Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,670
- 119,302
Wanabodi,
Hii ni barua wito kwa Baba Jesca, ili awatendee haki kina Jesca wengine wote wenye matokeo kama ya Jesca ili nao wapate bahati kama ya Jesca!.
Mpendwa Baba Jesca,
Salaam hapo ulipo.
Ama baada ya salaam, Baba Jesca, sisi wote ni wazima.
Dhumuni la barua hii fupi kwako Baba Jesca, ni kukuomba, kama unavyohubiri kuwa wewe ni mkweli daima na mtenda haki, hivyo barua hii ni kukuomba wewe Baba Jesca, uwatendee haki kina Jesca wengine wote, nao wawe kama Jesca.
Kuwaita kina Jesca wa wenzio kuwa ni vilaza, eti tuu kwa sababu wamepata "divisheni foo" sio kuwatendea haki!, kati ya hao kina Jesca wengine wanaopata divisheni foo, sio vilaza ila ni hali tuu.
Kweli kuna baadhi ya kina Jesca waliozaliwa kwenye familia bora zenye neema kama Jesca, tena wengine wazazi wao wote wawili sio tuu ni waalimu, bali wengine ni ma jiniasi wazuri wa kukariri nambari vichwani mwao, wanajua urefu wa kilometa za mababara kwa kichwa, wanajua idadi ya mifugo kwa kichwa, kuanzia idadi ya ngombe, mbuzi, punda, kondoo, kuku, wanajua hadi idadi ya samaki, kwenye bahari zetu, na maziwa yetu, kwa kichwa, hivyo kina Jesca wao, wakapewa kila kitu ili wafanye vizuri katika masomo yao, ikiwemo kupelekwa shule nzuri za kulipia, na kupatiwa mahitaji yote muhimu ya shule, vitabu vyote vya ziada na kiada, vifaa vyote vya shule, walimu wa kutosha na mazingira bora ya kusomea ikiwemo kupigwa tuisheni za nguvu!, lakini kwenye matokeo, bado waliopata matokeo kama ya Jesca wako, hawa ukiwaita ni vilaza, utakuwa hujakosea tena ndio utakuwa umewatendea haki, maana kiukweli kama hawa ni vilaza haswa!, kama mtoto amepewa kila kitu ili afanye vizuri akaishia kupata divisheni foo, kama ya Jesca, jee huyu angesoma shule za Senti Kayumba, angepata divisheni ngapi?!.
Kupata divisheni foo kwa hawa kina Jesca wengine kusiwe ndio sababu ya kudhalilishwa na kuitwa vilaza, kwa sababu ndani ya vilaza hawa wa divisheni foo, sio wote wamepata hizo divisheni foo kwa sababu ya ukilaza wao, bali kuna wengine wamepata divisheni foo kutokana na sakarimsitensesi mbalimbali za shule zetu za Senti Kayumba, hakuna vyumba vya kutosha vya madarasa, hakuna madawati, wengine wamesomea chini ya mwembe, au chini ya mti!. Kwenye vyumba vya madarasa hakuna walimu, hakuna madawati, hakuna vitabu vya kiada wala ziada, hakuna vifaa vya kufundishia, watoto wanaotoka familia masikini, wanashinda na njaa kubwa nzima kwa kupata mlo mmoja kwa siku, na kutembea umbali mrefu hadi kufika shule, na wote wanafanya mtihani mmoja ule ule aliofanya Jesca, sasa mtoto kama huyu kupata matokeo kama ya Jesca, na wewe ambaye ni mzazi wa Jesca, hukumuita Jesca kilaza, bali umewaita hawa watoto wa wenzio ndio vilaza na wanaowatetea nao ni vilaza, hivi ikitokea utafiti ukathibitisha kweli kuwa Jesca ni kilaza, litakuwa kosa au kukuonea kama tukikuita wewe ni Baba Jesca Kilaza, na mama Jesca tukamuita ni Mama Jesca kilaza, jee tutakuwa tumekukosea, kukuonea au hatukukutendea haki?!. Angalia mwenzako Baba MwanaAsha, baada ya matokeo yale ya MwanaAsha, angalia alimpeleka wapi Mwanaasha?, jilinganishe na wewe Baba Jesca, baada ya matokeo yale ya Jesca, linganisha na mahali Jesca alipo sasa.
Kwenye kupasi na kufeli, kuna wanaopasi wenye akili, lakini pia kuna wanaopasi kwa bahati tuu vivyo hivyo kwenye kufeli, kuna wanaofeli kwa ujinga au kwa ukilaza wa sample za kina Mwanaasha na Jesca, ila pia kuna wanaofeli sio kwa sababu ya ukilaza, wana akili nzuri tuu ila wanafeli kutokana na sababu nyingine tuu za kimaisha ikiwemo kupigika, kushinda njaa, kulala njaa, shule bila walimu, shule bila vifaa!, umbali wa shule zilipo, na matatizo mengine ya kimaisha na sio upungufu wa I.Q!.
Mfano hai ni mmoja wa mawaziri wako, yeye akiwa mtoto wa familia bora yenye uwezo, amesoma darasa moja na mtoto wa familia duni, masikini wa kutupwa!. Walipofanya mtihani wa darasa la saba, yule mtoto wa familia masikini ndio alipasi mtihani na yule wa familia bora, alifeli lakini kutokana na umasikini wa familia ya yule mtoto wa familia duni, masikini, hakuweza kujiunga shule ya sekondari maana hata pesa za kununua tuu sare ya shule hazikuwepo!, hivyo wazazi wa mtoto masikini wakalazimika kuiuza ile nafasi ya mtoto wao, kwa yule mwingine aliyefeli, hivyo huyo mtoto aliyefeli ndio akajiunga sekondari kuchukua nafasi ya yule mtoto wa masikini aliyepasi, na japo mwanzo alifeli lakini alifanya wandaz!, akafanya vizuri masomo yake, akaenda kidato cha tato na mwisho akajiunga chuo kikuu, na sasa ni msomi mzuri na ni mmoja wa waheshimiwa mawaziri wako!.
Dini zimetufundisha usimtendee mwenzio vile usivyopenda kutendewa nae!, Baba Jesca hao uliowaita vilaza, japo ni kweli wamepata divisheni foo za vilaza kama aliyopata Jesca, sio wote ni vilaza wa ukweli kama alivyo Jesca!.
Kubwa kuliko ni mahali Jesca alipo hivi sasa!, licha ya Jesca kupata matokeo aliyoyapa, lakini Jesca, sio tuu ana bahati kutokea familia bora kwa bali pia Jesca ana bahati ya kipekee kuwapo hapo alipo!.
Tanzania tuna kina Jesca wengi, ila sio kila mmoja wa Jesca hawa, ana bahati kama Jesca wako, wazungu wanasema "chariti bigini ati homu" kwa vile wewe ni mtenda haki, tunaomba u pirakitizi wati yuu purichi" kwa kumtumia Jesca kama mfano wa utendani wa haki bin haki, kwa ama Jesca ndio awe wa kwanza kuwepo mahali stahiki kwa mujibu wa matokeo yake, au kina Jesca wengine wote nao wapatiwe bahati kama ya Jesca!.
Salaam kwa Jesca na mama Jesca!.
Wasalaam.
Paskali
Kwa sisi wanabodi wengine!, katika kupigia chapuo usawa wa binadamu kuwa binadamu wote ni sawa, jee kuna haja ya kuwapigania kina Jesca wengine wote kwa kumchagiza Baba Jesca, Awatendee Haki Kina Jesca Wengine Wote Ili Nao Wapate Bahati Kama ya Jesca?!, au tukubali tuu binadamu hatulingani, kuna vilaza wenye bahati waachwe na bahati zao, na wale vilaza wengine wasio na bahati ndio waachwe wakafie mbali na ukilaza wao?!.
Angalizo!. Mhusika mkuu wa mada hii ni mtu anayeitwa Baba Jesca!. Nawaombeni tafadhalini sana, wana jf, sijataja jina lolote la mtu halisi zaidi ya neno Baba Jesca, nawaombeni sana, hata kama mnamdhania baba Jesca ni fulani, nawaombeni sana tena sana, tusitaje majina ya watu humu bila sababu, Jesca wako wengi, hivyo na kila mzazi wa Jesca, ni baba Jesca.
P.