Wito kwa WanaJF: JF Member anapokufa, je, tuanze kuonesha solidarity yetu kama msiba wa Regia, au tuache tu kila mtu na bahati yake na hadhi yake?

Wanabodi,
Kiukweli mimi ni follower mzuri wa Jukwaa la Siasa, halafu majukwaa mengine kutembelea mara moja moja.

Sasa jana, kutokana na Tanesco kutufanyia vitu vyake toka asubuhi, kwa wengine umeme ndio kila kitu, hivyo leo nikazianzia mapema tuu ile saa 10 tayari niko viti virefu, by saa 2:00 usiku nimeisha pindua gari, hivyo kufika saa 8 usiku, usingizi umakata. Mtu anabaki kuhesabu kelechi na hizi nyumba zetu za kupanga ambazo hazina siling board, na usiku wa manene ulivyo utulivu, unajikuta unayasikia yanayoendelea chumba cha jirani, kuna sauti na sauti, lakini sauti nyingine kiukweli, usingizi ndio unakata kabisa, nikajikuta naingia MMU, ndio usingizi ukakata kabisa baada ya kukuta taarifa ya kifo cha member maarufu number 1 wa jf kule MMU na Celebrity Forum.

Duh..., japo mimi sio mwanachama active wa celebrity forum, ila jamaa namkubali sana na nimeguswa.

Zamani JF ilikuwa tukipoteza mwanachama, if management ilikuwa inafanya some sort of organisation, nakumbuka msiba wa Regia if tulitengeneza hadi Tshirts na tuka jiorganize hadi kuhudhuria mazishi kule Ifakara, tena kuna member alijitolea gari yake!
Hebu tazameni hapa chini


I don't know what happened now. Should we push for equal treatment during the demise of our members, tuweke system ya ndugu kuripoti kwa jf management kifo cha mwanachama wetu yoyote regardless umaarufu wake, kisha waweke number ya mchango, wana jf kuchangie, na siku ya kuaga jf management iwepo na kukabidhi mchango kwa wakiwa na mtu wa jf atoe neno.

Na kwenye mazishi ya wana jf wa eneo husika wahudhurie kutuwakilisha.

Kwenye mchango wa rambirambi hata tukiweka minimum TZS 1,000 tuu, kwa jinsi tulivyo wengi, hiyo fedha ina kuwa ina impact kubwa na ni faraja kwa familia kujua mpendwa wao alikuwa mwanachama wa mtandao wa jf na jf wanajali.

Na kwa vile wengi wa wana jf wanatumia pen names, ili kuheshimu the unanimity ya marehemu, humu jf tuu ndio atatajwa kwa jina lake la jf, mfano huyu warumi , lakini
pale msibani no one will mention his name, hata kwenye Salaam za jf, hatamkwi popote kwa jina, bali "marehemu alikuwa mwanachama wetu, alijinga jf lini, amechangia mada mbalimbali etc just that, na if members watakao hudhuria msiba, kwa vile kule wataliona na kulijua jina halisi, kanuni yetu na "name calling" iwe strictly observed kumuheshimu marehemu kwa kutolitaja jina lake halisi, maadam humu kwetu alikuwa warumi , then he/she will always be warumi.

Hivyo naomba kutoa wito wa swali kwa sisi wana JF, JF Member are equal, sasa member mwenzetu anapokufa, jee tuanze kuonyesha solidarity kwenye msiba kwa kushiriki na kumuenzi member mwenzetu kama tulivyofanya kwenye msiba wa Regia Mtema?, au tuache tuu hali hii iendelee kwasababu kila mtu na bahati yake na hadhi yake na umaarufu wake?.

Mkuu Maxence Melo , if there is anything jf can do kuhusu huyu fallen hero, let's do something kuonyesha solidarity yetu.
RIP warumi !.
Pasco wa jf, anakulilia.
Paskali
Naunga mkono hoja
 
Kwa respect ya Jf ua n ya kiwango cha juu hata ukiwa public transport ukaona mtu ana buy time yake yuko jf anaperuz baadh ya mada ua inatia moyo sana naunga mkono hoja Maxence Melo Fanya KTU juu ya umoja wetu tutambulke kwenye jamii na tuheshmike kama jamii flan iliojkava kwenye knwolge flan kwa id zetu tuungane pamoja kwenye vtu kama hiv mwenzetu anapotutoka

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Namna pekee itajulikana umekufa ni kama una marafiki wapo humu na wakawa tayari kukuanzishia uzi.

Pia sababu pekee watu wataguswa ni kwa kiasi gani unainteract nao.

Wazo la ndugu kuwasiliana na uongozi wa jf kuripoti kifo ni zuri lakini wengine tunaishi Area Z wazazi na ndugu wapo Area A na hawajui kama nipo JF.

Tutake tusitake swala la bahati litaendelea kuchukua nafasi yake hata kama itakubaliwa member akifa achangiwe.
 
Binafsi siungi mkono michango ya aina hii maana ipo KINAFIKI tu.

Anafariki mtu ambaye hakuwa na ushawishi wowote na itataolewa taarifa ila sidhani kama kuna mtu atajali maana hakuwa na ushawishi humu.

Tumekutana hapa kwa sababu moja au mbili "Habari, Kusoma, na Burudani"

Ikitokea mwenzetu kaondoka basi tuambiwe na watakaoweza kushiriki washiriki kivyao siyo kwa sababu ya JF.

Huu utaratibu wa kuchangia mtu akifariki ni wa KINAFIKI na utakuwa na madaraja kati ya mtu na mtu.

Jamii Forum nashauri tuachane na uswahili wa aina hii tuendeshe mtandao huu kisasa kama mitandao mingine mikubwa duniani.

Akifa mtumiaji wa Facebook au Instagram basi linakuwa suala la wanafamilia na marafiki siyo suala la mtandao.

Sijaongea kwa ubaya lakini ila naona kutakuwa na UNAFIKI kwenye huu utaratibu.
 
Naona haya kwenye magrupu ya WhatsApp ya watu wanaofahamiana kabisa inavyokuwa ngumu kutekelezeka. Sembuse hapa ambapo hatujuani kabisa?

Mi nadhani liwe jambo la hiari kwa watakoguswa. Namba inatolewa watu wanachanga...

Tatizo naloliona hapa, nikituma hela kwa mchangishaji, mara paap anaona jina la mtumaji ni mimi niliyekuwa natukanana naye jamvini, kumbe ni bosi wake kazini.... Lahaula lakwata! Kumbe bosi yuko JF anamwaga pumba kichizi.
mara paap anaona jina la mtumaji ni mimi niliyekuwa natukanana naye jamvini, kumbe ni bosi wake kazini.... Lahaula lakwata! Kumbe bosi yuko JF anamwaga pumba kichizi.

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Hivi mnajuaje kama member wa JF kafa ?
Yaani unafikiri nini kazi ya Mshana Jr humu ndani? Bundi wake wanasoma nani anafuata sasa? Kisha wanampa taarifa.


Humu ndani kuna members wanafahamiana physically na ni marafiki, hao ndio hutupasha habari.

Mathalini, mimi na Mshana Jr ni marafiki hadi nje ya ulingo. Iwapo umauti ukinifika lazima atajua, atakuja kuwapasha ndugu zanguni wa JamiiForums habari.
 
Wanabodi,

Zamani JF ilikuwa tukipoteza mwanachama, Jf management ilikuwa inafanya some sort of organisation, nakumbuka msiba wa Regia if tulitengeneza hadi Tshirts na tuka jiorganize hadi kuhudhuria mazishi kule Ifakara, tena kuna member alijitolea, usafiri wa gari yake, akajaza mafuta, akawasomba jf wakatia timu kuhudhuria mazishi, Ifakara.
Hebu tazameni hapa chini

I don't know what happened now. Should we push for equal treatment during the demise of our members, tuweke system ya ndugu kuripoti kwa jf management kifo cha mwanachama wetu yoyote regardless umaarufu wake, kisha waweke number ya mchango, wana jf kuchangie, na siku ya kuaga jf management iwepo na kukabidhi mchango kwa wafiwa na mtu wa jf atoe neno.

Na kwenye mazishi ya wana jf wa eneo husika wahudhurie kutuwakilisha.

Kwenye mchango wa rambirambi hata tukiweka minimum TZS 1,000 tuu, kwa jinsi tulivyo wengi, hiyo fedha ina kuwa ina impact kubwa na ni faraja kwa familia kujua mpendwa wao alikuwa mwanachama wa mtandao wa jf na wana jf wanajali.

Na kwa vile wengi wa wana jf wanatumia pen names, ili kuheshimu the anonymity ya marehemu, humu jf tuu ndio atatajwa kwa jina lake la jf, mfano huyu warumi , lakini
pale msibani no one will mention his name, hata kwenye Salaam za jf, hatamkwi popote kwa jina, bali "marehemu alikuwa mwanachama wetu, alijinga jf lini, amechangia mada mbalimbali etc just that, na if members watakao hudhuria msiba, kwa vile kule wataliona na kulijua jina halisi, kanuni yetu na "name calling" iwe strictly observed kumuheshimu marehemu kwa kutolitaja jina lake halisi, maadam humu kwetu alikuwa warumi , then he/she will always be warumi.

Hivyo naomba kutoa wito wa swali kwa sisi wana JF, JF Member are equal, sasa member mwenzetu anapokufa, jee tuanze kuonyesha solidarity kwenye msiba kwa kushiriki na kumuenzi member mwenzetu kama tulivyofanya kwenye msiba wa Regia Mtema?, au tuache tuu hali hii iendelee kwasababu kila mtu na bahati yake na hadhi yake na umaarufu wake?.

Mkuu Maxence Melo , if there is anything jf can do kuhusu huyu fallen hero, let's do something kuonyesha solidarity yetu.
RIP warumi !.
Pasco wa jf, anakulilia.
Paskali
Zamani when jf was small, jf used to do something kwenye misiba ya members wake waandamizi, Sanctus Mtsimbe aliwahi kuwa a Tanzanite member.

I thought, kwa vile msiba huu ilikuwa hapa Dar, jf should have done something kwa kutushirikisha,
Mimi kwa upande wangu,
1. Kwanza nilichangia uzi wa msiba
2. Nikaandika Buriani.
3. Nikaandika makala kwenye gazeti
4. Nikahudhuria mazishi Kinondoni makaburini.

Should Jf do more member anapotangulia mbele ya haki.
P
 
Back
Top Bottom