Wito kwa Wananchi kuiangamiza CCM hawa ni mafisadi tu kama waliongamizwa zamani.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Kusema kweli Miccm au tuseme CCM ni chama ambacho kimejaa mafisadi tena mafisadi wa kimataifa (dili za Kimataifa) ,yote imesababishwa na wananchi kuwa watu watulivu kupita kiasi utulivu ambao sasa umeanza kutoweka.

Hawa huifisidi hii nchi ,nchi iliyojaaliwa kila neema ,neema ambazo huko majuu hazipo ,sisi tuna mbuga za wanyama kuna nchi zina ZOO tu na zinasaidia uchumi wa nchi ,huku kwenye mbuga na maziwa ni utajiri tosha ambao ungeweza kutatua mambo mengi sana kama si yote.

MiCCM na serikali yao imekuwa kama nuksi kwa miaka yote hamsini iliyopita ,badala ya nchi kusonga mbele tunazidi kudumaa ,ukiwasikia mafisadi wanasema tujiajiri wenyewe nenda katafute kibali uone mtaji wote utamalizika katika kutafuta kibali na ukikipata ni bahati yako.

Mwenyezi Mungu katika zama zilizopita mafisadi walikuwa akiwaangamiza kwa dhoruba mbalimbali ,kuna mafisadi waliojiona wao ni miungu kuna waliojiona wao ndio wenye mali za dunia nzima kuwa wao ,yaani dizaini kwa dizaini za mafisadi na hawa maccm tulionao inaonyesha dhahiri wameshaanza kuvuka mipaka ,hata wakipata matatizo ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu wanakuwa hawatanabahi kuwa wao ni viumbe dhalili kabisa ,wanajiona kama vile wameumiliki uhai wao na upo mikononi mwao ,wataishi milele ,aloo haikuwa firauni alitiwa mkononi ,itakuwa nyie mnaekwenda chooni asubuhi na mchana ,mkiumwa mnasafiri masafa kutafuta tiba ,oleni sana.

Tusingojee Mwenyezi Mungu kutuadhibia watu hawa ,kwani kama tutawapa sapoti hasa kwa kupitia hizi tunazoziita chaguzi basi adhabu ikifika haichagui itatuchanganya sote na si ajabu wale wanaowapa kura wakapata taabu zaidi na mifano midogomidogo ipo.
Angalieni mahospitali,mashule na sehemu nyengine kunakohitajiwa huduma ,ni shiida tupu maji umeme mifumuko ya bei maisha kuwa magumu ,hizi ni adhabu nyepesi nyepesi sana ,na ukiangalia utaona walewale wanaoipa sapoti CCM kwa kuwapa kura wamo wanajumuika ndani ya dhiki ni lazima muamke na kuona tunakoelekea sipo na wala siko ,kuvuka mitihani ya aina hii ni kuikataa CCM katika sanduku la kura,wakiiba hizo kura yupo anaewaona na aliekuona na utakuwa umeshatimiza wajibu wako.

CCM tuanze kuingamiza sisi wananchi katika upigaji kura ,hawa si watu wa kuwapa kura yako hata waje na maneno matamu ya aina gani ,ni wa kuepukwa na kama yupo kiongozi anajiona mzalendo na yupo CCM na aondoke huko kwa haraka sana ,wananchi wazalendo wote wapo katika kuipinga CCM wewe unabaki huko kufanya nini ,ungana na wenzako ili kuiangamiza CCM ,ni sehemu ndogo sana imebaki hiki chama kuondoka katika siasa ,ila kubakia kukiunga mkono ni kuwapa nafasi kuzidi kufanya ufisadi kwa njia zilizongumu kuzigundua.
 
Back
Top Bottom