Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Tunatahamu ya kusikia kutoka kwenye chama chetu pendwa yafuatayo:
Nadhani kimya hiki hakikisaidii Chama, na yale maneno kuwa vyama vya upinzani ni vya msimu yatapata nguvu kama mtaendelea kuwa kimya
Mtu wa PROPAGANDA wa CHAMA yuko wapi??
- Matokeo ambayo wao waliyapata kutoka kwa mawakala wao, sidhani kama sasa hii inaweza kuleta uvnjifu wa amani wowote,
- Tunaomba mtusaidie kujua nini kinaendelea, tangu uchaguzi upite hatusikia kutoka kwa shujaa wetu Dr Slaa akitushukuru kwa moyo na ushirikiano tuliomwonyesha kwa kuunga mkono agenda yao ya mabadiriko
- Tunaomba mharakishe mkakati wa maandalizi ya uchaguzi wa 2014 &2015, tuko tayari kuwaunga mkono kwa hali na mali, tunaomba muonyeshe mnajari kwa kutusaidia kutujurisha ofisi zenu kwenye kila mtaa, kata. Naamini mnaweza kuajiri vijana mkawalipa kutokana na michango yetu wakafanya kazi ya kutusaidia kutuunganisha. Mimi binafsi nataka kujua ofisi yenu ya kata ya KWEMBE/KIBAMBA ilipo, nataka chama kitusaidie wakazi wa Kibamba/Kwembe kudai haki yetu ya kupatiwa barabara na madaraja yanayopitika muda wote
Nadhani kimya hiki hakikisaidii Chama, na yale maneno kuwa vyama vya upinzani ni vya msimu yatapata nguvu kama mtaendelea kuwa kimya
Mtu wa PROPAGANDA wa CHAMA yuko wapi??