Wito kwa Salim Ahmed Salim - Mpinge Kikwete 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito kwa Salim Ahmed Salim - Mpinge Kikwete 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwafrika, Sep 28, 2009.

 1. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mzee Salim,

  Labda kwanza nianze na utambulisho mfupi -

  Mimi ni mmoja wa vijana wa kitanzania ambao tulikutana nawe kwenye moja ya hotels kule Cairo na kufanya mazungumzo ya kina nawe kuhusu siasa za Tanzania (miaka kadhaa iliyopita).

  Pili - moja kwa moja kwenye ujumbe -

  Naomba ubadili mtizamo wako kuhusu siasa za Tanzania na ufanye kile cha maana (do the right thing) - uombe kupewa uraisi wa Tanzania kwa kupitia chama cha mapinduzi mwakani (2010).

  Ni hayo tu kwa leo.

  Asante
   
 2. O

  Omumura JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamaa anafaa sana but sijui kama atakubali kwani 2005 walimpiga makombora mazito sana ambayo yalim frustrate hata akafikia hatua ya kusema siasa za Tanzania sasa basi!!!
   
 3. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hayo makombora ya 2005 ndiyo inabidi ayasahau na kuyaweka nyuma yake na kuiangalia jamii ya kitanzania kwa ujumla ambayo inazidi na itazidi kuumia chini ya serikali ya sasa.
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Siasa za Tanzania hasa kwenye CCM zimegeuka kuwa siasa za makundi..wenye nazo ndio wanatengeneza na kuongoza makundi. SAS hana kundi na wala hafiti kwenye kundi lolote lenye nguvu ndani ya CCM. Kwa hilo hawezi kufanikiwa hata akiamua kubadili mawazo na kugombea.
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Hiyo ni kweli Yebo Yebo kuwa CCM kuna makundi na mitandao n.k - and that's and could be the point here. Kuna kundi la watu ndani ya ccm ambao wameanzwa kuchoshwa na ubinafsi wa wanamtandao.

  Wana mtandao (wa Kikwete) sio tu kuwa wana ikulu, bali pia wanataka kuamua pia nini kifanyike ndani ya bunge na kwenye shughuli za kila siku za bongo. Kumbuka kuwa wengi wao ni mawaziri au wakurugenzi kwenye sekta kuu za nchi.

  SAS anaweza kutumia upenyo huu kuanzisha mtandao wake (yes .... naye pia ajenge mtandao wake) kumpinga Kikwete. Kutokana na umafia wa kila siku unaofanywa na wanamtandao wa Kikwete, SAS ana nafasi kubwa tu ya kuwachukua wale walio nje ya seti hii.
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mimi naona mbegu ni ile ile!tujaribu kitu tofauti kidogo
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwa kweli jamaa alipagawa sana maana alipigwa makombora mpaka akapoteza utulivu wa mawazo...but he is a very good leader, well composed on issues and well articulated compared to ze mkwere wetu.
   
 8. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ndio maana siwezi kusubiria kuona debate kati ya Salim Ahmed Salim na Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu issues na mwelekeo wa Tanzania. Nina uhakika siku hiyo Tido Mhando atasingizia kuwa mitambo ya satalaiti ina matatizo ili asiirushe live.
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sahau kitu kama hicho mkuu maana huyu jamaa alipata zahama kubwa sana kipindi chote cha mwaka 2005, Siasa za Tanzania ni za hatari sana
   
 10. N

  Nanu JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  We want a new blood and revolutionary ideas. Yes, Salim is a leader of his time. We want people who can focus and think of Tanzania 100 years to come and not only their office tenure...
   
 11. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Is Kikwete an old blood??
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Kwa siasa na namna ya kuwapa viongozi ilivyo, huyu bwana itakuwa ngumu sana kwake. Muda mrefu aliotumia kikazi nje ilimfanya awe stranger among his colleagues. Sijui itakuwaje ila angelikuwa ni kiongozi shupavu tu kwa mtazamo wangu kulikoni hizi sound tunazoziona zisizo na future yeyoto
   
 13. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  I agree with your views 100%. Yes it's about time the baton should be passed to a young leader with a clear vision of morden era we are living in.
  The big question is WHO? When I look around the only person I can see with that 'potential' is Zitto but he is not experienced enough yet for such a high position.
  If we put our political affiliation aside, we have to agree that right now there is no-one qualified for that position more than SAS.
  He has such impressive CV and command respect on the world stage. I believe he's the right person for our country right now no matter what party he'll stand for.
   
 14. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kweli tujaribu radha nyingine hata kama ni ndani ya CCM.
   
 15. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Nakubaliana na Salim kwa nafasi ya urais na anaweza akafanya vizuri kwa kuwa I believe yuko nje ya circle ya mafisadi lakini kwa ukweli kwamba atatoka CCM, basi hapo kila kitu kitakuwa kimeishaharibika. Yeye kama yeye ingawaje yeye ni msafi lakini atakuwa amezungukwa na watu wachafu na hivyo usafi wake yeye utafunikwa. Kama kweli tunataka mabadiliko kwenye nchi yetu kiongozi wa juu atoke nje ya hili kundi la majambazi.

  Kijana Zito anafaa na ana vision but is still too young.Mimi nafikiri Dr. Slaa ni mtu pekee ninayemuona kwamba anaweza kuleta ukombozi Tanzania.

  Tiba
   
 16. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tido Mhando hafai kufanya shuhuli hiyo kwani kuna kundi ndani ya CCM wanamtumia kwa maskimam, kutokea akiwa Uk mpaka hapa Tz na ipo siku Machafu yake yatadhirika kwa Watanzania na Ulimwengu kwa ujumla.
   
 17. A

  Adili JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,010
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Give us a name........
   
 18. M

  MchungajiMakini Senior Member

  #18
  Sep 28, 2009
  Joined: Apr 4, 2008
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafikiria umekosea sijui ulifikiria cuf?
   
 19. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,462
  Likes Received: 1,354
  Trophy Points: 280
  umzanie ndie aweza kuwa siye, nakumbuka hata JK tulikuwa tunamkubali sana lkn sasa tunajutia uamuzi wetu, bora tupate damu nyingine labda inweza ikaleta mabadiliko
   
 20. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0  SAS akiunda mtandao wake atakuwa ameshindwa vita kabla haingia kwenye uwanja wa mapambano. Huwezi kumshinda shetani kwa wewe mwenyewe kuwa shetani.!!

  Ufisadi umeshaota mizizi kwenye jamii. Hapa tulipofika sasa tatizo sio tena Rostam Aziz, Mkapa, Chenge wala mtu mwingine yoyote Tanzania au ng’ambo. Ufisadi umeshakuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Mwandishi Ayub Rioba kwenye makala yake wiki hii aliandika “Wasiwasi tu ni kwamba kadiri miaka inavyosogea wapiga kura wa aina hii – wanaoulizia chama cha Nyerere – wanazeeka na kupungua. Lakini wapigakura wa kuuliza: "Yule katoa nini hata tumchague?" hao bado wataendelea kuongezeka” Nakubaliana na maoni yake 100%, wapiga kura walio wengi wamekubali kuwa wabia kwenye biashara ya kuuza kura. Pengine wamekubali kwa kupenda wenyewe au kwa kudanganywa na viongozi wanaowamini watawaletea maendeleo.

  Katika mazingira hayo hakuna mwanasiasa atayeshinda uchaguzi bila ya kuwa na njia mbadala. Njia hizo ni lazima zifanikiwe kuwavuta wapiga kura upande wake bila kutumia mbinu chafu za fedha au aina yoyote ya utapeli.

  SAS sio mpiganaji wa aina hiyo, na pia wakati wake wa kupigania jamii yenye maadili mema umeshapita kitambo. Hili sasa ni jukumu la vijana walioelimika na wenye nia njema na Tanzania. Vijana watakaokuwa tayari kujitoa mhanga kuijenga upya misingi ya Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo.
   
Loading...