Wito Kwa Serikali na DPP: Kesi Ya Ugaidi Dhidi Ya Freeman Mbowe Na Wenzake Irushwe LIVE Kupitia Channel Maalum Ya Online TV

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,581
Habari wana Jamii,

Nimekaa na kutafakari kuhusu kesi ya Ugaidi Ya Freeman Mbowe na Wenzake ambayo inakaribia kuanza mwezi ujao. Na ndio nikaamua kuanzisha hii thread maalum ya kuomba kesi hio irushwe "LIVE COVARAGE" kwa kutumia Channel Maalum (Za Bure) kama ilivyofanyika;

I) South Africa - Katika kesi ya Oscar Pistorious (Mkimbiaji Kilema - Mwana Paralympic).

II) Kenya - Katika kesi ya kupinga Uchaguzi Mkuu uliopita.

Kwasababu kuu,

1) Ni Kesi yenye umuhimu na mvuto (attention) mkubwa kitaifa na kimataifa.

2) Kuepusha msongamano wa raia kwenda kuisikiliza Mahakamani kwasababu ya maambukizi ya Covid 19.

3) Raia wa Tanzania walio ndani na nje ya nchi wana haki ya kujua, kuona, kusikiliza mashtaka yalio dhidi ya kiongozi wao wa Chama Kikuu Cha Upinzani.

4) Vyombo visivyo vya Serikali (NGO's, Donners e.t.c) vina mvuto wa kujua na kufuatilia dhidi ya kuendeshwa kwa kesi hio kubwa.

5) Ni haki ya kisheria na katiba kwa kila mtu kujua au kufuatilia kesi mahakamani ambayo ana mahusiani nayo, au yenye maslahi nae.

6) Kuna raia wanaishi mbali na Dar Es Salaam na hawana uwezo wa kwenda kushuhudia kesi ya kiongozi wao.

7) Mahakama Ya Kisutu ni ndogo kuweza kutosheleza watu wote watakao kwenda kushuhudia kesi hio.

8) Usalama kwa washtakiwa. Live coverage itapunguza msongamano wa watu nje ya mahakama kwaajili ya usalama wa washtakiwa. Sio kesho tusikie watu wasiojulikana wamemimina risasi kwenye gari ya washtakiwa na kuwaua au kuwajeruhi. Week hii gari ya kina Freeman Mbowe iliharibika mahakamani, hivi kweli unasafirisha makomandoo na mwenyekiti wa upinzani ambao wana kesi kubwa na yenye public interest kidunia kwenye gari bovu??? Usalama wao huoni unakua mashakani??? Watu wasiojulikana (Kama Serikali inavo waita) wakivamia na silaha za moto na kuwamiminia risasi???

9) Dunia na Taifa kwa ujumla lijiridhishe kwamba watuhumiwa watatendewa haki.

Kwa unyenyekevu mkubwa ningependa kutoa vito (Tuweke Itikadi Za Vyama Pembeni) kwa;

A) Wana Familia Wenzangu Wa JamiiForums Na Wana Mitandao Ya Kijamii - Kupaza Sauti.

B) Wanasheria na Mawakili Wote - Kupeleka Maombi Mahakamani Ya Kutoa Kibali Cha Kuoneshwa LIVE COVERAGE.

C) Wanasiasa - Kupaza Sauti Serikali/DPP Ikubali Maombi Ya Kuoneshwa LIVE COVERAGE.

D) Wana Habari - Kupeleka Maombi Mahakamani na Kupaza Sauti ya Kuoneshwa LIVE COVERAGE.

E) NGO's (Human Rights Watch) - Kupeleka Maombi Mahakamani na Kupaza Sauti Ya Kuoneshwa LIVE COVERAGE.

#KesiYaUgaidiLIVE.

Zitto
Pascal Mayalla

Mfano wa Kesi Ya Uchaguzi Kenya.
Screenshot_20210803-175846_Opera%20Mini.jpg

Mfano Wa Kesi Ya Oscar Pistorious Nchini South Africa.

Screenshot_20210803-175925_Opera%20Mini.jpg
 
Hii kesi ni ya kutengeneza serikali hawawezi kujiaibisha kujiweka uchi namna hiyo, ila ingekuwa mbowe mastaka yake ni yakweli na maccm wanavyo mchukia hii kesi ingekuwa live kila sehemu
Ndio maana nikatoa wito; Tupaze sauti na wenye uwezo wa kwenda mahakamani kuomba kibali cha kuonesha LIVE COVERAGE, waende.

Ili sisi raia na dunia kwa ujumla tuweze kuona LIVE COVERAGE kuanzia Day 1 mpaka Mwisho. Tujiridhishe kwamba haki imetendeka.
 
Maisha hayapo fea kuna watu kesi zao zina miaka ushahid haujakamilika na wengine hawajui hata mahakaman watapelekwa lini na hakuna wa kuwatetea ingawaje inafahamika fika hawana hatia na wanasheria wanataka pesa nying lkn huyu bwanyenye kila mmoja anampigania
 
Umewaza vizuri Ila,
Kwa Nini Mbowe,wale viongozi waliokuwa na kesi Kama yake walikuwa hawalihusu taifa!?
Haya Ni masinema Kama yalivyo ma+cinemaRee mengine.kma Ni unabii acha utimie
 
Habari wana Jamii,

Nimekaa na kutafakari kuhusu kesi ya Ugaidi Ya Freeman Mbowe na Wenzake ambayo inakaribia kuanza mwezi ujao. Na ndio nikaamua kuanzisha hii thread maalum ya kuomba kesi hio irushwe "LIVE COVARAGE" kwa kutumia Channel Maalum (Za Bure) kama ilivyofanyika;

I) South Africa - Katika kesi ya Oscar Pistorious (Mkimbiaji Kilema - Mwana Olympic).

II) Kenya - Katika kesi ya kupinga Uchaguzi Mkuu uliopita.

Kwasababu kuu,

1) Ni Kesi yenye umuhimu na mvuto (attention) mkubwa kitaifa na kimataifa.

2) Kuepusha msongamano wa raia kwenda kuisikiliza Mahakamani kwasababu ya maambukizi ya Covid 19.

3) Raia wa Tanzania walio ndani na nje ya nchi wana haki ya kujua, kuona, kusikiliza mashtaka yalio dhidi ya kiongozi wao wa Chama Kikuu Cha Upinzani.

4) Vyombo visivyo vya Serikali (NGO's, Donners e.t.c) vina mvuto wa kujua na kufuatilia dhidi ya kuendeshwa kwa kesi hio kubwa.

5) Ni haki ya kisheria na katiba kwa kila mtu kujua au kufuatilia kesi mahakamani ambayo ana mahusiani nayo, au yenye maslahi nae.

6) Kuna raia wanaishi mbali na Dar Es Salaam na hawana uwezo wa kwenda kushuhudia kesi ya kiongozi wao.

7) Mahakama Ya Kisutu ni ndogo kuweza kutosheleza watu wote watakao kwenda kushuhudia kesi hio.

8) Dunia na Taifa kwa ujumla lijiridhishe kwamba watuhumiwa watatendewa haki.

Kwa unyenyekevu mkubwa ningependa kutoa vito (Tuweke Itikadi Za Vyama Pembeni) kwa;

A) Wana Familia Wenzangu Wa JamiiForums Na Wana Mitandao Ya Kijamii - Kupaza Sauti.

B) Wanasheria na Mawakili Wote - Kupeleka Maombi Mahakamani Ya Kutoa Kibali Cha Kuoneshwa LIVE COVERAGE.

C) Wanasiasa - Kupaza Sauti Serikali/DPP Ikubali Maombi Ya Kuoneshwa LIVE COVERAGE.

D) Wana Habari - Kupeleka Maombi Mahakamani na Kupaza Sauti ya Kuoneshwa LIVE COVERAGE.

E) NGO's (Human Rights Watch) - Kupeleka Maombi Mahakamani na Kupaza Sauti Ya Kuoneshwa LIVE COVERAGE.

#KesiYaUgaidiLIVE.

Zitto
Pascal Mayalla

Mfano wa Kesi Ya Uchaguzi Kenya.
View attachment 1878832

Mfano Wa Kesi Ya Oscar Pistorious Nchini South Africa.

View attachment 1878833

Kenge akisikia kwa wito tu, huyu atakuwa wa kwanza.
 
Unataka jamuhuri iumbuke mubashara?
Aaaah kaka, wataumbuka vipi wakati wao wapo juu ya sheria na mahakama? Si umeona IGP Sirro ametumia vyombo vya habari kumtia hatiani Mbowe hata kabla ya mahakama kusikiliza kesi. Kesho hakawii kuita press tena na kumhukumu na kifungo cha gerezani, kwasababu alisahau kumtajia kifungo kwenye press iliopita.

Mi nacho taka, wananchi wanaotaka kwenda kusikiliza kesi wanazuiwa na kukamatwa kisa wanaambiwa wanaandamana. Basi irushwe live coverage kila mtu aangalie na mkewe nyumbani kwa amani.
 
Amesikika Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Magdalena Ntandu akielekeza utaratibu mpya kuhusiana na kufuatilia kesi inayomkabili Mbowe.

Kasema eneo la mahakama ni dogo kuwatosha wote ambao wangependa kuhudhuria. Suluhu ya hapa ilikuwa kutafuta namna wezeshi kwa wote ambao wangependa kuhudhuria na kufuatilia kesi hii.

Umuhimu wa kuonekana haki ikitendeka katika shauri lolote hakuwezi kudunishwa.

Kama mkoloni aliyaacha majengo ya mahakama wazi bila madirisha milango ya kufungwa, kwanini serikali ya rais mwanamke mtarajiwa wa 2025 leo ifungie wasikilizaji wa kesi ya mtuhumiwa wake nje na kwa matumizi ya nguvu?

Katazo la mtu kuwa na simu au hata kuwasiliana kwa maandishi au memo mahakamani ni kinyume sheria. Kwanini serikali ijipe jukumu la kuvunja sheria ndani au katika viunga vya mahakama kwa namna yoyote?

Kuna mawazo kuwa kuna mhimili mmoja unaendelea kuiingilia mingine na kushurutisha yake. Jambo hili si la afya hata kidogo. Mambo kama haya ndiyo yanayoleta udharura kwenye madai ya katiba mpya.

Ili kuonyesha haki inatendeka pia katika kesi hii, dhana ya mahakama kuwa ni sehemu ya wazi na iheshimiwe.

Kuliacha shauri hii kuendeshwa kwa uwazi likiwemo kurushwa kwenye Runinga ikibidi, kungejibu changamoto ya nafasi na pia kupunguza mkusanyiko usiokuwa wa lazima mahakamani hapo.

Ikumbukwe kuwa serikali ya haki ni mwakilishi wa wananchi wake. Ni jambo la aibu sana kama serikali ina nia yoyote ovu dhidi ya raia wake awaye yote.

Ni muhimu sana jitihada zote zikafanyika kuonyesha kwa vitendo kuwa haki inatendeka.

Itambulike kuwa hatutakaa kimya kwa uonevu dhidi yetu kama raia.
 
Back
Top Bottom