Wito kwa serikali ya mh.jakaya m.kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito kwa serikali ya mh.jakaya m.kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mallaba, Mar 7, 2011.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Tumeona na kusikia kuwa kumekuwa na maandamano makubwa na yenye kutia simanzi kila mara unapoongalia zile picha kwa jinsi mwananchi anavyoonekana akiwa amechoka na kukata tamaa.Baada ya hapo tumeshuhudia maneno ya vitisho,kejeli na kutishiwa kuFungiwa kwa CDM kwa sababu zisizokuwa na msingi.

  Kweli hawa watu hawajajua kabisa maana ya upinzani na multi-party system kwa ujumla.
  Angalia USA pamoja na mambo mengi anayojitahidi kufanya Obama lakini hutakosa kusikia maneno ya kejeli,chuki binafsi,vijembe n.k kutoka kwa wapinzani wake Republican.
  Hilo ni swala la kawaida kabisa katika mfumo wa vyama vingi.

  CCM walipaswa baada ya kuona na kusikiliza hizo hoja zinazotolewa na CDM wazijibu kwa vitendo kama ifuatavyo:
  1.kupunguza mfumuko wa bidhaa,kwa kupunguza kodi ya bidhaa muhimu au kwa kuweka fedha maalumu katika sekata hizo( incentives) ili kupunguza mfumuko wa bei.

  2.kuongeza mishahara kama China wanavyofanya kwa sasa.Huwezi kunieleza mshahara ule ule utakidhi mahitaji wakati zamani nilinunua sukari 1600 leo 2200, petrol iko juu,nauli ziko juu ..je huyo mtu ataishije??

  4.Hapo ndipo serikali inapotakiwa ichukue hatua za haraka zaidi wala sio kuanza kulaumiana na CDM au watu wengine.Wenye matatizo ni wananchi wala sio CDM kama wananyotaka kusema.

  5.Kama watasema kuwa hawana pesa basi walifanye hili, kupunguza mishahara ya watu wakubwa wote kama wabunge,mawaziri etc Hawa wapunguziwe kabisa hiyo mishahara yao au wawekewe tax kubwa zaidi ili hizo pesa ziende moja kwa moja ku-subsidize wale wenye low income ,hili linafanywa na nchi za wenzetu na limeonekana kuwa linafaa sana.Mwaka juzi nimeshuhudi kipindi cha mtikisiko wa Uchumi Serikali ya Hong-Kong ilipitisha sheria ya kupunguzwa mishahara kwa wote wanakuwa over-paid ili ku-compensate na wale wasio kuwa na kipato kabisa.

  Cha kushangaza sisi katika serikali yetu pamoja na hali kuwa ngumu kwa uchumi bado wameendela kuwa na matumizi yale yale ya mwaka 1947 kitu ambacho hakiendani na uhalisia wa hali ya sasa.Tumeona USA katika bajeti yao wamepunguza na kutoa mambo mengi sana ambayo yanaonekana kuwa hayana kipaumbele na hao wenzetu wana pesa sembuse na sisi tulio ombaomba katika kila kitu?

  Pamoja na miradi mingi kuwa inachangiwa na nchi za wahisani serikali yetu matumizi yake ni mengi sana na mzigo mkubwa kwa walipa kodi.Hili ni lazima libadirike,lasivyo siku zijavyo sitashangaa kusikia kuwa miradi yote iko juu ya mawe,sababu serikali inachangia kiasi kidogo sana katika miradi ya maendeleo wakati pesa nyingi zikitumika katika uendeshaji wa serikali ,na nchi wahisani pia wako katika hali ngumu sana kiuchumi hivyo itafika wakati nao watasema hatuwezi kuendelea kusaidia ninyi wakati wananchi wetu nao wanahitaji msaada.

  6.Ukweli ni kwamba kuna income gap kubwa kati ya rich and the poor na hapo social instability haiepukiki lasivyo wawasaidie hao walio na kipato cha chini.Kuna watu wanaoishi maisha ya kifalume na wakati wengine hata ule mlo mmoja kwa siku ni anasa.

  This can be done without even affecting other social development projects.

  Ni wito wangu,je wito wako ni upi?
   
 2. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Ni wito wangu,je wito wako ni upi?
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  the major focus of the government's work this year should include reining in inflation by keeping the consumer price index, a major gauge of rising costs, to an increase of about 4 percent.
   
 4. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Government should also be concerned on priorities that include improving people's well-being, advancing education and healthcare, conserving natural resources and protecting the environment.
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  These include the creation of more jobs, reducing the tax burden on low- and middle-income people and increasing government subsidies for the rural cooperative medical care system.
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tatizo letu mkuu siyo sera mbovu, bali ni utekelezaji wa sera zetu nzuri
   
 7. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  sasa kama sera zipo na hazitekelezwi kuna haja gani ya kusema kuwa tuna sera kaka??
  Sikatai mipango ipo na huwa inakuwa mingi sana ikichanganywa na michakato yao lakini tatizo siku zote matokeo yake huwa ni kama sufuri.
  so what should we call this, bad implementation or poor supervision??
   
Loading...