Wito kwa wachumi nini kifanyike ili nchi yetu uchumi ukue?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Kichwa cha Habari kinajieleza kama wewe ni mbobezi wa uchumi lete hoja hapa ili wachumi wenziyo wadadavue pia Serikali ina masikio mkubwa inaweza kutoa hapa kitu cha kusaidia Taifa.

Angalizo: Kama unakuja hapa njoo bila itikadi ya vyama.
 
Tuache siasa kwenye maamuzi ya MSI GI.haswa bungeni.huku kusema kilakitu ndiyooooo.alafu spika anasema,waliosema ndio kwa kishindo ndio walioshinda Imegharimu hili taiga sana,na sasa tunashindwa tuanzie wapi,imebaki kukurupuka tu.
 
Vijana wajiajiri waache kukaa wanatafuta visingizio. Leo utauliza utasikia ajira hazijatoka, kesho utasikia Kufuli kabana pesa, kesho kutwa excuse nyingine. Hivi mtu anashindwa vipi kuanza kuhangaika mwenyewe kufungua biashara? Kama uoga umejaa a-team up na mtu mwenye uwezo huo acontribute skills zake. Pitia sites kama Kickstarter au Indiegogo: Crowdfund Innovations & Buy Unique Products uone watu wanavyofungua biashara from nothing wanakua funded wanafungua makampuni.

Vijana wabongo wanaolialia nawashangaa sana, nafahamu watu ambao wameanza from zero kipindi hiki hiki cha Kufuli na sasa hivi wanachezea sio chini ya 20m kila mwezi. Huwezi kuta wanalalamika. Waliamua kutumia akili wakaona tatizo flani wakatafuta njia ya kulisolve wakageuza ikawa biashara. From Zero sio kwamba walizaliwa kwenye familia za kitajiri wakarithi. Tukijitahidi kuwa entrepreneurs ipo siku mtu atatengeneza kampuni ikaja kujua kubwa mno ikabadilisha uchumi wa Tanzania moja kwa moja hadi tukashangaa. Angalia mfano wa Samsung group anavyoshika almost 50% ya uchumi wa S.Korea. One major company can transform the entire economy ila tusikae tusubiri Bakhresa au Dangote. Tuwe na hamu ya kufika hapo sisi wenyewe.
 
Mimi si mchumi ila kwa maoni yangu, ili uchumi ukue inabidi kwanza kuwe na uzalishaji unaoenda sambamba ama kwa karibu na population.
Ukuaji wa uchumi unaanzia kwenye ngazi ya familia, kama familia inachozalisha ni kidogo kisichotosheleza familia basi na uchumi kwa ujumla utaathirika, ambao wengi wetu tunaulenga na kuutizamia, kama tujuavyo kuna micro na macro economy, figure zinazopigiwa debe ni za macro economy wakati micro economy inabeba fungu kubwa la watanzania maskini .
 
Back
Top Bottom