Wito kwa Wana JF wote: Maombi maalumu kwa ajili ya Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli

Mkuu tunaomba sana usichokijua pia maombi ni mashtaki kwa Mungu kwa unayemuombea asiye na hofu ya Mungu. Aliye na visasi, muuaji, asiyetenda haki etc etc
 
Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo
Kwa ndugu zangu Waislamu nanyi pia nawasalimu!
Sote tu familia moja ya JF
Leo tarehe 01/02/2018 nimerejea tena kuwaomba tuzidi kumuombea Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli. Majukumu aliyokabidhiwa ni makubwa na yanahitaji sio tu ujasiri mkubwa ili kuweza kuyatekekeza ipasavyo bali pia yanahitaji mibaraka ya Mungu.
Kama mwana familia ya JF usiku huu tena nawaomba kwa unyenyekevu mkubwa kuwa m zidi kumuombea Kiongozi wetu mpendwa ili afanikishe yale yote aliyokusudia kuyafanya kwa faida ya nchi yetu Tanzania. Mjitahidi kutenga muda wetu kwa kumuombea Kiongozi wetu azidi kupata nguvu za kuwatumikia Watanzania wote.
Natambua yapo mengi mazuri aliyofanya hadi sasa na nyie ni mashuhuda wa hayo lakini kumbukeni kuwa yapo mengi pia anayotakiwa kuyakamilisha. Ukweli yote aliyokusudia kuyafanya yatawezekana tu kwa uwezo wa Mungu unaotokana kupitia maombi yetu. Natambua kuwa safari ni ndefu ikiwa na majaribu mengi lakini kwa neema za Mungu tutafika salama kwenye nchi ya ahadi.
Niwashukuru sana kwa kunielewa na Mungu azidi awabariki sana.
Mungu wetu tunakuomba uzidi kumbariki na kumpa ulinzi Rais wetu yeye pamoja na familia yake.
Shetani hana nafasi tena mbele za Mungu
Usiku mwema wapendwa
mnafiki mkubwa wewe, Ben saa nane anaenda mwaka wa pili hajulikani alipo, Tundu Lissu anauguza majeraha, Azory naye alitekwa hajulikani alipo, kuna watu ni wagonjwa mahospitalini hawana msaada, kuna watu wamefungwa bila hatia na husemi tuwaombee, acha kujipendekeza wewe.
 
kwa majibu haya! wengi mnaenda kulala mmenuna na asubuhi wengi mnaamka mmevurugwa matokeo yake kunauwezekanano watu wakaenda ofisini kufikiria weekend na hakuna jipya zaidi ya hasira na matumizi yasiyopangwa
 
Acha masihara basiii mkuu
Jana mama yetu kakulaza mzungu wa 4 nini ..umeamua kuja Jf kujifariji !!

watanzania wengine hata Uhakika wa mlo hawana hizo nguvu za kupaza sauti ili maimbi yao yasikike wanazitoa wapi !!?
 
Imefika hatua nakula msosi mmoja kwa siku.
Then nimuombee kwa lipi aisee.
Mi hamna we Omba mwenyewe lbd baba yako kaishapewa ka uteuzi wenzio sie tulitumbuliwa.
 
Unafiki na wanafiki kama wewe ndio unatugharimu,,,kuwa makini hata kama mamlaka ya juu lazima iheshimiwe,,swali ni hayo maombi yako ni halisi au batili kwa ajili ya maslahi yako...
 
Wee jamaa sio mzima upstairs! Utamuombeaje mtu aliyekataa kutubu! Kwa mujibu wa imani yangu maombi hunoga baada ya kutubu kwanza!
 
Mwenyezi Mungu ni mwenye wivu, kuombea wa as hirizi ni kuwazidushia mikosi
 
Ni kazi yake kutekeleza majukumu ya kitaifa, kumbuka aliomba kazi hiyo mkampa dhamana ya kuongoza nchi, amepewa ulinzi mkali kila anapoenda, kama haitoshi bado unataka tumwombee?? This is too selfish!!
Mtoa uzi ombi lako linawezekana tu kwenye kichwa cha mwendawazimu...
 
Mleta mada umebugi kuleta jambo hili hapa jf, hapa 90% ni ukawa - ndoto zao nikuona ngosha anashindwa tuu!!!
 
Back
Top Bottom