Wito kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Kuboresha bajeti na si kusifia bajetii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Kuboresha bajeti na si kusifia bajetii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mo-TOWN, Jun 16, 2011.

 1. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Ni kwa masikitiko makubwa imenibidi kuandika yafuatayo kwa lengo la kuwakumbusha wabunge kilichowapeleka Bungeni

  Nimekuwa nikifuatilia mjadala unaondelea wa bunge la 10 kikao cha 4. Mheshimiwa waziri wa fedha na timu yake wamefanya kazi yao na kuleta muswaada wa bajeti bungeni ili uweze kujadiliwa kwa maana ya kuboreshwa (naamini) na si vinginevyo walau kwa tulio nje ya bunge tunapenda kuamini hivyo.

  Masikitiko yangu ni haya yafuatayo

  1. Wabunge kutojadili kilichoandikwa badala yake kutumia muda mwingi kusifia bajeti ilivyo kuwa na titile za vipaumbele vya wanananchi yaani maji, umeme, barabara, elimu etc

  2. Wabunge kusifia ilani ya CCM ilivyokuwa reflected kwenye bajeti

  3. Wabunge kutumia muda mwingi kure-cite vipengele vilivyoandikwa ktk muswaada na kusema bajeti ni nzuri etc

  4. Unafiki wa wazi wazi wakati mbunge anaona wazi kuna kasoro fulani ktk bajeti

  Kuna mengi ambayo yanaonyesha behavior ya wabunge kutojua hasa kilichowapeleka Bungeni..... no siyo posho

  Nimeseme kuwa Mkulo ameleta bajeti kwa maana ya kuboreshwa na kama ingekuwa iko vizuri serikali isingekuwa na haja ya kuileta bungeni kwa majadiliano ingekuwa inaletwa kwa ajili ya kupitishwa..... hii siyo spirit ya kuwa na hayo majadiliano.

  Ukweli ni kwamba wabunge wa CCM hawaisadii serikali wala chama tawala kwa kutofanya kazi wanayotarajiwa kuifanya vizuri. Ni wakati sasa wabunge wajifunze kuwa sakata la kutokuwa na umeme wa uhakika linatokana na wao kubariki mipango mibovu ambayo mwisho wa siku haisaidii taifa bali inalirudisha nyumba.

  Nitoe mifano michache. Mbunge Ester Bulaya alipokuwa anachangi alianza kwa kusema bajeti ni zuri sana..... naipitisha 100 kwa 100.... etc. Kisha akaanza kusema hana ukakika kama bajeti iliyotengwa ktk eneo la umeme kweli inareflect kuwa hicho ni kipaumbele cha taifa.... aliendelea kufanya uchambuzi mzuri kuonyesha kuwa mwisho wa siku mkakati huo hautafanya kazi jinsi ulivyo na kwa vijijini ambako investment kubwa ya infrastructure ya umeme inatarajiwa kufanywa kiwango kanachokwenda huko ni kidogo sana like 7% kama sijakosea.

  Kwa hakika hayo aliyosema Bulaya ni sahihi na ndicho Mbunge anatarajiwa kufanya nasiyo kuanza kusifia bajeti kisha unaikosoa kwa upande mwingine huo ni unafiki.

  Mbunge mwingine Dr Ndungulile anasimama na kuanza kusifia bajeti na kutaja vipaumbele na kucite ktk ilani ya chama cha mapinduzi. Mimi nadhani haswa hawa ma-Dr wanatakiwa kuwa smart zaidi kwa kuchambua hizo bajeti.............

  Waheshimiwa wafahamu kuwa kinchotarajiwa kutoka kwao ni confidence kuwa hiyo bajeti itafanya kazi hili swala ni technical na sio ushabiki wa chama. Mfano unasema utajenga barabara sawa its good barabara ni kitu muhimu sana ukija ktk bajeti ukutane hela ya kujenga Calvert sio sahihi hapo ndio tunatarajia wabunge wachambue na kufanya kazi zao vizuri.

  Kwa kweli niwe muwazi kuwa watz wengi wanafuatilia Bunge kuona drama na si kunufaika na midajala ...... at times ni kama mipasho watu wengi hawako objective....... badala ya kujadili hotuba unasikia ilani ya chama imezingatiwa ......so what . Nawaomba wabunge wawe makini pamoja na kuwa wamezoea business as usual... Oooh mara CDM hawawezi kutawala mpaka miaka 47 ijayo (Bulaya)..... total nonsense.

  Namaliza kwa kuwaasa wabunge kupeleka matani ya vyama nje ya bunge (mfano Chako ni chako) na si wakati wa kujadili hoja muhimu kama bajeti ya serikali.
   
Loading...