Wito: Gomeni kwenda kuangalia mechi ya Brazil na Taifa Stars!

kama kweli mna nia ya kugoma basi sio kwa kukaa nyumbani bali chukueni mabango yenu yenye kulalamika shida ambazo wananchi wanazipata muende kila sehemu timu ya brazil itapita na hoteli kwao kwani international media zote zitakuwepo na ujumbe wenu utafika mbali sana.

lakini mkisema mkae nyumbani hakuna kitu kitachosaidia zaidi kwani brazil washalipwa na wananchi wataendelea kutaabika.nafasi nzuri hii ya kueleza matatizo ya wananchi kama itatumika vizuri.
 
Kwanza kabla sijasahau naunga mkono hoja,

Kuna baadhi ya watu wanataka kututoa kwenye msingi wa issue yenyewe ambao ni matumizi mabaya ya pesa za serikali ili tuone kiingilio kama ndiyo issue kubwa, kwangu mimi kiingilio siyo issue, kama wakituambia Brazil wameletwa na mtu binafsi hata kiwe laki kwa mzunguko sawa waende wenye nazo, lakini kama pesa ya serikali imetumika hiyo ndiyo issue, serikali isiyo na kiburi ilitakiwa ituambie imetoa kwenye fungu gani wakati bajeti ilishasomwa, hata kama ni TFF watuambie hizo hela wamekopa wapi serikalini? lakini kwa kiburi cha serikali yetu hilo kwao ni kitu cha kawaida sana.

Tanzania imelanguliwa na Brazil kwa kuuziwa mchezo wa gharama kubwa ilihali Brazil ikijua Tanzania ni masikini. Uingereza iliingia kwenye kashifa ya rada kwa shirika lake BAE kuiuzia Tanzania rada ya gharama wakati inajua Tanzania ni masikini. Tatizo letu hatuna wanasheria wazalendo wenye uchungu na nchi yao wengi wanaangalia matumbo yao vinginevyo ikichunguzwa kwa makini lazima kuna mchezo mbaya umefanyika.

Serikali inatumia kodi ya wananchi kufanya biashara kichaa, inakamua wananchi wake ili kuwafurahisha inaowaita watalii wa mbuga za mchangani inge-subsidise basi ili wakipato cha chini wanufaike kwa kodi yao. Binafsi naiona biashara hii ni sawa na kashifa ya Rada na ikifuatiliwa zaidi kuna wengi watahusika wakiwemo waliotoa baraka, TFF na Brazil yenyewe.
 
Br. Luteni I side with u,

Hapa tatizo sio gharama au kiingilio. Tatizo hapa ni suala la serikali kujitumbukiza kwene biashara ambazo hazipo justified.

Kwanza kisera serikali ilishasema inajivua kwene kufanya biashara..sasa iweje leo inafanya kinyume?. Serikali imejitoa kwene kuendesha mambo muhimu kama ya miradi yenye tija kwa taifa, badala yake inajiingiza kwene mambo ya burudani ambayo mwisho wa siku wafaidika ni wachache na jamii haifadiki na lolote. Kwanini serikali kama inawashwa na fedha 'nyingi' kwanini basi isianzishe miradi ya umwagiliaji vijana wakaajiriwa na tukaondokana na aibu ya kusaidiwa chakula now and then? Au kwanini isifungue miradi mikubwa ya kutengeneza bidhaa ndogo zisizohitaji capital kubwa, tukaondokana na aibu ya kuagiza mpaka chopstick kutoka nje?

Nashindwa kabisa kuelewa..
 
Hivi huyu serikali ya Tanzania angekuwa ni individual, say John agekuwa na sifa zipi mtaani na angekuwa anaelewekeje. Just try to image our govt to an individual. I will tryh to mention a few:

1. Ombaomba

2. Mnafiki

3. Muongo

4. Mwoga etc. etc. etc.
 
5. Tapeli

6. Muuaji

7. Mpenda starehe (lakini hapendi kazi)

8. ...
 
kama kweli mna nia ya kugoma basi sio kwa kukaa nyumbani bali chukueni mabango yenu yenye kulalamika shida ambazo wananchi wanazipata muende kila sehemu timu ya brazil itapita na hoteli kwao kwani international media zote zitakuwepo na ujumbe wenu utafika mbali sana.

lakini mkisema mkae nyumbani hakuna kitu kitachosaidia zaidi kwani brazil washalipwa na wananchi wataendelea kutaabika.nafasi nzuri hii ya kueleza matatizo ya wananchi kama itatumika vizuri.

Unafikiri kuna mwenye ujasiri huo?Watabaki kulalama hapa JF na majina ya kujificha wote hao wanaobweka hapa JF hakuna hata mmoja mwenye ujasiri huo!
 
Unafikiri kuna mwenye ujasiri huo?Watabaki kulalama hapa JF na majina ya kujificha wote hao wanaobweka hapa JF hakuna hata mmoja mwenye ujasiri huo!
Mkulu

1.Suala la kujificha kwa majina yetu ili khali wanatufahamu haisaidii..

2.Hoja nyingine ambayo nimeikumbuka ni serikali kujihusisha na Biashara wakati ilishaacha,kama alivyosema Mzee Mwanakijiji ni bora ingeruzukuk hiyo pesa kama kweli lengo ni kuwafariji watanzania..Mnaweza mkalipa hata 15,000 kama JK akiamua..

3.Tatizo la Mechi hii imegubikwa na Rushwa,suala la mtu kufanya lobbying ya kuipata Brazil ilitakiwa ifanywe kama Tender kama sheria zinavyosema.Ndiyo maana naomba PCCB wachunguze

4.Msimamo wangu bado uko pale,Kugomea mechi hii na nakwambia wito unaendelea kupokelewa na watanzania wengi na utasikia habari yake
 
Unafikiri kuna mwenye ujasiri huo?Watabaki kulalama hapa JF na majina ya kujificha wote hao wanaobweka hapa JF hakuna hata mmoja mwenye ujasiri huo!
Asavali ya sisi tunaobweka kuliko mikondoo inayoenda machinjioni huku ikishangilia..

Tunachokosa waTz ni institutions imara zenye nia ya kweli na mustakabali wa waTz. Institutions kaa hizo ndizo zingekuwa kitovu cha ku-create awareness na moves za kuipelekea mbele nchi. Kinyume cha hapo tulionao ni waganga njaa ambao wana nia na pupa tu ya kushika uongozi na sio kumsadia mtz wa kawaida.

Hicho kitu kinakosekana na nakubali, kukosekana kwa vitu kama hivo ndo haswa vinavosababisha CCM waendelee kupeta na watapeta mpaka kizazi cha kondoo kitakapoamka.
 
Inawezekana hata kupiga danadana kumi tu walikuwa hawezi enzi zi kucheza ipira ya makaratasi primary skuli

Mtazamaji
Hivi ni lazima kupiga dana dana ndiyo uweze kujenga Hoja,Mbona unakuwa na mawazo hafifu katika kujibu hoja nzito?Jenga hoja na siyo unaleta Viroja.

Wakati mwingine inatosha kuwa mtazamaji na msomaji bila kuchangia
 
hatutaambiwa pesa kiasi gani wametumia .........watasubiri mpaka mechi iishe watuambie hawajala hasara!

wanaoendesha na wanaoendeshwa kwenye nchi hii ni wendawazimu
 
Gharama za Ufisadi Hulipwa na Maskini, Maadam kuna Mafisadi hawatagoma basi na Maskini itabidi tu wajikakamue wakaone Mtanange
 
Watanzania wenzangu,

Siku zote nimekuwa nikiwahurumia sana kwa ajili ya matatizo yanayowakabili,ila hili la ujio wa timu ya Brazil nimelifurahia sababu ni moja ya michezo ambayo mnaipenda

Kwa kuwa tumesikia na kuona na nimeukuu hapa chini basi nawasihi sana mgome kwenda kuwatazama Brazil na njia sahihi ni kutazamana kupitia TV zenu huku mkiburudika na ulanzi au coca cola

Sababu za kugomea mechi hizo ni hizi hapa

1.Mpira wa miguu haujawahi kuwa anasa kiasi cha watu kulipa dola 25.(TSH 30,000)kuangalia mechi moja katika nchi iliyo na huduma mbovu za kijamii,maisha duni kwa kila mtannzania.

2.Hii wizara imekaa na kuamua kutoa Dola milioni sita,Hii pesa imetoka kwenye bajeti ipi?

3.Gharama hizi ni za juu sana na tunaomba kupatiwa mchakato mzima wa jinsi ya makubaliano yalivyofanyika

4.Sulivan Summit ilifanyika hapa ,Wor;d Economic Forum pia.Je ni faida gani tumepata kutokana na Mikutano hiyo?Je na huu utalipatia faida taifa kiasi gani?au ni kutafuta Sifa tu zisizo na tija?

Baada ya kutoa sababu hizo hapo juu naomba kuwauliza serikali.

1.Kama kuwaongezea walimu pesa kunahitajika pesa nyingi,kwanini wizara isikae na kutafuta pesa kwa ajili ya kuwaongezea mishahara?imeonekana wanaweza kukaa na kupata pesa.Ndiyo tupo tayari kukchangia hata kwa kwenda kuwaona Simba na Yanga ili mradi pesa iende kwenye Maendeleo

2.Nchi ambayo haina walimuwa kutosha,madawati ya kutosha na upungufu wa maji kwanini pesa kama hizi hata kama ni za kukopa zisielekezwe huko.

3.Hizo pesa mmezitoa kwenye Bajeti gani?nataka kupata jibu haraka iwezekanavyo ili nishauri nini cha kufanya.Haiwezekani pesa inachukuliwa chukuliwa ovyo ovyo kwa maamuzi ya wachache bila bunge kuidhinisha?

I don't buy this idea at all unless otherwise.Ila siwalazimishi kugoma kama Mnataka endeleeni tu kuunga mkono na mtakuwa mkifanya hivyo kuongeza kiwango ya umasikini mlionao..

hivi tenga kabla ya TFF alikuwa anafanya kazi wapi?i need to know sababu naona akili yake inakwenda tenge.

Nipo na wachungaji tunawaombea .Gharama za zimbabwe hizi hapa chini

Kweli Tanzania ni nchi yangu tutayaona mengi ndani ya miaka mingine mitano.
 
Attachments

  • ujinga.jpg
    ujinga.jpg
    33.9 KB · Views: 50
Jameni , watu huwa tunachangia harusi/send off/ kitchen party kwa garahama kubwa zaidi ya viingilio vya hiyo mechi. Hii yote ni kujifurahisha nafsi zetu. Like wise , hata hiyo mechi ni kwa ajili ya kujifurahisha nfsi zetu.
 
Tofauti ya harusi na hii mechi ni kwamba harusi by default hazihusishi matumizi ya public funds.

Hii mechi imehusisha irresponsible use of public funds.

Big difference.
 
Hizi gharama zinaweza kurudishwa na uchumi wa Tanzania na tukanufaika bado kiuchumi. Utalii: kuna wageni watatoka nje kuja Tanzania kwa ajili ya mechi hii na watatembelea sehemu mbali mbali za utalii. Hakuna sababu ya kuwa skeptical na kila kitu. Hili la Brazil litajilipa nadhani TFF wanakosa confidence ya kwenda OUT na kusema, tumechukua mkopo hazina na tunatarajia kuzirudisha through sponsourships na gate fee collections.

Of course kukosekana kwa uwazi wa kuwa tumelipa shillingi ngapi ni issue, lakini this is a plus kwa nchi kama Tanzania. Ilitakiwa TFF waje na forecast za kutosha za kuonesha jinsi nchi itakavyonufaika, kwa sababu nchi itanufaika no doubt about it. Tatizo TFF na serikali hawajiamini kutokana na historia ya utendaji mbovu hivyo wanakosa confidence ya kuwa face watu na kuwaambia tumetumia X tunatarajia kupata Y.

Bado naona safari ya Brazil Tanzania is a PLUS kubwa sana. We rely heavily on tourism and anything that will put us on a tourist map is a plus. Labda wengine hamjui mambo ya marketing, lakini safari kama hii ya Brazil ni marketing nzuri sana inayoifanya Tanzania i stand out in EA.

Kuna benefits nyingi nchi itapata, TFF na serikali ilitakiwa waje na forecasts za kueleweka. We are spending too much on tourism promotions for too little benefits. This will have a Mamoth imnpact on tourism promotion we need to support it.
 
Mazee unaweza kutoa breakdown ya mahesabu yako? Tutarudishaje hizi gharama?

Unataka kutuambia Brazil itatumia $ 6m kwa siku chache itakayokaa hapo bongo?

Is this the best use of this money in therms of ads? Unajua ukitaka kuchukua prime time ads za CNN zinazowafikia Wamarekani nchi nzima ni kiasi gani kwa 30 seconds? na kwa kutumia hela hizi ungeweza kupata ads hizi ngapi? Prime time, nationwide, kwa watalii haswa si watazamaji mpira tu? Unajua kitu kinaitwa "Return on Investment" ? Unajua ad spanning? Unajua kitu kinaitwa target market ?

Siyo tunakuja kuimbishana ngonjera za "follow the leader" tu hapa, mradi wakubwa wamesema tuwa support tu.

Haya ni matumizi mabaya ya pesa za umma na ni lazima tuseme.

Zaidi ya yote hayo, unataka kutangaza utalii kwa mamilioni ya dola wakati hata infrastructure za ku support utalii huo huna.
 
Kwakeli Gembe mkuu una point kuna mashimo pale barabara ya umoja wa mataifa kwenye kona ya kuelekea hospitali ya taifa usipime,kwanza kero kwa foleni hata huyo mgonjwa anayewahishwa anaweza asifike salama either akaongezea magonjwa au kupoteza uhai,pili foleni yake pale ni usumbufu pia,sasa kweli hata hayo mashimo kufukia kweli tunasubiri bajeti ya 2010/11?!! huku tuna bajeti ya mahela kibao kuleta timu kubwa kama hizo na bado hapo mtanzania wa kawaida atozwe kiwango kikubwa,kwani tulisema wawawelete hao? mbona hatukushirikishwa wote na tukakubaliana nani aje na tuingie kwa kiingilio kipi?!
 
Hili la Brazil kuja limekamilika. Limeisha. Tuangalie tu jinsi ya kuyazuia matumizi kama haya kwa visingizio vya kukuza utalii. Angalau BUNGE letu liwe linaulizwa. Natumaini pia kikao kijacho cha bajeti wabunge wetu watahoji hili. Serikali/TFF wataulizwa mapesa haya ya kuwaleta Brazil yametoka wapi, yametumikaje, yamerudi kiasi gani, tumenufaika vipi kama TAIFA.
 
Back
Top Bottom