Wito Kwa Diaspora wenzangu na Niliyoyashuhudia Arumeru Mashariki kwa Kushiriki Kampeni za Ukombozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito Kwa Diaspora wenzangu na Niliyoyashuhudia Arumeru Mashariki kwa Kushiriki Kampeni za Ukombozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by George Maige Nhigula Jr., Apr 4, 2012.

 1. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu Wana JF,

  Namshukuru mwenyezi mungu kwa kufanikisha safari yangu kutoka ughaibuni na kuwasiri kwenye uwanja wa mapambano mkoani Arusha, jimboni Arumeru Mashariki na kubahatika kuwa karibu na viongozi wa CHADEMA wa kitaifa, mkoa, wilaya, na kata na wapambanaji wote. Lengo kuu la safari yangu ilikuwa ni kushiriki kwa hali na mali kuhakikisha natoa mchango wangu wa fedha, mbinu na ushawishi kwa wana wa meru kupiga kura ya mabadiliko na ukombozi.

  Nilifurahi sana kupata nafasi hii ya kushiriki katika harakati za kuleta ukombozi na mabadiliko ya ki uongozi katika Taifa letu, Kwa kweli nimefarijika sana na nilipata hamasa kubwa baada ya kuwasili Arumeru Mashariki na kujumuika na wapambanaji wenzangu kwa nguvu na ujasili waliokuwa nao.

  Ilinifanya nijisikie deni kubwa sana kwa nchi yangu, kwani vijana, wake kwa wa ume walionesha shauku kubwa na utayali wa kufanya mabadiliko, Nikajiona kama mimi nimechelewa kuja kujitoa na kuungana nao kwenye safari ya ukombozi, Lakini nikajiapiza nitatumia nguvu zangu zote hata kama nitarejea ughaibuni kwa mihangaiko ya kujipatia riziki na masomo basi nitakuwa daima na makamanda wote wa Ardhini kwa hali na mali, sitawatelekeza kamwe na vita hii tutashinda.

  WITO KWA DIASPORA WENZANGU:

  Nimeshuhudia kwa macho yangu na kwa kushiriki mwenyewe kuwa CHADEMA wako vizuri na hakika watatwaa DOLA 2015, Nimeshuhudia Jeshi kubwa la ardhini la makamanda wakijitoa kwa kidogo walichonacho kusaidia ushindi na ukombozi wa Taifa letu, Nimeshuhudia viongozi wa ngazi mbalimbali wakifanya kazi usiku na mchana kwa kujituma kuhakikisha ushindi, Nimeshuhudia watanzania wa kada zote wakiitakia Mema chadema kwa uwazi na kwa usiri kutokana na unyeti wa majukumu yao katika jamii.

  Hivyo basi ndugu zangu watanzania tunaoishi nje ya nchi tuwaunge mkono makamanda wetu wa ardhini ambao wako tayali kudhulika na hata kupoteza uhai wao kwa ajili ya ukombozi wa nchi hii.

  Kama huwezi pata nafasi ya kurejea nyumbani na kushiriki mapambano tunaweza kushiriki kwa kuwachangia fedha, vifaa mbalili mbali vya kiofisi kama, computer, fax mashine, photocopy mashine, scaner, magari, baiskeli, pikipiki, ili tuweze kuimarisha ofisi zote za kata na tuweze kuunganisha ofisi zetu zote za kata na makao makuu kwa mtandao wa kompyuta na kuwezesha teknolojia ya mawasiliano kuwa ya kisasa na bora wakati tunajiandaa kuchukua dola mwaka 2015.

  Diaspora wenzangu, napenda kuwapa changamoto tusibakie kupigania mabadiliko kwenye mitandao tu, tushiriki kwa vitendo kadri ya uwezo wetu na hakika mwenyezi mungu atatubalika na Tataikomboa nchi yetu.

  Jamani Ukombozi unakuja, sasa tuwe sehemu ya ukombozi na mabadiliko tunayoyataka, TUWAUNGE MKONO MAKANDA WETU!
  raisi wa watu.jpg raisi wa watu.jpg raisi wa watu.jpg kamanda-10.jpg
  makamanda-meru.jpg makamanda-meru.jpg mkutanoni.jpg police-meru.jpg dogo janja.jpg
  kamanda-11.jpg kamanda-9.jpg photo-20.jpg

   
 2. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vizuri sana, hili la kuchangia mabadiliko kwenye MTANDAO nimelipenda sana. Wengi wetu tunaishia kusema VIVA CHADEMA, lakini hakuna ambacho tunakifanya kuhakikisha kuwa tunafanya kampeni za kuwaelimisha wananchi ili waachane na ahadi za miaka hamsini iliyopita ilihali mambo yanaendelea kuwa magumu. Tufanye kwa vitendo. Kwa mfano, mimi nina maliza college mwezi wa sita. Nina mkakati wa kurudi kijijini kwetu na kuhakikisha kuwa nafungua matawi ya CHADEMA karibu kila kijiji ambacho nitaweza kufika. Siyo kwa msaada wa chama, la hasha, nitahikikisha kuwa nayafanya haya kwa muda na fedha zangu mwenyewe. Vijana wako tayari kubadilika, wanachohitajji ni kuhakikishiwa kuwa TUKIICHAGUA CHADEMA 2015, matatizo ya vijana yatabaki kuwa historia. SASA kama msmi w degree nitashindwa kuwashawishi vijana katika hili, NIMETUMIA KODI YAO BURE MIAKA YOTE HII TANGU DARASA LA KWANZA HADI CHUO KIKUU (Takriban miaka 18). Tuongee na tufanye vitendo. Mimi nawaahidi hapa JF nitakuwa naweka picha za mawawi ya chadema na wanachama wapya wa chadema kila ambapo nitafungua tawi. Mungu ibariki chadema, Mungu wabariki wote wanaopenda mabadiliko na kuichukia CCM kama ukoma.
   
 3. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu..
  Umenikosha sana binafsi kwa kuwa front line..

  Diaspora this's the way forward, shime tuunganishe nguvu!!
   
 4. a

  audacious Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 25
  umenena vema mkuu,hili swala linahitaji jitihada za kila mtanzania haijalishi anaishi wapi..tuunganishe nguvu kwa pamoja kufanya mabadiliko ya ki-uongozi ktk taifa letu,tujitoe kwa hali na mali ktk kuleta mabadiliko ambayo yatakuwa ni chanzo cha kupata tanzania mpya yenye amani ya KWELI,demokrasia na maendeleo tunayotamani kuyaona.thanks GOD watanzania sasa wameamua kilichobaki ni chadema sasa kukabiliana na changamoto ambazo ni dhahiri zisipopatiwa ufumbuzi zitaizuia kuchukua dola2015,ambazo zinafahamika kwani zimekuwa zikijadiliwa sana humu JF.TUNAYAWEZA YOTE KTK YEYE ATUTIAE NGUVU.
   
 5. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu hata sisi tunapigana na M4C na michango yetu inawakilishwa huko.
   
 6. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  pamoja sana mkuu
   
 7. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Safi sana.
  Offtopic kidoogo: Viongozi wetu chadema wawe makini na uchangiaji kupitia mobile money maana kuna wakati najaribu kutuma pesa kwa M-pesa system inanambia "Huwezi kutuma sh. 10,000/= kwenda chadema". Huenda kukawa na hujuma fulani. Naomba hili lifuatiliwe.
   
 8. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tena fanyeni haraka maana mchango wenu ni muhimu sana, hivi nyinyi huko huwa hamuoni aibu rais wenu anapohojiwa kuhusu chanzo na sababu za umasikini wa Tz harafu anajibu hata yeye hajui??? huyu ni rais wa nchi au wa kilabu ya mpira tena wa pete? au rais wa chama cha wauza mbilimbi soko kuu la tandale?

  Kutembea mji na nchi nyingi ni kufungua mawazo na mtazamo, fungukeni kama mnashindwa hata japo dogo kama hili basi we should count you in the list of enemies of the country; nasema fungukeni nchi inawahitaji sana, kukaa kimya ni kujumuika na waharamia nchini kwetu.
   
 9. Y

  Yetuwote Senior Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana, lakini nakuomba ushirikiane na uongozi wa wilaya na kata katika juhudi zako za kufungua matawi. Kama kuna mbunge au diwani shirikiana nae kwa karibu.
   
 10. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Ndugu Executive, Asante sana kwa ubunifu.

  Nawashauri CDM waanzishe Online merchants za kupokea pesa kwa credit cards.

  Hii itarahisisha Diaspora kutuma michango kwa urahisi

  Kiongozi wa CDM anaweza kunipm ili nimpe details.
   
 11. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Lakini hata hivyo chadema ijiepushe na wajanja wachache wanaojiandaa kupanga mikakati ya kiukanda kuongoza nchi hii. Nchi yetu ni yetu sote kwa hiyo ni lazima kuwe na uwiano wa kuijenga nchi yetu ktk nyanja zote vinginevyo there will be another people's power not from chadema but from the public severe anger
   
Loading...