Wito kwa Chadema: Msikilizeni Wilfred Rwakatare astaafu kwa amani, atawafaa Baraza la Wazee

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,531
8,616
Nimefuatilia sakata la wabunge wa Chadema, na naona chama hicho kimefanya uamuzi wa busara, hasa kwa mamluki kama Antony Komu, David Silinde, na Joseph Selasini hawa walishatamka kwa kinywa kuwa wanahama chama kwa hiyo hakuna maswali.

Kwa busara nadhani ni vema wafikirie upya ombi la Wilfred Rwakatare la kuomba asikilizwe, ukizingatia anastaafu na mchango wake kama Mkuu wa Usalama na historia yake. Na ukizingatia pia chama hicho kimekua naye kwa shida na raha. Basi watimize ombi lake la kuomba asikilizwe kwanza; kuna makosa amefanya kama kutoa ile hotuba lakini kwakuwa anaenda kustaafu, atakuwa na muda wa kutafakari na kuwafaa kwenye baraza la wazee wa chama.

Hivyo basi, barua za kuwafukuza ni vema zikaandikwa kwa hao watatu Silinde, Komu na Selasini. Tena mtu kama Silinde ndio kabisa kaonesha upofu na kuvimbiwa kwa kiwango cha juu.

Natoa ushauri huu kama mzoefu kwenye baraza hili ambako tumeshiriki kushauri vyama vyote bila kuangalia itikadi zetu, iwe CCM au Chadema.

freeman
@jjmnyika
CHADEMA
 
Lakini yupo kwenye ile list ya Mbatia ya watakaogombea kupitia NCCR, iweje useme anastaafu?

Mbatia anapoteza muda , anayemlipa kufanya hiyo kazi hatakuwa na hiyo nguvu tena. That is a failed project ya CCM MASLAHI, NCCR Hakiwezi kushinda ubunge mahali popote bila kupewa kwenye bakuli na dola na hiyo itategemea na uwepo wa "sponsor" wao.

CCM Halisi haiwezi kubariki huo upuuzi, na kwa wananchi wa kawaida NCCR mvuto wake uliisha 1995..Makosa ya Mbatia na Komu yamekuwa hayo hayo ya kusuka Mapinduzi.
 
Lakini yupo kwenye ile list ya Mbatia ya watakaogombea kupitia NCCR, iweje useme anastaafu?
Hagombei tena. Huyu mzee safari za Muhimbili hazimkatiki watu wanamshauri kutokana na afya yake ajikinge yeye anaona masihara. Huyu ni ana tatizo kubwa sana la moyo! Siombei mabaya ila time will tell!
 
Jumbe aliisaidia sana CCM ni mmoja wa waasisi wa CCM lakini alicross red lines.

Seif Shariff Hamad ni mmoja wa vijana waliokuwa kindakindaki wa CCM lakini alipozingua walimtosa.

Ni precedence mbaya kusamehe usaliti kama wa Lwakatare, mtu aliyepaswa kuelewa magumu ambayo chama kimepitia mpaka leo hii kwenda kuunanga uongozi wa Chadema unaotetea maisha ya watu dhidi ya Covid-19 ambayo serikali ya CCM imekwepa vita dhidi yake.
 
Huku mtendea haki Mzee wa watu na kwanza umemvunjia heshima, ugonjwa anautaja mgonjwa mwenywe na sio mtu mwingine.
 
Nimefuatilia sakata la wabunge wa Chadema, na naona chama hicho kimefanya uamuzi wa busara, hasa kwa mamluki kama Antony Komu, David Silinde, na Joseph Selasini hawa walishatamka kwa kinywa kuwa wanahama chama kwa hiyo hakuna maswali.

Kwa busara nadhani ni vema wafikirie upya ombi la Wilfred Rwakatare la kuomba asikilizwe, ukizingatia anastaafu na mchango wake kama Mkuu wa Usalama na historia yake. Na ukizingatia pia chama hicho kimekua naye kwa shida na raha. Basi watimize ombi lake la kuomba asikilizwe kwanza; kuna makosa amefanya kama kutoa ile hotuba lakini kwakuwa anaenda kustaafu, atakuwa na muda wa kutafakari na kuwafaa kwenye baraza la wazee wa chama.

Hivyo basi, barua za kuwafukuza ni vema zikaandikwa kwa hao watatu Silinde, Komu na Selasini. Tena mtu kama Silinde ndio kabisa kaonesha upofu na kuvimbiwa kwa kiwango cha juu.

Natoa ushauri huu kama mzoefu kwenye baraza hili ambako tumeshiriki kushauri vyama vyote bila kuangalia itikadi zetu, iwe CCM au Chadema.

freeman
@jjmnyika
CHADEMA
Uchukue msaliti umuweke baraza la wzee, kwani kuna shida ya wazee wenye hekima na busara CDM?
 
Jumbe aliisaidia sana CCM ni mmoja wa waasisi wa CCM lakini alicross red lines.

Seif Shariff Hamad ni mmoja wa vijana waliokuwa kindakindaki wa CCM lakini alipozingua walimtosa.

Ni precedence mbaya kusamehe usaliti kama wa Lwakatare, mtu aliyepaswa kuelewa magumu ambayo chama kimepitia mpaka leo hii kwenda kuunanga uongozi wa Chadema unaotetea maisha ya watu dhidi ya Covid-19 ambayo serikali ya CCM imekwepa vita dhidi yake.
Anaketi kwenye vikao vya kamati ya uongozi na utumishi bila ridha ya KUB na mengine lkn CDM kwa uamuzi huu mmepotoka

Chama makini
Kingewahoji hata kwa simu basi kwa wakati huu

Baada ya kuvunja bunge mkawafukuza hapo chama kingegain momentum ya wabunge wenyewe na umma
Lkn leo inaonekana ni hasira, wivu na roho mbaya ambayo inatazama mafao tu ili wakose fedha za kampeni lkn chadema inapaswa kuwa na roho mbaya hivyo wakati umma ukiwahurumia ktk nyakati zao za shida?
 
Hahahahaahahaha wangefutwa uanachama baada ya bunge kuvunjwa???hahahahahah
 
Nimefuatilia sakata la wabunge wa Chadema, na naona chama hicho kimefanya uamuzi wa busara, hasa kwa mamluki kama Antony Komu, David Silinde, na Joseph Selasini hawa walishatamka kwa kinywa kuwa wanahama chama kwa hiyo hakuna maswali.

Kwa busara nadhani ni vema wafikirie upya ombi la Wilfred Rwakatare la kuomba asikilizwe, ukizingatia anastaafu na mchango wake kama Mkuu wa Usalama na historia yake. Na ukizingatia pia chama hicho kimekua naye kwa shida na raha. Basi watimize ombi lake la kuomba asikilizwe kwanza; kuna makosa amefanya kama kutoa ile hotuba lakini kwakuwa anaenda kustaafu, atakuwa na muda wa kutafakari na kuwafaa kwenye baraza la wazee wa chama.

Hivyo basi, barua za kuwafukuza ni vema zikaandikwa kwa hao watatu Silinde, Komu na Selasini. Tena mtu kama Silinde ndio kabisa kaonesha upofu na kuvimbiwa kwa kiwango cha juu.

Natoa ushauri huu kama mzoefu kwenye baraza hili ambako tumeshiriki kushauri vyama vyote bila kuangalia itikadi zetu, iwe CCM au Chadema.

freeman
@jjmnyika
CHADEMA
Lwakatare ameongea kama mtu mzima na anastahili kupewa nafasi ya kujieleza na ikiwezekana kusamehewa. Hamna haja ya kumbeza. Wakina Komu na Selasini walishaaga kuwa wanahamia chama kingine kwa hiyo wao kukaidi maagizo ya Mwenyekiti wa chama wanachokiacha haikuwa kitu cha ajabu. Silinde ni arrogant na inaelekea anaamini kuwa chama kinamuhitaji kuliko anavyokihitaji. Huyu aachiwe aende maana alibaki atawasumbua wenzake. Lwakatare alikosea alipoonekana kuchochea wanachama wengine wawaunge mkono. Pamoja na hayo anastahili kupewa nafasi ya kubaki kwenye chama.

Amandla...
 
Siasa za Bongo ni umiza kichwa. Mwanasiasa si mtu wa kuaminika kwa asilimia kubwa. Kwa maoni yangu asimilia ya kuamiklnika kwa mwanasiasa ni 10% tu. Asilimia zilizobaki ni uongo na ulaghai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom