Wito kwa Wana JF wote: Maombi maalumu kwa ajili ya Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo
Kwa ndugu zangu Waislamu nanyi pia nawasalimu!
Sote tu familia moja ya JF

Leo tarehe 01/02/2018 nimerejea tena kuwaomba tuzidi kumuombea Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli. Majukumu aliyokabidhiwa ni makubwa na yanahitaji sio tu ujasiri mkubwa ili kuweza kuyatekekeza ipasavyo bali pia yanahitaji mibaraka ya Mungu.

Kama mwana familia ya JF usiku huu tena nawaomba kwa unyenyekevu mkubwa kuwa m zidi kumuombea Kiongozi wetu mpendwa ili afanikishe yale yote aliyokusudia kuyafanya kwa faida ya nchi yetu Tanzania. Mjitahidi kutenga muda wetu kwa kumuombea Kiongozi wetu azidi kupata nguvu za kuwatumikia Watanzania wote.

Natambua yapo mengi mazuri aliyofanya hadi sasa na nyie ni mashuhuda wa hayo lakini kumbukeni kuwa yapo mengi pia anayotakiwa kuyakamilisha. Ukweli yote aliyokusudia kuyafanya yatawezekana tu kwa uwezo wa Mungu unaotokana kupitia maombi yetu. Natambua kuwa safari ni ndefu ikiwa na majaribu mengi lakini kwa neema za Mungu tutafika salama kwenye nchi ya ahadi.

Niwashukuru sana kwa kunielewa na Mungu azidi awabariki sana.
Mungu wetu tunakuomba uzidi kumbariki na kumpa ulinzi Rais wetu yeye pamoja na familia yake.

Shetani hana nafasi tena mbele za Mungu
Usiku mwema wapendwa

UPDATES:
Hivi sasa ni saa 8:51 usiku
Nimeshaamka naendelea na maombi maalumu kumuombea Rais wetu Dkt John Magufuli.
Tafadhali mwana JF amka na utumie angalao dakika tano tu kumuombea Rais wetu.

Ubarikiwe sana
 
Hoja ndio kuombeana!!
Tangu lini mwenye shida zake atakumbuka kumwombea jirani!!!
Embu tupambane tu na hali zetu kila mtu kwa nafasi yake..
Sidhani kama maombi yataenda ilhali mimi kwangu panawaka moto
 
huyu unayempigia debe aombewe Na tundu lissu nani muhimu kuombewa?? MTU wako Sikh hizi amestuka kuombewa
 
Ili sala ikubaliwa inatupaswa tutubu kwanza. Mshawishi rais wetu anungane nasi kwenye kutubu kabla hatujaanza kumfanyia maombi yaliyotukuka...
acha wafu wazike wafu wao
sijui ni mathayo ngapi...
 
Katika Kusali huwa tunatanguliza Tobaa, Kama Kiongozi Atuongeze sala ya Toba kwanza kisha kama taifa Tutaungana kumuombea.
 
Nilikuwa nimesahau jinsi alivyoshauriwa na Kakobe.

Ivi alishatubu? Au lile lidude alilojifunga ndio Toba yake?

NB:Usipende kutingisha hali za wengine, pambana na Ulumumba wako
 
Back
Top Bottom