Wito kwa wazazi wote wa Tanzania. Ni wakati muafaka sasa wazazi turudi kwenye majina ya asili ya Afrika(Tanzania)

Chrismoris

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
13,550
16,631
Tunapokataa tamaduni za kigeni tusiishie kwenye mavazi yasiyo na heshima na ushoga. Ifike kipindi tuanze kutumia majina yetu yenye asili ya Afrika na kuachana na majina ya ku import. Wazazi tulio wengi tumeacha utamaduni wa kuita watoto zetu majina yenye asili ya Afrika.

Zamani ilikuwa kasheshe umzae mtoto asipewe jina lenye asili ya kiafrika ... Siku hizi tumeenda mbali tunatumia majina tunayoyaona kwenye movie na series za nje.

1.Nolan
2. Stich
3. Ian
4. Ivy Augus
5. Alsina
6. Trump
7. Michael Scolfield
8. Vladmiracovic
9. Salah
10. Torah

Badala ya majina yetu ya asili kama vile.
1.Mwarekwa
2. Ngamaka
3. Njobelo
4. Mlekwa
5. Kokubanza
6. Chausiku
7. Sikudhani
8. Togolani
9. Themdidi
10. Ngudua
11. Nangumbi na kadhalika.

Ebu wazazi wa leo tuungane kuyaenzi majina yetu ya asili.

Mimi binafsi nimeshaenda kuapa mahakamani na kubadili jina langu la ubatizo (James Alberto) na sasa nitakuwa nikiitwa Mfadule Mwakupenda.
 
Dogo Umeleta thread yenye Akili leo, watanzania wengi tumekuwa malimbukeni hata lugha mama zetu tumekuwa tukizikataa, kuna dada mmoja nilimkuta mwendokasi pale ubungo maji akiongea kilugha na mama yake nadhani, kwakuwa anaongea lugha mama ambayo pia ni yangu na naielewa nikamsalimia kilugha.. akachuna kumuuliza wewe sio wa Kabila hili?? akaasema NO, Nikasema Poaa.. Nikamtukana Bonge la Tusi kwa Kilugha... Nikashangaa sasa Mbona unanitukana? Nikamwambia aah si umesema Hujui? umeelewaje kama ni tusi?

Ndugu zangu turudi kwenye Asili yetu, kabila langu mtoto akizaliwa atabatizwa na Kupewa Jina la Kikristo lakini at the same time atapewa na jina la Asili, ajabu siku hizi wengi hawa practice hiyo Mila na inaenda Kupotea..

Tuamke!
 
Shule na kwenye document zake atatumia jina lipi la asili au la kanisani ?
 
Majina ya asili yamebaki kwenye majina ya mwisho tu. Kuna haja kufanya kama Wamarekani weusi walioamua kutunga majina yao na pia kutumia majina ya asili ya Kiswahili mwanzoni mwa miaka ya sitini
 
Back
Top Bottom