Wito JF, dont add an insult to an injury, JF itafungwa!, karma ipo, kwa kuteseka kwake, JF itaponywa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,811
2,000
Wanabodi,

Kwanza naomba kuchukua fursa hii kuungana na Wana JF wenzangu kupeana pole kwa kilichomkuta Mkuu Max.

Alipokamatwa nilikwenda kumuona pale central na kuzungumza nae kwa kina.
Kwa sasa niko ziarani kutembelea Central Corridor, next week nitarejea na kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja na tusiishie kwenye keyboards tuu, bali tujipapase mifukoni hata ikibidi kupunguza kasma ya matanuzi ya mwisho wa mwaka, na tupunguze tunyooshe mikono kuungana na uongozi wa JF kufanya kila litakalowezekana.

Tangu kukamatwa kwa Max, nimenote concentration kubwa na hasira za wengi ni tendo la kukamatwa na kuzuiliwa, ma deep thinkers hawajikiti sana kwenye tendo la kukamatwa bali kwenye the motive behind kukamatwa kwa Max. Baada ya kuyasikia mashitaka anayotuhumiwa nayo, nimejiridhisha pasi shaka kuwa Max sio target, target ni kui silence JF, and Max is just a means katika kutimiza lengo hilo, hivyo let's be very careful tusiwape sababu.

Hivyo natoa wito kwa wana JF wote, tupunguze hasira na kutoa maneno makali, let's be as calm as we can, pamoja na uchungu wote, pamoja na hasira zote, no matter how bad our situation is, please let us not to loose our temper, if we loose our temper, we can make it worse hadi kuihatarisha JF kufungwa.

What is happening to Max, it's an injury, please let's not add an insult to an injury, tutamponza zaidi Max na you never know...

Kila mwenye akili ameisha jua kinachoendelea, wala simaanishi tunyamaze kimya as if nothing has happened or the government is doing the right thing, no!, ninamaanisha tupunguze hasira na jazba katika kulipigania hili, tuwe watulivu tuiache karma itake it's cause ndio sheria pekee ya haki bin haki duniani, na hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuizuia karma, let's keep calm, tuchangie kwa makini na utulivu kwa lugha ya staha, and sit and watch as karma takes its course in taking care of the situation.

Namalizia kwa kusisitiza huu ni wito tuu,

Namalizia kwa kusisitiza, huu ni wito tuu kwa wana JF, dont add an insult to an injury, JF asije akakasirika akaamua kuifunga kabisa JF!, Kuna kits kinaitwa karma kipo, kwa kadri Max anateseka kwa ajili ya JF, hivyo ndivyo JF itakavyo zidi kupaa, kukua, kuongezeka na kuimarika.

Maxi Pole Sana kwa mateso haya, ni kwa kuteswa kwako, sisi tutaponywa na JF itaendelea kusimama juu zaidi, bigger and stronger.

God Bless You,
God Bless JF,
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea kwa wasio jua Karma ni nini, tembelea hapa
https://www.jamiiforums.com/threads...ili-hapa-duniani-unahukumiwa-kwa-matendo-yako.

Na hapa
https://www.jamiiforums.com/threads...i-serikali-haramu-hukumu-ya-karma-ii-juu-yake.
 

Graph

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
2,748
2,000
Karma?
Hehehe tuache utani, ingekua karma leo hii nchi zote zilizokuja kugeuza waafrika kua slaves kwa kutumia nguvu zingekua zimefulia, ila ndizo bado zinatupelekesha hadi leo hii, wanaishi kwa raha mstarehe huku sisi bado tunasumbuka kama ombaomba.

Hakuna kitu kibaya kama silence. Tungekua kimya sidhani hata hiyo mahakamani kama angefikishwa, bongo unaweza rushwa miezi unazungushwa tu hadi kelele zipigwe ndipo watu wakushughulikie.
 

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,919
2,000
Wanaweza kuifunga jamiiforums wanayejua wamiliki wake, lakini ikaibuka Jamaaforums ambayo mmiliki wake ni anonymous asiyejulikana, na ikawa more powerful, more secure, more daring kuliko hata hii JF, mtandao utakao kuwa hosted nje ya nchi, lakini hiyo ni last option. Huwezi kuwanyamazisha watu kwa dunia ya leo!. Ukikomaa sana kubana uhuru wa habari mitandaoni wakumbuke kuwa duniani wapo mabwana wakubwa zaidi wanaomiliki Internet, wanaweza kuamua kuiblock hata hiyo intaneti isipatikane kabisa!
 

mirisho pm

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
3,311
2,000
So sad indeed.....I don't think if keeping it "quite " is the good idea....
Any ways [HASHTAG]#FREEMAXENCEMELO[/HASHTAG]
 

Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,316
2,000
mimi mwanzoni mwa utawala wa Magufuri ndio nilikua na hasira, chuki na ghadhabu nae, ila sasa nimemuelewa hata sina hasira nae tena na simshangai tena.

Akili yangu nilishaiandaa isishangae yatakayotokea katika utawala huu na hata yatakayonitokea mimi binafsi, tulifanya maamuzi sisi au ndugu zetu mwaka jana hivyo lazima tukubali uhalisia unaotokana na hayo maamuzi bila kujali yalifanywa na wewe au watu wengine.
 

stemcell

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
677
1,000
Wanabodi,

Kwanza naomba kuchukua fursa hii kuungana na Wana JF wenzangu kupeana pole kwa kilichomkuta Mkuu Max.

Alipokamatwa nilikwenda kumuona pale central na kuzungumza nae kwa kina.
Kwa sasa niko ziarani kutembelea Central Corridor, next week nitarejea na kuunganisha nguvu.

Huu ni wito wangu kwa wana JF, pamoja na uchungu wote, pamoja na hasira zote, no matter how bad our situation is, please let us not to loose our temper, if we loose our temper, we can make it worse hadi kuihatarisha JF kufungwa.

What is happening to Max, it's an injury, please let's not add an insult to an injury, tutamponza zaidi Max na you never know...

Kila mwenye akili ameisha jua kinachoendelea, tupunguze jazba, tuwe watulivu tuiache karma itake it's cause ndio sheria pekee ya haki bin haki, hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuizuia karma, let's keep calm sit and watch as karma takes care of the situation.

Maxi Pole Sana kwa mateso haya, ni kwa kuteswa kwako, sisi tutaponywa na JF itaendelea kusimama juu zaidi, bigger and stronger.

God Bless You,
God Bless JF,
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Mtu anapo tafuta sababu anaanza na mahali utakapo poteza busara,na kwa sisi ni kuwa makini na post zetu tusitoe mwanya wa kupata sababu.
 

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Hili suala ni tata sana ndo maana ilifika kipindi tukanyimwa misaada halafu tunaenda kwao kupiga chapuo waje kuwekeza kwenye Viwanda..
Daaaah.! tusipoongea hili raia watazidi kuumia sana tu...
Hakuna uongozi hapa tz ila majaribio ya uongozi.....
 

Papizo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
4,686
2,000
Sawa sawa mkuu ila leo wamefanya makusudi kumuweka ndani mpaka Monday inauma sana na why wamefanya hivyo....ila na sisi lazima tutoe kauli zetu ili wajue kwamba wanachofanya sio sahihi na Max yupo ndani kwa ajili yetu sisi wote....na tupo nae kwa ukaribu na akirudi lazima tuangalie namna ya kufanya......tutapigana miaka yoteee hii nchi yetu wote
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,874
2,000
Bila kuonyesha hasira wakosaji watajuaje kuwa wametenda maovu? Max ameshateseka na anaendelea kuteseka sasa Pasco unataka tuseme lugha laini ili wampunguzie machungu waliyo kwisha mpatia?
La hasha, kama Max atashuhudia hali hiyo atakata tamaa kwa udhaifu wetu.
Hata Mandela alizidi kuwa jasiri jela kila alivyokuwa anasikia ari ya watu inaongezeka na sio kuwapigia magoti makaburu. Mkuu unadhani tusipo onyesha temper zetu watamhamisha Segerea ili akalale Holiday Inn hadi siku ya kesi?
Haiwezekani, tumekasirika na wajue tumekasirika. Na kesho na keshokutwa tutakasirika zaidi. Najua nia yako ni njema ila acha mwenye kufurahi na afurahi sana lakini na mwenye kuchukia na achukie hadi hapo atakapo furahi
 

Eros

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
417
500
Wafanye sarakasi zao zote, lkn watuachie JamiiForums yetu. Nimejifunza mambo mengi sana kupitia JF, wakijaribu kuifunga wajue watakuwa wameongeza watu wenye hasira kali dhidi yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom