Wito kwa Salim Ahmed Salim - Mpinge Kikwete 2010

Hakuna kitu mule kwanza tujiulize amefanya nini kwa africa alipokua mkuu huko african union and amefanya nini kwa tanzania kwa nafasi alizoshika.hakuna kitu.
Jibu ni kuondoa kabisa ccm.kama mkono wa kushoto unaiba wakulia hauweku kuwatofauti jibu ni kukata
 
Kwa siasa na namna ya kuwapa viongozi ilivyo, huyu bwana itakuwa ngumu sana kwake. Muda mrefu aliotumia kikazi nje ilimfanya awe stranger among his colleagues. Sijui itakuwaje ila angelikuwa ni kiongozi shupavu tu kwa mtazamo wangu kulikoni hizi sound tunazoziona zisizo na future yeyoto

I think you are mistaken. Stranger among colleagues wepi maana wanaohitaji uongozi wa Rais sio colleagues bali wananchi wote kwa ujumla. Salim has never been a stranger in Tanzania pamoja na kukaa nje miaka yote hiyo. Chukua mfano hai tu. Katika mchakato wa kutafuta mgombea mwaka 2005 Salim alikubalika sana hata kwenye remote areas za Tanzania na kupata supporters wengi waliomuunga mkono. Mfano ni Songea, Tabora, Kilimanjaro etc. Hata Dar es Salaam alikubalika na watu walikuwa wakitaka apatikane kiongozi mature na shupavu wa aina ya akina Salim. Siri ya mafanikio aliyoyapata hadi akawa namba mbili katika kinyang'anyiro kile ni kwamba alipokuwa Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi kwa kipindi kile kifupi alifanya mengi kwa manufaa ya wananchi, wanajeshi n.k. Pia ni Salimu ni kiongozi ambaye ana hulka ya kupenda kusaidia watu. Siri ya mafanikio ya kiongozi yoyote ni kuwa karibu zaidi na wananchi anaowaongoza na kuwajali kwa dhati na si kinafiki. Ndivyo alivyofanikiwa Mwalimu na viongozi wengine wa aina hiyo.

Nakubaliana na waliosema kwamba Salim hana mpango wa kugombea na siamini kwamba atakuwa na haja tena ya kuwa Rais. Ule uhuni uliofanyika katika ule mchakato wa kumtafuta mgombea wakati ule umetosha kuonyesha hali halisi ya mambo yalivyo kombo nchini mwetu. Unless yanakuwepo mabadiliko ya wazi ya kuwadhibiti wanaonunua uongozi, nchi hii haitaweza kamwe kuongozwa na mtu makini na mahiri kwa manufaa ya wananchi wa kawaida.
 
Mitanzania Ndivyo tulivyo

Huyu jamaa almanusra achukue ukatibu wa UN, leo kuna mitanzania inasema hafai, hakubaliki

waulize katika nyakati zile ngumu za kiuchumi Tz

Salim alikuja na ''ASANTE SALIM'' mitumba

They guy can make changes, nchi yetu hii afadhaki tuajiri rais toka nje ya nchi sio hawa wanaojuana juana
 
Boramaisha said:

Boramaisha,

..wana CCM wamefundishwa kulinda maslahi ya chama badala ya maslahi ya taifa.

..JK nchi imemshinda kuongoza. inasikitisha kuona mtu tuliyekuwa na matumaini naye kama Salim Salim, kuvunja kimya chake na kumtafutia JK kila aina ya excuses.

..Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Raisi wa Tanzania ana madaraka makubwa sana na akiamua anaweza hata kuwa Dictator. sasa pamoja na ukweli huo Salim Salim anaibuka na kudai ati mfumo umeoza na Raisi wetu pamoja na madaraka makubwa aliyonayo hawezi kurekebisha mfumo huo.

..binafsi nabaki kujiuliza Salim Salim alikuwa anagombea Uraisi ili alifanyie nini taifa lake? alikuwa anataka kuleta mabadiliko ya kweli ikiwa ni pamoja na kuupiga vita rushwa? au alikuwa alikuwa anagombea kwasababu alishakuwa Waziri Mkuu, Waziri wa Ulinzi, Waziri wa Mambo ya Nje, na Katibu Mkuu OAU?

NB:

..nilikuwa na matumaini na Salim Salim lakini kauli zake za hivi karibuni zimenichefua kwelikweli.
 
Mambo mengine ni intuitive tu ndugu yangu.Naomba nikuulize swali umeshaona mababu wangapi kati ya 100 unaowajuwa ,walio zidi miaka 70 kuwa wakali kwa wajuguu wake kwa kuwachapa bakora na adha za namna hiyo.?
Na u conside mababu wale tu waliokuwa wakorofi wakati wa ujana wao. Na ukimaliza uje na majibu kwanini saizi hao mababu wako hivyo tofauti na ujanani mwao.?Ukileta majibu hapo nipo tutajadiri vizuri.
..kati ya wazee 10 wenye umri above 70, wanane kati yao sio tu wanawachapa bakora wajukuu wao, lakin hata watoto wao!!
Na hapa ninamaanisha bakora ya fimbo au maneno!vile nimejibu swali lako, nipe jibu la swali la kwanza halafu na swali jingine hili, je unawajua vijana wangapi wenye umri kati ya miaka 30 na 50 hawawezi hata kukaripia na kumkanya mtoto anapokosea zaidi ya kufanya mizaha na kucheka cheka achilia mbali kumchapa mtoto?
 
Hapo mkuu umekosa vibaya sana,wewe peleka mzee mtoto wako akalelewe na babu wa miaka 80 uone matokeo,akitoka humo salama ujue huyo mtoto ana hekima za asili .
 
Mitanzania Ndivyo tulivyo

Huyu jamaa almanusra achukue ukatibu wa UN, leo kuna mitanzania inasema hafai, hakubaliki

waulize katika nyakati zile ngumu za kiuchumi Tz

Salim alikuja na ''ASANTE SALIM'' mitumba

They guy can make changes, nchi yetu hii afadhaki tuajiri rais toka nje ya nchi sio hawa wanaojuana juana

Mkuu wangu taratibu.
mie nafikiri alikuwa anafaa kwa wakati muafaka ,sasa wakati mzee wetu umempita nafikiri kabisa mikiki mikiki ya kibinadamu na mitazamo ya kiafrika mzee hafai tena kuongonza nchi masikini na yenye watu wajeuri na wenye roho za paka kama TZ.

Nafikiri ni tabia ya kibinadamu na mitazamo ya kiafrika mzee miaka yake ya kuishi ni michache sana ikizidi ishirini basi bahati japo namuombea aishi miaka zaidi ya mia,kutokana na hilo swala na mitazamo ya kiafrika nafikiri akipata urais hatatilia maanani sana maana atakuwa anahisi anajisumbua bure wakati mda wake wa kuishi unahesabika ,hii ni mentality yetu ya kiafrika na haiepukiki.

Hivyo mimi naomba mzee apumzike ,tutafuta mwingine mwenye nguvu na nia ya kweli.
 
Wakuu zangu Umri sio hoja kabisa.... Reagan alipata Urais akiwa na umri gani?..Na kafanya mangapi mazuri wakati Us ilikuwa hohehahe kiuchumi..iweje leo iwe sababu wakati tumeona vijana hao kina JK waloyafanya. Huwezi kupima uwezo wa mtu kuongoza kutokana na Umri bali vision ya mtu huyo..Salim has a vision ambayo inakubalika sana kwa wenye kujua maana..

By the way China wamesherehekea miaka 60 ya Ukomunist kwa kujipongeza na sio kulaaani, mnajuan kwa nini!.. The big word - CHANGE ni kubadilisha ways to run resources in hand ili kuleta maendeleo na sii kubadilisha what you have to become something else!
Hii ndio tofauti yao nasi kwa sababu wao wameweza kuboresha mazingira na maisha ya wananchi wao badala ya kujaribu kubadilisha mazingira na maisha ya wananchi...
 
Last edited:
SAS anafaa sana. Pamoja na kusema siasa yeye basi kitendo chake cha kukaa kimya wakati nchi inaenda mrama mimi kinanisikitisha sana.

Kwanini mtu mwenye hadhi kubwa kama SAS katika jumuiya ya Kimataifa anakaa kimyaaa huku nchi ikendelea kwenda mrama!? Huu ni uzalendo kweli!? Unaiona nchi yako inasambaratika na wewe kutotia neno kuhusu hali mbaya ndani ya nchi yako kwa maoni yangu sijambo jema kwa kweli. Kuna haja ya SAS kuanza kuongea sasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa 2010 hata kama hayuko tayari kugombea tena.
watanzania tunatatizo la kutofanya tadhimini,naomba kujulishwa mchango wa Salim kwa watanzania pamoja na kushika nyadhifa zote hizo kubwa ?
Nini Salim amekifanya kwa watanzania. Naomba mtu ambaye anaweza kunielimisha maana vigezo vya kiongozi wa umma ninaamini ni huruma kwa watu anao waongoza,hivi leo hii kiongozi yupi amesimama na kupinga ufisadi unaoendelea sija msikia Salim wala wazee wanaoheshimika sana kama kina Kawawa wakisema kitu.Hii nipicha fupi inayoonyesha ni jinsi gani
hatuna na wala tusitegemee viongozi katika safu ya vikongwe hawa"tusibadilishe mvinyokwenye chupa ya zamani"
 
Wakuu zangu Umri sio hoja kabisa.... Reagan alipata Urais akiwa na umri gani?..Na kafanya mangapi mazuri wakati Us ilikuwa hohehahe kiuchumi..iweje leo iwe sababu wakati tumeona vijana hao kina JK waloyafanya. Huwezi kupima uwezo wa mtu kuongoza kutokana na Umri bali vision ya mtu huyo..Salim has a vision ambayo inakubalika sana kwa wenye kujua maana..

By the way China wamesherehekea miaka 60 ya Ukomunist kwa kujipongeza na sio kulaaani, mnajuan kwa nini!.. The big word - CHANGE ni kubadilisha ways to run resources in hand ili kuleta maendeleo na sii kubadilisha what you have to become something else!
Hii ndio tofauti yao nasi kwa sababu wao wameweza kuboresha mazingira na maisha ya wananchi wao badala ya kujaribu kubadilisha mazingira na maisha ya wananchi...

Mkuu Kikwete sio kijana naye ni babu miaka 60 wapi na wapi na ujana? ila ni babu kijana
 
watanzania tunatatizo la kutofanya tadhimini,naomba kujulishwa mchango wa Salim kwa watanzania pamoja na kushika nyadhifa zote hizo kubwa ?
Nini Salim amekifanya kwa watanzania. Naomba mtu ambaye anaweza kunielimisha maana vigezo vya kiongozi wa umma ninaamini ni huruma kwa watu anao waongoza,hivi leo hii kiongozi yupi amesimama na kupinga ufisadi unaoendelea sija msikia Salim wala wazee wanaoheshimika sana kama kina Kawawa wakisema kitu.Hii nipicha fupi inayoonyesha ni jinsi gani
hatuna na wala tusitegemee viongozi katika safu ya vikongwe hawa"tusibadilishe mvinyokwenye chupa ya zamani"

Nimekupata mzee ndo hivyo vijibabu vyote tuvitupe nje bado vyote vinafikiria ya kikumonisti.

Hii ikienda sambamba na kupoteza kabisa na msemo unaosema zidumu fikra za Mwalimu.
 
Hapo mkuu umekosa vibaya sana,wewe peleka mzee mtoto wako akalelewe na babu wa miaka 80 uone matokeo,akitoka humo salama ujue huyo mtoto ana hekima za asili .

Kwa nini upeleke mtoto wako akalelewe na babu?
 
Mkuu wangu mengine ni historia yani hadithi hadithi --- hadithi njoo na utamu kolea.

Watu wengine wanasinginzia tu mara wamekoribwa mara wame wachifupa lakini wengine wana UKIMWI ,wamebadirisha damu mara kadhaa wakiwekwa kati kwa kuhojiwa na kupewa kapresha kidogo ,haooooooo wamekwisha .

Hakuna anayeua mwingine mpaka pale ushahidi unapokuwepo wa wazi zingine nafikiri ni kuzidanganya nyakati.

Bwa ha ha ha ha ...

Ushahidi sio, enhe
 
Kabla ya uchaguzi wa USA wengi walimuwekea vikwazo obama vikiwemo kuwa Muisilamu, si Mmarekani hakuzaliwa pale mweusi NK, sasa jee hivi nyie mpo tayari salim agombani Urais ?au manjisahaulisha kuwa na yeye ni miongoni mwa wale mnaowachukia ambao sasa ndio mnawafanya kama tambara bovu?
 
Mkuu,

Unawaongelea kina nani hawa?
 
Mkuu Kikwete sio kijana naye ni babu miaka 60 wapi na wapi na ujana? ila ni babu kijana
Haaa! haaa, JK babu wapi mkuu Ridhwan hana mtoto...wewe unaweza kuwa babu na miaka yuako sijui 35 au 40, kifupi JK hayupo nyuma ya tafrisiri yoyote ya Ujana.
Mimi nitazikubali tu sababu nyingine nje ya Umri kwani mnataka kutuvua wazee madaraka pasipo sababu za msingi. At the sametime hao wazee mnaosema wakiondoka nina hakika uchafu mtakao ufanya vijana utakuwa hauna kipimo..
Binafsi naamini kabisa kwamba magonjwa kama HIV ni mfululizo wa matunda ya Vijana, ni hao vijana siku hizi mnatembea na mbwa, Punda, Chatu mkiona ati ni art fulani mnachukua hadi video! jamani.....Kisha magonjwa ya ajabu ajabu yanapokuja mnaanza kutafuta mchawi.. mnasema ooh! ni magonjwa ya maabara sijui Jeshi la Amerika limefanya hivi na vile... mkashindwa kujiangalia nyie wenyewe.
Wazee kama sisi vitu hivyo hatuwezi fanya bado tunathamini utu na mila zetu kiasi kwamba ni rahisi kuanza UPYA na Mzee kiutawala, mkaweka mikakati endelevu lakini sii vijana maanake party za Ikulu zitakuwa kila siku pengine hata Disco linaweza funguliwa mkajirusha. Yale yale ya toka kina Kaizali na Pharaoh Tat..
Hivyo ukitazma swala zima kwa ushabiki kweli mtu kama Salim kesha zeeka lakini he is the ONLY one ambaye anaweza kumwangusha JK ktk uchaguzi ndani ya CCM...Kufikiria hivyo tu ni mwanzo mzuri wenye tumaini kabla ya uchaguzi mkuu.
 
Haha haha
Wazee wana idea za kikomnisti lazima watupwe nje kwanza,hili Taifa ndipo litaendelea.

Wazee kwa ngono ni noma acha kabisa ,angalia % ya vijibabu vilivyooa wajukuu wao ni kubwa mno.Wasichana wanapewa HIV ni vibabu maana wanapewa huko fedha ndefu.

Katembelee mtaa wa OHIO,UHURU pale DAR uone rate kubwa wanaochukuwa machangudoa ni wazee ama vijana, mkuu sisi vijana wengi hatuna fedha za kumlipa changudoa 100000Tshs ni vijibabu hivi vilivyo na fedha hiyo.

Kama wazee mngekuwa si mkamonisti tuachieni vijana na sisi tujaribu mikakati yetu ya kuendeleza nchi mda kama nyie vijibabu mliokaa madarakani zaidi ya miaka 50.
 
Haha haha
Wazee wana idea za kikomnisti lazima watupwe nje kwanza,hili Taifa ndipo litaendelea.

Acha ubaguzi wa umri (ageism); ukomunisti hausababishwi na uzee. Kuna mivijana kibao ni mikomunisti kuliko maelezo. Ahukumiwe kama yeye, sio kwa sababu ya umri wake.
 
Kosa kubwa mnalofanya kwenye ushauri wenu ni kumshauri agombee kupitia CCM wakati mnajua kwamba hataenda popote. Can you guys come out of box and think of a life without CCM? Yaani nyie watu hili limbwata la CCM hali-expire tu?
 
Acha ubaguzi wa umri (ageism); ukomunisti hausababishwi na uzee. Kuna mivijana kibao ni mikomunisti kuliko maelezo. Ahukumiwe kama yeye, sio kwa sababu ya umri wake.

Mbona wazee wenyewe wanatubagua vijana ?? Na hata hivyo umri wa Mzee Salim mie naamini kabisa hauwezi kuhimili misukosuko ya mabadiliko yanayotakikana ktk nchi yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom