Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,522
Kitendo cha IGP Said Mwema kuruhusu matumizi makubwa ya nguvu zidi ya maandamano ya amani mjini Arusha hakiwezi kupita bila kulaaniwa na sisi wanamageuzi. CHADEMA alikuwa na kibali cha kufanya maandamano na mkutano halali kwa kufuta sheria zote za nchi. RPC wa Arusha alitoa kibali na kuahidi kutoa ulinzi. Ilikuwaje wewe unayedai taarifa za kiintelijinsia kungekuwa na uvunjifu wa amani kutumia nguvu za kipolisi kufanya mauwaji? Ifike wakati ufahamu kuwa mishahara ya polisi ni kodi zetu sisi wananchi. Kitendo cha polisi kupiga wakina mama na watoto wasio na makosa tunakilaani kwa nguvu zote. Demokrasia ya kweli na mageuzi haviwezi kuzuiwa kwa nguvu za dola. Wewe kama ni Muungwana tunakuomba ujiuzulu maana ni dhahiri humeshindwa kazi ya kulinda usalama wa raia.
Saidi Mwema tupe zawadi ya mwaka mpya kwa kujiuzulu. Jeshi la polisi ni la watanzania wote, kitendo cha kutumiwa na wanasiasa kunyamazisha upinzani ni sawa na kuzima moto kwa kutumia petrol.
Rev Masa K