Wito Kwa Watanzania:Tuitumie Nguvu ya Kauli, Kumuingiza Ikulu Kiongozi Tunayemtaka!. Mdomo Huumba!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,463
113,532
Wanabodi,

Jumapili ya leo. nimepata tena fursa ya kuwahamasisha Watanzania, tujitokeze kwa wingi kupiga kura. Mada yangu ya leo ni nguvu ya kauli za ushindi!.

Kuna msemo, kuwa mdomo huumba, au kauli huumba!.

Kitu chenye nguvu kuliko kitu kingine chochote hapa duniani, ni nguvu ya nia, "will power". Hii no kuweka nia ya dhati kwenye jambo lako, hiyo nia inakuwa ina nguvu na kulifanya jambo lako litokee!. Hata wenzetu Waislamu, wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hutakiwa kuweka nia ya kufunga kwa kunuizia!, kila siku kabla ya kuanza mfungo wa siku inayofuata!. Ukifunga bila kunuizia au bila kuweka nia ni kujishindia tuu na njaa!.

Will Power ni Nini?.
Hii ni nguvu ya Mungu iliyomo ndani yetu ambayo inauwezo wa kufanya kila kitu!, where there is a will, there is a way!, yaani penye nia, pana njia!.
Rejea mada zangu hizi!.
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo
"Will Powers!", "Faith Healing!"-Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani

Kauli hizo ambazo hii miongoni mwake ni kauli inayoitwa laana!. Kuna watu wanadhani laana ni lazima mtu mwingine akulaani, kumbe sisi bila kujijua, unaweza kujikuta unajilaani mwenyewe kwa kauli zako bila kujijua, halafu yakikufika, huku nyuma watu wanaanza kumtafuta mchawi!.

Kujilaani huku sometimes ni kwa kujitakia lakini bila kujijua!. Hata kauli hizi za kujikubali kuwa sisi ni masikini, ni kujilaani na tunakuwa masikini kweli!, kumbe bila kujijua, hata ukiwa masikini vipi, ukijiwekea kauli kuwa mimi ni tajiri, kauli hiyo inakuumbia utajiri, na mwisho wa siku, unakuwa tajiri kweli!.

Naomba niwape ushuhuda wa nguvu ya kauli kwa kutolea mfano, kifo cha Mchungaji Mtikila (RIP), miaka 5 nyuma wakati tukijiandaa kwa uchaguzi wa 2010, nilikutana ana kwa ana na Mchungaji Mtikila, na kufanya nae mazungumzo ambayo nilipandisha uzi huu, humu jf, Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100!

Katika pita pita zangu mchana wa leo jiji Dar es Salaam, nimekutana
na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila katika ofisi fulani, yeye kaja na yake, nami na yangu hivyo tukaa waiting room pamoja kumsubiria mwenyeji wetu.
huwezi amini alinichangamkia sana na tukaanza kuchat.

Kwanza nilimuuliza kwa nini wapinzani hawaungani?.
Jamaa alishusha nondo nzito kwa kubonda wapinzani wote kuwa Tanzania, hakuna mpinzani yoyote isipokuwa ni yeye tuu!, tena kuhusu Chadema, ndio usiseme kabisa, eti ni afadhali ya CCM!. Alisema mengi kwa lugha kali na matukano kibao, huku akizungumza kwa sauti ya juu, ofisini kwa watu!.

Nikamsisitizia, kwa vile chama tawala ni CCM, vingine vyote ni upinzani, jee haoni kuikandia Chadema na CUF at this time ya kuelekea uchaguzi mkuu ni kuikampenia CCM kwa mlango wa nyuma?, au ameshikishwa kidogo dogo?!.

Jamaa aliwaka sana akasema CCM imshikishe nani pesa, hapa nilipo, japo sina pesa ila nimekataa hongo ya milioni 100! toka kwa ....(akamtaja jina....) naomba nilihifadhi ili kuilinda hadhi ya JF, maana huyu mtu kwa JF, ni "mtakatifu fulani" sana humu jf, na ni mmoja wa waheshimiwa wetu kitaifa, hivyo anaheshimiwa sana tuu humu jf!

"Niligundua kuwa ... (akamtaja) ni muuaji, anatoa pesa kutuma assasins kutekeleza mauaji mbali mbali na kisha kufake accidents!, alitoa shilingi milioni 120 kuwapa Wakenya fulani wawili kumuua ...(akamtaja..), ushahidi ninao!.

Mtikila akaendelea kudai kuwa, Mfanyabiashara huyo tajiri alipomgundua siri yake ya mauaji imefichuka, kwanza alimuita kwenye(Mtikila) kwenye moja ya vitega uchumi vyake (akataja siku, muda na mahali) akampa offer ya hongo ya Sh. Millioni 10 ili afute jina lake kwenye dossier ya wauaji. Mtikila akamkatalia.( Akimaanisha analo andiko hilo la mauaji!).

Mara ya pili (tajiri) huyo alimuita ofisini kwake, (akataja siku, muda na osisi ilipo!) akapanda dau toka ile milioni 10! mpaka milioni 50!, bado Mtikila alizikataa!. Ndipo tajiri huyo akamuita Mtikila nyumbani kwake (akataja siku, muda na eneo nyumba ilipo!) akampa offer ya Sh. Millioni 100!. Ndipo Mtikila alimkubalia kwa shurti ya tajiri huyo, kwanza ampigie magoti yeye Mtikila na akiri dhambi zake, na pili atubu kwa Mungu, Mungu akishamsamehe ndipo yeye Mtikila, ataipokea hiyo pesa kama asante yake!.

Tajiri akagoma kukiri na akagoma kutubu!. Ndipo Mtikila akasimama akatoka nje!, ila anadai kila kitu amerekodi kwenye digital sound recorder yake, na sasa anasubiri tuu time muafaka ili amlipue!.

Na baada ya maelezo yote haya ya kukataa hongo ya milioni 100!, Mchungaji Mtikila alimalizia kwa ...(nakihifadhi)

Paskali
Nimekitumia kisa hiki kama ushahidi wa nguvu za kauli kuhusu la tuhuma za mauaji kwa ku fake accidents!, wajameni "karma' is real!, mdomo huumba!, au kauli huumba!.

Nawaombeni sana wanasiasa wetu na sisi wana jf tuchunge sana kauli zetu! na haswa kipindi hiki cha uchaguzi. Kama ni kweli huyo tajiri muuaji kwa ajali za kupangwa ndio ametekeleza mauaji hayo, then, ushahidi wote upo na utawekwa hadharani na mwisho wa siku, karma pia itamfika muuaji huyo!.

Lakini kama sio kweli, bali ulikuwa ni uzushi tuu, then, masikini Mchungaji Mtikila, alijiumbia kifo chake yeye mwenye kwa kauli yake ya fake accident kwenye yale mazungumzo yetu!. Karma haikwepeki!, lakini kama Mtikila, alimzushia tuu, jambo kubwa kama hili!, then ni kauli ya Mtikila ndio iliyokiumba kifo chake!, na kweli amekuja kufa kwa accident yenye utata sana like a fake accident!.
Mungu ampumzishe kwa amani Mchungaji Mtikila.

Mfano mwingine wa kauli zinazoumba ni huu.
Tarehe 1 mwezi wa 8 mwaka 2008, kuna mwana JF mmoja alipandisha uzi fulani humu jf, kuhusu member fulani wa jf anavyoendesha vibaya pikipiki!. Wachangia wa uzi ule walitoa kauli mbaya kumhusu huyo jamaa wakizungumzia atapata ajali!, na baada ya siku 4, huyo jamaa aliyezungumziwa ni kweli, alipata ajali mbaya mbaya ya pikipiki na hadi sasa bado hajapona!. Baada tuu ya kutokea kwa ajali hiyo, mode waliofunga ule uzi, na kuufuta kabisa!. Jamaa apata ajali.
Soma watu walisema nini,

Mdau Mpoki Bukuku wa Mwananchi na The Citizen anatujulisha kwamba Mwandishi wa siku nyingi na mtangazaji ambaye pia ni mjasiliamali amepata ajali mbaya ya pikipiki amepata majereha sehemu mbalimbali za mwili ikiwa namkono ambao umepoteza mawasiliano na sehemu nyingine za mwili.
Kuna watu hapa bodini wana midomo kama manabii.
Nakumbuka haijapita wiki tangu ile thread ya kuhusu kuendesha pikipiki ijadiliwe hapahapa. Na wengi tulipendekeza ile thread ifungwe kwani ilikuwa haina maslahi kwa jamii.
There was mention of someone meeting a biker in one of the threads ..... and some comments were made - similar to what has happened.
Kuna watu wali observe kuwa anaendesha reckless, haujapita muda ajali.Hivyo "midomo kama manabii".Wameweza kuonya kabla na hatimaye wamekuwa vindicated.
Nakumbuka haijapita wiki tangu ile thread ya kuhusu kuendesha pikipiki AINGESOMa asingefika huko kwenye ajali huu ndio umuhimu wa JF FUNDISHA
nakumbuka siku si nyingi kuna mwanajf aliandika kua mtu huyu (superstar wa bongo pm)anaendesha pikipiki kwa fujo sana huko mitaani na hivyo anaweza kusababisha athari za maisha watu wakamjia juu kua si kweli.............. yamaetokea. ama kweli lisemwalo laja.....loo,
Hivyo wandugu, huu ni uthibisho wa kuwa kauli huumba!. Tuzitumie kauli zetu kuumba mema na sio maovu!. Wish the people all the best all the time and not the worst!.

Tuwe Makini sana na kauli zetu na haswa kipindi hiki cha uchaguzi, kauli kama bao la mkono, wizi wa kura, nchi kutotawalika, au fulani atashindwa, kauli hizo ndizo zinazoyaumba matukio hayo!.

Na kwenye uchaguzi huu, mshindi wa uchaguzi, utatokana na kauli nyingi zaidi za kutamka na ku wish kwa dhati kuwa fulani ndio atashinda!. Kauli hizi ndizo zitakazo umba ushindi kwa mgombea wako!.

Mfano: Ikitokea Watanzania wengi zaidi, wana wish Lowassa ndie ashinde uchaguzi huu, then wakitamka kuwa Lowassa ndio mshindi!, amini usiamini, Lowassa ndie atakuwa rais wetu!, hata CCM inunue media zote, iweke matangazo yake kwenye redio na TV zote, magazeti yote na kwenye billboards zote nchi nzima, bado atakayeshinda ni Lowassa kwa sababu kauli ya wengi ndio kauli ya Mungu!. Rejea
Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi ..
Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 2015!.
Namalizia kwa kukusisitiza, tumia nguvu iliyoko ndani ya kauli yako, kumfanya mgombea wako ashinde uchaguzi!, kura zitatumika kukamilisha tuu taratibu za kuhalalisha!.

Hivyo ewe Mtanzania, uwe ulijiandikisha au hukujiandikisha, tumia nguvu ya kauli ya ushindi kwa kiongozi unayemtaka, atashinda kwa kauli kwanza, lakini usibweteke na ushindi wa kauli, bali siku ya kupiga kura, jihimu uende kwenye kituo cha kupiga kura na upige kura yako, ili kumthibitisha kiongozi unayemtaka!.

Kwa upande wangu nimeobserve haya!.
Kwa Hali Niliyoishuhudia Leo Old Bagamoyo Rd: There is No Way CCM inaweza Kushinda!.
Kama Kipimo Cha Ushindi ni Idadi ya Watu, Then, Lowassa Ndiye Rais
Kama Ushindi wa Uchaguzi Utatokana na Wingi wa Mabango na Matangazo. CCM ndie mshindi!.
Nawatakia jumapili Njema.

Paskali
 
Propaganda at its best!

Kama mdomo huumba basi watu wangekuwa wanasema mimi sitaki nife milele na wangeweza kuishi milele.

Kinachoumba ni Tafiti/uchunguzi.

Bila logic, thinking, and reasoning huwezi kuumba lolote.

Tafiti/chunguzi zilizofanywa zimeonyesha Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania hata kama utahamasisha watu wengi wakapige kura.
 
Mkuu,MsemajiUkweli, hii sio propaganda bali ni reality, yaani ndio ukweli wenyewe!.

Jee hujawahi kusikia ule msemo wa "lisemwalo lipo kama halipo linakuja"
unamaanisha kuna jambo ukilisema, unakuwa umeliumba, then linatokea kweli!.

Au hujawahi kulisikia neno hili "sema neno moja tuu na roho zetu zitaponywa!".

Au unaijua nguvu ya sala inatokana na nini?, au nguvu ya maombi inatokana na nini?!, kauli!.

Mungu ndio aliyetuumba hivyo anaona shida zetu zote na mahitaji yetu bila hata kuyataja, hata ukisali kimoyo moyo ukiwa kimya kabisa, au kufikiria tuu, Mungu tayari anasikia, but ,why watu wanasali kwa sauti?!, ni kwa sababu kauli huumba!.

Nimefanya utafiti nikagundua, hata ukiombwa pesa na mwenye shida, ukajifanya huna pesa kwa kauli za "sina kitu kabisa!", then unajiumbia kuchacha na ni kweli unakuja kuishiwa kabisa!. Lakini ukiombwa pesa huku ukiwa huna kitu kabisa, ukisema nikipata nitakusaidia, amini usiamini, utapata pesa na utamsaidia huyo mwenye shinda!.

CCM imekuwa ukituaminisha kuwa Tanzania ni masikini, na Watanzania ni masikini, na ni kweli, Tanzania imekuwa masikini, na Watanzania tumekuwa masikini kiasi kwamba kimepelekea rais wetu mpendwa, Dr. Jakaya Kikwete siku zote kulazimika kusafiri kwenda nje ya nchi kutembeza bakuli, tena huku akiwa very proud kuomba na kulifanya taifa letu ni taifa la omba omba!. Hivyo kuichagua tena CCM ni kuuchagua umasikini!, hivi kweli kuna mtu mwenye akili zake timamu, anayejua umasikini wa taifa letu ni umasikini wa kujitakia tuu na umesababishwa na CCM, lakini bado akaichagua tena CCM?.

Lowassa amesema wazi, Tanzania sio nchi masikini, Tanzania ni nchi tajiri, yeye sio masikini, ni tajiri kwa sababu ametoa kauli ya kuuchukia umasikini. Amesema nchi hii ina rasilimali za kutosha kuwezesha kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, ukimchagua Lowassa, unsakuwa umeamua kuachana na umasikini ambao CCM imeuumba kwa kauli zake, na badala yake sasa tunafanya mabadiliko hadi ya kauli, kuwa ukimchagua Lowassa, umeuchagua utajiri!.

Sasa nakushauri hata wewe hapo ulipo, hata kama ni mwana CCM, na ulipanga kumchagua Magufuli, usibadilishe chochote katika msimamo wako huo, bali sema neno moja tuu kati ya kuchagua umasikini au utajiri!, kauli yako tuu ndio itamaliza kila kitu!.

Pasco

Kama kauli inaumba, basi JPM ndie Rais wa 5 wa JMT.
Mkuu Freema Agyeman,

Uko very right, kauli inaumba, hivyo kitendo cha kutoa kauli ya ushindi kwa chaguo lako, JPM, then unamuumbia ushindi JPM, sasa ili JPM ndie awe mshindi, ni lazima hizo kauli zinazomuumbia ushindi, ziwe ni nyingi kuliko za Lowassa, hili likitokea, then hakuna ubishi, rais wetu 2015 atakuwa ni JPM!.

Pasco
 
Propaganda at its best!

Kama mdomo huumba basi watu wangekuwa wanasema mimi sitaki nife milele na wangeweza kuishi milele.

Kinachoumba ni Tafiti/uchunguzi.

Bila logic, thinking, and reasoning huwezi kuumba lolote.
Tuchunge sana kauli zetu, kauli huumba!.

P.
 
Ndg Mayalla. kwa Ujuzi wangu katika maisha nimegundua Hakuna mwanadamu Maskini, ila umaskini uanzia kichwani na matokeo udhiirika mwilini, ukitaka kuwa Bilionea Badili fikra zako jinsi unavyowaza, na ukitaka kuwa maskini endelea kuwaza kushindwa na kulalamika utakuwa maskini wa kutupwa.

Siku zote fursa za kufanikiwa uwa zimesitirika sana uonekanatu kwa wale wanao waza kinyume na mazingira.huwezi kuwa tajiri kama fikra zako hazikubaliani wewe ni tajiri,unapoanza kuwaza tofauti na kujitamkia maneno ya ushindi na kufanikiwa kamwe mwili wako hautoweza kutoa ushirikiano wa kutekeleza yale unatoyakiri maana maneno ni Nguvu na Mwongozo wa mwili.

computer kama chombo uendeshwa na program zilizoingizwa ndani yake! vivyo mwili utegemea mawazo kujiendesha, hivyo ukitaka kuwa tajiri utajiri uanzia kichwani na mwili ni mtekelezaji. watanzania wanalalamika Vyuma vimekeza!!!!! uo ni uvivu wa kufikiri unaopelekea kuzubaa kwa mwili katika kuona fursa na kutengeneza fedha. Mimi Binafsi Nampongeza sana Mh Magufuli. kwa kuwafanya watu wafikiri zaidi na kufanya kazi. Taifa hili lillikua Watu hawafanyi kazi na kupelekea kuwa Taifa la watu Tegemezi.

Mimi Tangu Rais Magufuli Aingie Madarakani nilibadilika Kufikiri kwangu Kulikopelekea Kunifanya Nifokasi zaidi kwenye Biashara zangu kulikopelekea Kuwa Bize Muda Wote na Kutengeneza Pesa Nyingi sana kwa Muda Mchache kabisa, hivyo kama unataka kuendelea kuwa maskini wewe ilaumu Serikali Mwanzo wa Asubui mpaka jioni na kumtukana Mh Rais na kuhakikishia utakuwa mtumwa na homba hoba katika nchi yenye utajiri mkubwa ila watu wake ni maskini wa fikra.

Nakutakia Siku Njema Ndg Paskali.
Mkuu Prince Crown, angalia hapa nilisema nini?.
Wanabodi,
Jumapili ya leo. nimepata tena fursa ya kuwahamasisha Watanzania, tujitokeze kwa wingi kupiga kura. Mada yangu ya leo ni nguvu ya kauli za ushindi!.

Kuna msemo, kuwa mdomo huumba, au kauli huumba!.

Kitu chenye nguvu kuliko kitu kingine chochote hapa duniani, ni "will power". Hii ni nguvu ya Mungu iliyomo ndani yetu ambayo inauwezo wa kufanya kila kitu!. Rejea mada zangu hizi!.
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo
"Will Powers!", "Faith Healing!"-Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani

Kauli hizo ambazo hii miongoni mwake ni kauli inayoitwa laana!. Kuna watu wanadhani laana ni lazima mtu mwingine akulaani, kumbe sisi bila kujijua, unaweza kujikuta unajilaani mwenyewe kwa kauli zako bila kujijua, halafu yakikufika, huku nyuma watu wanaanza kumtafuta mchawi!.

Kujilaani huku sometimes ni kwa kujitakia lakini bila kujijua!. Hata kauli hizi za kujikubali kuwa sisi ni masikini, ni kujilaani na tunakuwa masikini kweli!, kumbe bila kujijua, hata ukiwa masikini vipi, ukijiwekea kauli kuwa mimi ni tajiri, kauli hiyo inakuumbia utajiri, na mwisho wa siku, unakuwa tajiri kweli.

Leo nafanya mapitio ya baadhi ya kauli zangu ambazo hatimaye zilikuja kuumba hilo jambo nililolizungumza.
....

P
 
Wanabodi,

Jumapili ya leo. nimepata tena fursa ya kuwahamasisha Watanzania, tujitokeze kwa wingi kupiga kura. Mada yangu ya leo ni nguvu ya kauli za ushindi!.

Kuna msemo, kuwa mdomo huumba, au kauli huumba!.

Kitu chenye nguvu kuliko kitu kingine chochote hapa duniani, ni nguvu ya nia, "will power". Hii no kuweka nia ya dhati kwenye jambo lako, hiyo nia inakuwa ina nguvu na kulifanya jambo lako litokee!.

Na kwenye uchaguzi huu, mshindi wa uchaguzi, utatokana na kauli nyingi zaidi za kutamka na ku wish kwa dhati kuwa fulani ndio atashinda!. Kauli hizi ndizo zitakazo umba ushindi kwa mgombea wako!.

Mfano: Ikitokea Watanzania wengi zaidi, wana wish Lowassa ndie ashinde uchaguzi huu, then wakitamka kuwa Lowassa ndio mshindi!, amini usiamini, Lowassa ndie atakuwa rais wetu!, hata CCM inunue media zote, iweke matangazo yake kwenye redio na TV zote, magazeti yote na kwenye billboards zote nchi nzima, bado atakayeshinda ni Lowassa kwa sababu kauli ya wengi ndio kauli ya Mungu!.

Namalizia kwa kukusisitiza, tumia nguvu iliyoko ndani ya kauli yako, kumfanya mgombea wako ashinde uchaguzi!, kura zitatumika kukamilisha tuu taratibu za kuhalalisha!.

Hivyo ewe Mtanzania, uwe ulijiandikisha au hukujiandikisha, tumia nguvu ya kauli ya ushindi kwa kiongozi unayemtaka, atashinda kwa kauli kwanza, lakini usibweteke na ushindi wa kauli, bali siku ya kupiga kura, jihimu uende kwenye kituo cha kupiga kura na upige kura yako, ili kumthibitisha kiongozi unayemtaka!.

Nawatakia jumapili Njema.

Paskali
Mlengwa wa bandiko hili ilikuwa ni Edward Lowassa

Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Back
Top Bottom