Wito kwa Dkt. Faustine Ndugulile na Mhandisi Kilaba; Semeni ukweli kuhusu vifurushi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Hii trend ya hivi sasa ya gharama za vifurushi hatukuiona ikipigiwa kelele awamu iliyopita, lakini ninyi mlikuwa hapohapo kwenye nafasi mlizonazo Sasa.

Ukiona kelele zinakuja kwa kiasi hiki ndani ya saa 24 tambua aidha Wapo watu hasa watoa huduma wameamua kwa makusudi kutingisha kiberiti kwa kupandisha gharama au ninyi mlipotoa ahadi yakushisha vifurushi mliwadanganya wananchi au kuna maamuzi mnafanya bila kufanya utafiti na mashauriano yakutosha.

Hawa wanaolalamika ni wananchi na wanasiasa wakubwa nchini, msiwapuuzwe maana wanaweza kuwang'oa hapo mlipo.

Nayasema haya kwa kuwa natambua uwezo wenu wakutenda, haya mawimbi kaeni mwone namna yakuyakata kuondoa lawama zinazoendelea Sasa.

One more advice: Kama makampuni haya yanashindwa kuwasikiliza zungumzeni na TTCL washushe gharama za virushi kuvutia watu wengi kutumia ttcl hata kwakuwapa ruzuku itakayowasaidia kuimarisha huduma yao. Hii ni ambayo kutegemea msaada wa wahisani kwenye hii Vita nikuplan kufeli, wapeni kiburi TTCL kwenye bando mtaona hao wengine Kama wataendelea kuuza GB moja 3000.

Niwatakie Pasaka njema huku nikiwaombea msiathirike na ahadi ya Mhe. Rais ya kuapisha jumanne baada ya pasaka
 
Hapo kwakweli umepotea na kupotoka kwa hali ya juu..., Ruzuku ?, Yaani Kodi zetu ziende kuendesha hili dubwasha ambalo limekuwa liki-underperform tangu enzi na enzi ?

Kama wanaona ni rahisi na kuna uwezekano basi hizo siri za kufanya huo urahisi wawape TTCL ili bei ipungue hawa wengine waendelee kama walivyokuwa (competition baina yao ndio ilipelekea bei ahueni na sio kelele za TCRA) Siku zote Siasa zikiingizwa matokeo yake ndio huwa kama haya
 
Hakuna mtanzania mwenye akili ataitegemea hiyo ttcl yako
 
Mkuu,

Kwahiyo kupanda kwa bei ya vifurushi haiwezi kuwapunguza waerevu humu mitandaoni???

Dawa ya mjinga ni kumuondoa ujinga wake..
Hilo ni garasa wachana nalo maana halijitambui
 
Yaweza kuwa athari za wito wa kutowauwa wafanyabiashara, walikosa kupumua vyema, sasa wamepata ahueni, ili shida ilipoanzia iwezekumulikwa. Subira ya vuta heri.Tutaweza kujifunza kitu katika hili.
 
Back
Top Bottom