Wito kwa vyombo ya habari - kwa kuzingatia maslahi ya umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito kwa vyombo ya habari - kwa kuzingatia maslahi ya umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyoofu, Jun 21, 2011.

 1. M

  Mnyoofu Senior Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  TAFADHALI VYOMBO VYOTE VYA HABARI!

  Kwa kuzingatia uzalendo na maslahi ya umma, kwa kumwogopa Mungu na kutumia vipawa na previleges zenu kama wanahabari, tunaomba muitawanye, muandike kwa mapana na kuhakikisha kuwa kila mtanzania, wakuangalia TV, Radio, magazeti, blogs nk, wanapata hotuba ya Mh Mbowe aliyoitoa leo kuhusu matumizi mabaya ya pesa za umma, kwa kupitia mwanya wa Posho, Magari ya kifahari, gharama za safari nk.

  Publicity kubwa itawafanya Watawala watapata kimuhe-muhe cha aibu, toka ndani wakati dhamira zao zinawasuta, maana ukweli ni ukweli tu hata kama utaupaka matope au kuukanusha. Wananchi pia wakipata habari watapata fursa ya kuwahoji wabunge wao kwa mapana zaidi, hasa ili watoe misimamo yao, wao wako upande upi.

  Tunataka Serikali ikate matumizi, posho ni kiashiria tu, tunasema tumechoka kutumika na kunyonywa na watu tuliowakasimu madaraka. Watawala wasitegemee utoaji wa kodi kwa hiari kwa kuzingatia uzalendo, kama pesa tunayoisotea sana inaishia mifukoni mwa walio wachache wasio hata na soni ya matatizo yanayouwakumba watanzania.

  Kama alivyozoea kusema Mtikila miaka ya 90, saa ya ukombozi ni sasa! This is your corporate social responsibility, tutawakumbuka kwenye historia ya kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye ukoloni wa ndani, tulionao sasa!

  Tunaomba yeyote aliye na hotuma kamili ya Mh Mbowe ya leo aibandike hapa. Nasikia maumivu ya moyo, and I remain helpless, pleas emedia people help the helpless in the villages, we need for once your moral support!
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Anza na Tanzania Daima ambayo ndiyo inaongoza kwa kuwalinda hao wanaokwapua fedha za umma. Utadhani gazeti lenyewe halimilikiwi na huyo Mbowe, au kajitoa umiliki?
   
Loading...