Wito kwa Viongozi Wetu: Tutende Mema na Haki kwa wote. Nimeanza kumkumbuka Kikwete! Atakuja kuonekana kama Malaika!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,543
Wanabodi,

Siku za weekend tuwe tunaleta mada za furaha furaha with a light touch ya kumbukumbu njema.

Leo katika pita pita yangu humu JF, nimekutana na comment moja ya mmoja wa ma GT wetu humu JF wa ukweli, akimzungumzia Kikwete enzi zile.
Kikwete is the worst president in the history of our country.

Mkuu Nguruvi3, comment yako hii, imenitafakarisha na kumkumbuka Kikwete!.

Kwa vile historia yetu bado inaandikwa, jee by now, msimamo wako huu kumhusu JK bado ndio huu huu or by now utakuwa umebadilika?.

Siku Kikwete anaaga. kuna mahali alisema mtanikumbuka, sisi wengine ambao tulimbeza sana, pia tukabeza hiyo mtanikumbuka kwa kujiuliza tutakukumbuka kwa lipi?!.

Lakini as times goes by, kiukweli kabisa, nimeanza kumkumbuka Kikwete!.

Japo tulimbeza sana JK, mimi nikiwemo, tukamtukana, tukamkashifu, tukamkejeli na kumdhihaki sana tuu hadi kumuita dhaifu, lakini kwa hali inavyoendelea sasa, utakuja kufika wakati JK ataonekana na kama malaika fulani!. Kiukweli Tutamkumbuka!.

Tena Kikwete angekuwa Mkristu Mkatoliki, kama Mwalimu Nyerere, kanisa lingeanza hatua ya kwanza ya ku document mema yake ili kuusubiri wakati muafaka wa kumfanyia canonization process kumtangaza kuwa Mtakatifu. Process hii kwa Mwalimu Nyerere imeisha anza na hatua ya kwanza ni kutangazwa "Mwenye Heri".

Ukiachilia mafao yao na stahiki zao kama viongozi wastaafu, hivi hakuna kitu kinaweza kufanyika kuwaenzi viongozi hawa wakiwa wangali hai, na kushuhudia jinsi wanavyokuwa appreciated?.

Hakuna namna ya kumuenzi Mzee Mwinyi kwa "Rukhsa" yake, Mkapa kwa "Mr. Clean" na JK kwa kuwa "Mtu wa Watu"?.

Hii itakuwa kama encouragement kwa viongozi wa sasa kutenda mema in view ya kuja kupata appreciation muda wa uongozi wao, ukipita, wajiulize wanaacha amali gani, watakumbukwa kwa lipi?, jee watakumbukwa kwa wema au kwa ubaya?. Watu wakiwakumbuka, jee watakuwa na furaha machoni na moyoni, au watakuwa na furaha machoni tuu lakini mioyoni huzuni?.

Wito kwa viongozi wetu, Tanzania ni nchi yetu sote, ni nchi ya watu wote, rangi zote, dini zote, jinsia zote na vyama vyote!, watendeeni haki watu wote wa vyama vyote, na sio kwa chama kimoja, kwa vile ndio chama tawala, kujiona kama ndio chenye haki zaidi na kustahili kutawala milele!, wasijisahau na kujiona utawala wa nchi hii ni haki ya chama fulani tuu hadi kutoa kauli za kibri, jeuri, kibabe, kujisikia na kujiona ndio zaidi hadi kujifananisha na Mungu kwa kutoa definitive statements kama "kutawala milele!".

Uongozi sio stahiki, ni dhamana tuu, leo upo, kesho haupo, na ukiwepo, ujijiue upo kwa ajili ya wote, kumbukeni kuna leo na kesho, after all kuna kitu kikubwa zaidi kinaitwa "Karma!" hakina mswalie Mtume kwa wasiotenda haki!. Karma is real!.

Hebu waangalieni Mwinyi, Mkapa na Kikwete wanavyoishi kwa furaha halafu compare na wastaafu wa Zanzibar!. Tusifanye masikhara na Karma.

Tutende mema jameni!.

Jumamosi Njema!.

P.
Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour" - JamiiForums
 
Magu anaendeleza ya kina JK na BM ila kwa style tofauti na ya bila kuona aibu ila wote ni wale wale isipokuwa tu kwa viwango tofauti.

Watanglulizi wake walilea misingi mibovu walioikuta kama katiba ya mwaka 77,n.k na pia wakaweka ya kwao mibovu ambayo leo hii Magu ndio anaitumia kufanya anayoyafanya na hii ndio sababu wanashindwa hata kukemea hadharani .

Ya kung'oa watu kucha na meno hayana tofauti sana na haya ya watu wasiojulikana.

Sheria za mitandao ni kazi ya JK ambazo leo hii zinatesa watu.

Hata hii sheria ya uchaguzi inayowatambua wakurugenzi wa Halmashauri na watendaji wa kata kama maafisa wa Tume ya Uchaguzi nakumbuka wapinzani waliipinga sana na kutaka waondolewe wakati sheria ya uchaguzi inafanyiwa marekebisho Bungeni(kwa kumbukumbu zangu) ila Bunge la Makinda likagoma na likapitisha sheria kama ilivyo na JK akaisaini kuwa sheria.

Sema tu walau wao walikuwa na ile kuona haya na kaubinadamu kidogo.
 
Nukuu

Wito kwa viongozi wetu, Tanzania ni nchi yetu sote, ni nch ya watu wote, rangi zote, dini zote, jinsia zote na vyama vyote!, watendeeni haki watu wote wa vyama vyote, na sio kwa chama kimoja, kwa vile ndio chama tawala, kujiona kama ndio chenye haki zaidi na kustahili kutawala milele!, wasijisahau na kujiona utawala wa nchi hii ni haki ya chama fulani tuu hadi kutoa kauli za kibri, jeuri, kibabe, kujisikia na kujiona ndio zaidi hadi kujifananisha na Mungu kwa kutoa definitive statements kama "kutawala milele!".
 
1. Sipangiwi cha kufanya (Kujiona bora kuliko wengine)
2. Siwezi kukujengea barabara halafu mkanitukana (kupenda kutukuzwa, Sifa, kuabudiwa)
3. Wewe hilo bango lako hata ulinyooshe silisomi. Watu mnajitafutia matatizo (kutoheshimu mawazo ya wengine)
4. Machinga wa Mwanza wasisumbuliwe maana ndo walipatia kura. Hata nyumba zilizoko barabarani Mza zisibomolewe. (ubaguzi, ukanda na ukabila)
5. Kimara bomoa Hata ikiwezekana bomoeni nyumba zote mpaka kibamba (visasi, kinyongo, chuki)
 
Jk he is living legend; siku zote kiongozi mzuri ni yule anayejua mambo mengi! Sitorudi tena Tanzania ntakaa ugenini mpaka tupate kiongozi sahihi, nawaonea huruma sana ndugu zangu! Nchi siasa za kishamba zinashika kasi Badala ya uchumi; kila siku uchaguzi; shwaini
 
1. Sipangiwi cha kufanya
2. Siwezi kukujengea barabara halafu mkanitukana
3. Wewe hilo bango lako hata ulinyooshe silisomi. Watu mnajitafutia matatizo
4. Machinga wa Mwanza wasisumbuliwe maana ndo walipatia kura. Hata nyumba zilizoko barabarani Mza zisibomolewe.
5. Kimara bomoa Hata ikiwezekana bomoeni nyumba zote mpaka kibamba.
Ila hapa kama kuna kitu alikuwa ametumia
 
Back
Top Bottom