia bank transfer kulipia hivyo vigae ili kupunguza tension zakubeba furushi la fedha mkononi? Na kama uwezekano huo haukuwepo then tunajifunza nini kutokana na kifo hiki na vingine vingi kama hiki? Ni wazi kuwa sasa tunahitaji kuimarisha mifumo yetu yakibenk nakuifanya ifanye kazi kisasa zaidi ili kuhakikisha usalama kwa wateja wake na pia kudhibiti matumizi ya pesa chafu. Kwa jinsi watanzania wamekuwa active kwenye mitandao na social media mbali mbali kama whatssapp, Instagram, facebook nk ni dalili tosha kuwa matumizi yetu ya internet na upatikanaji wake umekua. Je kwanini tusitumie ukuaji huu kuokoa maisha ya ndugu zetu nakulinda uchumi wa taifa letu? Kwa mfumo wa sasa ni wazi kuwa hakuna udhibiti wowote wa fedha na nivigumu kufahamu ni nani mwenye fedha halali kwa maana kuwa ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mkulima au jambazi. Wote hawa wanauwezo wakufanya manunuzi wakiwa na maburungutu ya fedha bila uwezekano wakuwatofautisha. Je kwa hali hii how can we differentiate dirty money from clean money? Je tunajihakikishia vipi kuwa kila mmoja anatumia fedha alizojipatia kwa halali? Hivyo kwa maswali haya natoa wito kwa waziri wa fedha. Mabenk, wanasheria na wabunge wetu kushirikiana ili kuleta ufumbuzi ni jinsi gani yakujibu maswali haya. Kwa mtazamo wangu ningependa kushauri yafuatayo;
· Ipitishwe sheria itakayotoa maximum amount ya mtu kulipia huduma yoyote kwakutumia cash.
· Bank zote zilazimishwe kuimarisha net banking na iwe salama. Wateja waweze kulipia huduma mbali mbali ndani na nje ya taifa letu online.
· Wafanya biashara mbalimbali na huduma zozote zinazohusisha fedha ziweke utaratibu wamtu kulipa fedha kwenye mashine kwakutumia bank card. Hii iwe compulsory kwa mteja na muuzaji pia kwakuweka kiwango fulani cha fedha. Mfano inapozidi laki tano ni lazima kulipia kwa bank card na siyo cash.
· Bank ziweke transparency yakutosha kuhusu cash flow za wateja wao. Hii inamaana ukiwa nyumbani uweze ku log in nakuangalia transactions zote zilizofanyika.
· Pia kufanyike utaratibu wa security kisheria kwa watoa huduma mbalimbali na wateja wao. Wafanyakazi wa bank wawekewe sheria very strict zakuhakikisha confidentiality za wateja na wale wote watakaoripotiwa kukiuka sheria itumike bila kuchelewa. Security hii pia ilenge kuhakikisha safe transactions kwa mteja na mtoa huduma. Mfano mteja aweze kununua bidhaa kwakusign fomu au mkataba then anaenda kulipia huduma hiyo bank through bank transfer. Naamini tukifanya hivi tutapunguza temptation za wezi na majambazi kufuatilia watu wanaotoka mabenk wakihisi wana fedha au kuvamia baadhi ya maeneo yabiashara wakitaraji kukuta big cash itokanayo na mauzo. Pia tufanye promotion na uhamasishaji kwa kila mwananchi kuwa na bank account hata kama ni mkulima ili transactions zetu ziwe more virtual. Na kuwe na sheria yakuzuia mtu kukutwa na certain amount of cash ambazo hawezi kuzitolea maelezo. Hii pia itasaidia ku control na kufahamu ni nani ana fedha halali na zisizo halali.
Mwisho niwakumbushe mawaziri, wabunge na viongozi mbalimbali wa serikali kuwa mwaka 2016 uwe ni mwaka wakuwa tayari kufanya kazi na wananchi kwa ukaribu, kupokea ushauri nakushirikiana na wanachi katika kuboresha huduma zetu. Ni wazi kuwa wapo wananchi mbali mbali wenye ujuzi au elimu kwenye fani mbalimbali. Hivyo tukihimiza ushirikishaji wa mawazo mbadala nakutoa nafasi kwa wananchi kutoa ushauri au mtazamo kwenye huduma tuzitoazo tutapiga hatua kwa kasi zaidi kuliko kufikiri sisi ndiyo tunaojua kila kitu.
Last but not list jeshi letu la polisi wajipange kufanya kazi kisasa zaidi nakuweka mbele matumizi ya teknolojia ili ku detect nakuzuia uhalifu. Pia waweke ukaribu na wananchi ili waweze kuwapa taarifa mbalimbali zenye kuboresha ulinzi na usalama au kuzuia uhalifu.
Niishie hapa kwakutoa pole kwa wale wasiopenda maandishi marefu. Niseme tu mimi siyo mwandishi ila ni mwananchi mzalendo ninayejaribu kutoa mawazo yangu ili kwa pamoja tulijenge taifa letu!
Nakaribisha mawazo zaidi yote tukiyaelekeza kwa serikali yetu na viongozi walioko madarakani.
Nawatakia kila la kheri mwaka 2016.
Let this year be the year to think outside the box!