Wito Kwa Wakulima: Ni wakati muafaka wa kupandisha bei ya mazao yetu

Fursakibao

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
6,676
11,110
Toka awamu ya sita kuingia madarakani sote tumesguhudia mfumujo wa bei kwa bidhaa mbali mbali huku serikali imekaa kimya.

Vilianzaa kupanda bei vifaa vya ujenzi sasa zimepanda bidhaa muhimu kwa matumizi ya kawaida kwa kisubgizio cha vita vya Ukraine na Urusi.

Bila hata kuwa na haya kiongozi mkuu wa nchi anathubutu kusema hadharani kuwa lazima vitu vipande bei;kwa kauli hii kwa nchi za wengine wenye kujielewa ilikuwa inatosha kuanzisha maandamano ya kuiondoa serikali madarakani kwa njia ya maandamano.

Kwakuwa serikali imeamua kuwabeba wafanyabiashara na dhani sasa ni Wakati wetu wakulima na sisi Kupandisha Bei za mazao yetu ukizingatia sababu tunazo.

Ifike mahali wakulima tugome kuuza mazao kwa bei isiyo na tija kwetu; ASIETAKA ASILE AU AKALIME MWENYEWE.
 
Nia inaweza kuwa nzuri.Kwamba mpate faida na kuweka hata akiba ya fedha.Changamoto itakuja;

-wateja wenu wengi ni wanunuzi wa kawaida.Je,mkipandisha bei watamudu kununua?

-Hoja hii mnataraji kuifanya kwa muda gani ili mpate mrejesho wa nia yenu?

-kupandisha bei ni suluhu ya yaendeleayo?
 
Mkulima hasa wa Tanzania hana uwezo wa kupandisha bei ya mazao yake .... wafanya biashara ndio masterminder wa game hizi.
 
Kama wanaweza kununua mafuta ya kula watashindwa kununua unga?
 
Mkulima hasa wa Tanzania hana uwezo wa kupandisha bei ya mazao yake .... wafanya biashara ndio masterminder wa game hizi.
Ndipo suala la kuthubutu kugoma kuuza linatakuwa ikitokea watu wakagoma kuuza unadhani nini kitatokea?
 
Nimepata maarifa ya kupandisha bei makaranga,maalizeti na maufuta yangu,bei itakuwa hivi
Maalizeti kilo buku 5
Makaranga kilo buku 4
Maufuta kilo buku 6
Mtama kilo buku 4
Hutaki Acha!
Safi sana wakipatikana wakulima kama buku hivi kitaeleweka
 
Ndipo suala la kuthubutu kugoma kuuza linatakuwa ikitokea watu wakagoma kuuza unadhani nini kitatokea?
Hao wakulima Tanzania bado hawapo. mkulima mdogo ambaye anategemea mbaazi zake ili kumudu maisha ya kila siku ataweza kugoma?

Labda wakulima kama kina Sumry ndio wanaweza .
 
Ni kujiendekeza tu ila uwezo hip upo watu wakiamua.

Ngoja tuone mbolea ilivyopanda bei kama watu watauza mahindi gunia kwa 30k
 
Toka awamu ya sita kuingia madarakani sote tumesguhudia mfumujo wa bei kwa bidhaa mbali mbali huku serikali imekaa kimya.

Vilianzaa kupanda bei vifaa vya ujenzi sasa zimepanda bidhaa muhimu kwa matumizi ya kawaida kwa kisubgizio cha vita vya Ukraine na Urusi.

Bila hata kuwa na haya kiongozi mkuu wa nchi anathubutu kusema hadharani kuwa lazima vitu vipande bei;kwa kauli hii kwa nchi za wengine wenye kujielewa ilikuwa inatosha kuanzisha maandamano ya kuiondoa serikali madarakani kwa njia ya maandamano.

Kwakuwa serikali imeamua kuwabeba wafanyabiashara na dhani sasa ni Wakati wetu wakulima na sisi Kupandisha Bei za mazao yetu ukizingatia sababu tunazo.

Ifike mahali wakulima tugome kuuza mazao kwa bei isiyo na tija kwetu; ASIETAKA ASILE AU AKALIME MWENYEWE.
Mazao yenyewe ya kupandisha bro yako wapi? Mvua ya mwaka huu haieleweki.
 
Back
Top Bottom