Wito: Gomeni kwenda kuangalia mechi ya Brazil na Taifa Stars! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito: Gomeni kwenda kuangalia mechi ya Brazil na Taifa Stars!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gembe, May 31, 2010.

 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Watanzania wenzangu,

  Siku zote nimekuwa nikiwahurumia sana kwa ajili ya matatizo yanayowakabili,ila hili la ujio wa timu ya Brazil nimelifurahia sababu ni moja ya michezo ambayo mnaipenda

  Kwa kuwa tumesikia na kuona na nimeukuu hapa chini basi nawasihi sana mgome kwenda kuwatazama Brazil na njia sahihi ni kutazamana kupitia TV zenu huku mkiburudika na ulanzi au coca cola

  Sababu za kugomea mechi hizo ni hizi hapa

  1.Mpira wa miguu haujawahi kuwa anasa kiasi cha watu kulipa dola 25.(TSH 30,000)kuangalia mechi moja katika nchi iliyo na huduma mbovu za kijamii,maisha duni kwa kila mtannzania.

  2.Hii wizara imekaa na kuamua kutoa Dola milioni sita,Hii pesa imetoka kwenye bajeti ipi?

  3.Gharama hizi ni za juu sana na tunaomba kupatiwa mchakato mzima wa jinsi ya makubaliano yalivyofanyika

  4.Sulivan Summit ilifanyika hapa ,Wor;d Economic Forum pia.Je ni faida gani tumepata kutokana na Mikutano hiyo?Je na huu utalipatia faida taifa kiasi gani?au ni kutafuta Sifa tu zisizo na tija?

  Baada ya kutoa sababu hizo hapo juu naomba kuwauliza serikali.

  1.Kama kuwaongezea walimu pesa kunahitajika pesa nyingi,kwanini wizara isikae na kutafuta pesa kwa ajili ya kuwaongezea mishahara?imeonekana wanaweza kukaa na kupata pesa.Ndiyo tupo tayari kukchangia hata kwa kwenda kuwaona Simba na Yanga ili mradi pesa iende kwenye Maendeleo

  2.Nchi ambayo haina walimuwa kutosha,madawati ya kutosha na upungufu wa maji kwanini pesa kama hizi hata kama ni za kukopa zisielekezwe huko.

  3.Hizo pesa mmezitoa kwenye Bajeti gani?nataka kupata jibu haraka iwezekanavyo ili nishauri nini cha kufanya.Haiwezekani pesa inachukuliwa chukuliwa ovyo ovyo kwa maamuzi ya wachache bila bunge kuidhinisha?

  I don't buy this idea at all unless otherwise.Ila siwalazimishi kugoma kama Mnataka endeleeni tu kuunga mkono na mtakuwa mkifanya hivyo kuongeza kiwango ya umasikini mlionao..

  hivi tenga kabla ya TFF alikuwa anafanya kazi wapi?i need to know sababu naona akili yake inakwenda tenge.

  Nipo na wachungaji tunawaombea .Gharama za zimbabwe hizi hapa chini
   
 2. masharubu

  masharubu Senior Member

  #2
  May 31, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi kale ka mkutano ka World Economy pale ubungo si ndio kalishusha thamani ya shilling hafla bin vuupu?Wakija hawa brazili naona ndio itafika dola moja 2500. Hivi nchi hii ina wachumi kweli? Kiingilio hicho jee watu wasipoingia hiyo hasara atalipa nani?tulishasikia TFF wamepata hasara mechi na Ivory Cost na kiingilio kilikua cha chini ni 5,000.00 jee hapa pa 30,000.00 penyewe pakoje?

  Tiketi muuze kihalali hatutaki wizi hasa hizo za 30,000.00, Tenga upoooooo
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  haiwezekani kugoma mkuu.umeshachelewa...ukitaka kuamini, nenda weka mabango kwenye kila kituo cha mabasi hapo dar, mabango yanayotangaza kuwa watu wagome mechi...YATANG'OLEWA LISAA HILOHILO kwasababu watu wanapenda kuingia kwa garama yoyote...pia, namba ya watu hapa jf ni kidogo sana kufanya mgomo, hivyo labda jiandae kwaajili ya matukio yajayo ili kuorganise watu wagome lakini si hili...hili tunatakiwa tu kwenda kuangalia mpira.
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  May 31, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,411
  Likes Received: 1,868
  Trophy Points: 280
  Gembe ni kweli kabisa hakuna sababu ya watu kwenda mpirani kwani kuna shida ngapi ambazo serikali inadai haiwezi kuzitatua kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha na shida hizo zipo miaka nenda rudi,sasa huu ujio wa Brazil billioni 3 zimepatikana ndani ya wiki moja! Kwa kugomea mechi hii sisi wananchi tutaonyesha kupinga serekali kwa matumizi yasiyo ya lazima yanayo maliza pesa ambazo zingeelekezwa kwenye sehemu muhimu.

  Wazazi wanalala chini hakuna vitanda,wanafunzi wetu wanakaa chini hamna madawati, wanafunzi wa vyuo vikuu wanaburuzana na bodi ya mikopo kwa madai kuwa pesa hamana sasa hii fahari ya kuagiza Brazil tunapata wapi nguvu ya kufanya hivyo? Hizo billioni 3 zingenunua vitanda vingapi au madawati managapi kwa faida ya watu wetu?
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  I concurr.

  BOYCOTT.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kukugongea senks, napenda kukupongeza tena kwa maneno, Kaka Gembe umenena
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  May 31, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,411
  Likes Received: 1,868
  Trophy Points: 280
  Ni aibu na fedheha kwa serekali inayoshindwa kutoa huduma muhimu kwa raia wake ina thubutu kufanya ufujaji mkuu kama huu wa pesa nini faida ya timu hii kwetu? Suala la kujitangaza kwa ajili ya utalii haliingii akilini kwani hawaendi kwenye hivyo vivutio vyetu vya utalii. Hizo billioni zingeelekezwa mahosipitalini kusikokuwa na vitanda na mashuleni ambapo wenetu wanakaa chini!
   
 8. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  kwani wameshaanza kuwauzia tiketi?

  kuna haja ya kukata mambo mabaya hata kama ni kesho..Mie nataka kugoma ili muwashinikize waseme wametoa pesa kiasi gani na zimetoka wapi?

  Pili waambie ni lini watakaa na kutafuta pesa kushughulikia mambo mengine ya Msingi,wakati ndiyo huu na sababu mnayo
   
 9. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hamu yote imeniishia jamani. Nchi nyingine ni katiri sana, yaani kweli wanakubali kuchukua kiasi chote hichi kutoka kwa omba omba. Nasikia agent fee ni $1,800,000 du du du du! eeeh ebwana eee!
   
 10. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Seconded. Tugome, period!!!
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Lazima ukubali kuliwa ili nawe ule.....vipi Texas!
   
 12. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135

  Nimegundua serikali ina dharau kwa wananchi..

  wana uwezo wa kupata pesa kabisa ...tunakalia kupenda sifa tu

  Agent ni nani?we need to dig all this shit..lazima atakuwa ametoa Commission.We need to know the whole story!
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Watz ni mapunda wana-ask for more MIZIGO..Gembe relax and chill dude, mabadiliko kwa kizazi hiki cha punda haiwezekaniki.
   
 14. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160


  Una akili sana. Ya nini Brazil, ya nini? Inatusaidia nini? Sisi ni mabwege au?
   
 15. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watu wengine wasiopita kwenye jukwaa hili wahamasishwe kwa njia ya SMS, Facebook, Twitter n.k.
   
 16. Mike-Austin

  Mike-Austin Member

  #16
  May 31, 2010
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unataka kugoma?, wewe peke yako labda.

  1. Unataka ukamuangalie KAKA; ROBINHO etc kwa TZS 5,000?, sio wakina MGOSI hao......tambua thamani ya starehe, kwanini usiseme Ngasa kusajiliwa kwa TZS 58mil ni nyingi leo wasema wanaosajiliwa kwa USD 58mil ni anasa?
  2. Thamani kubwa tutatangazwa katika vituo visivyopungua 164 dunia nzima, utalii tosha kwetu kaka na tutajulikana vema kwa soka letu tukicheza vema......si kuwategemea watalii maskini wajao TZ unamkuta mtalii anajua hata nauli ya G/mboto - Posta?.
  3. Ku-maintain nyumba ndogo a.k.a "assistance" bei ghani? ipi bora kuliko kutii kiu yako ya mpira?....starehe gharama.

  NB: Ila hoja ya pato lenyewe naona litakuwa kubwa sana, hoping wakina Tenga & Kaijage etc watamalizia vibanda vyao, hata ikiwezekana kuwa-Liyumba wakina d..d.ddd wetu.

  Mie simo kwenye huo mgo
   
 17. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Viingilio mechi ya Stars vs Brazil

  VIP A 200,000 (sold out)
  VIP B 150,000
  VIP C 100,000
  Orange 80,000
  Mzunguko 30,000
   
 18. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Thamani ya starehe ni kulipa pesa nyingi?watu huko vijijini wanaangalia gobogobo kwa kulipa mia mbili tu na wanapata starehe.Hauna hoja hapa

  Watalii wanakuja kutokana na kucheza mpira vizuri?hao watalii masikini wamekuja hata kabla ya Brazil haijaja ,hauoni kuwaita masikini ni kuwakosea nidhamu?Tulishakuwa na Sullivan,WEP etc Je ni watalii wangapi wameongezeka?dude even Drogba was here..ulifaidika na nini?

  Siyo kila mtu ana nyumba ndogo.Starehe gaharama kama una pesa za ziada bila kutumia pesa ya mwenzako,kutumia bil3 ni kuwaibia masikini walioko Mtwara na Lindi,na Nchi yote.

  hilo linawezekana ila sijui
   
 19. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hivi TFF walifikiria nini kuweka viingilio vikubwa hivi?.............Inasikitisha sana kwa kweli.........Ni vema tukagoma tu kwenda kuangalia ili liwe fundisho........Kiingilio laki 2!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!................kisa Brazil????????...aaaaaaaaaaaaaargh


  Naunga mkono hoja...............Tugome
   
 20. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Swali..................Ni nani hasa walengwa wa mechi hii????????????????????????????????????....................Ni watanzania wote ama wachache wenye uwezo?


  Mbona Cameroon ya akina Eto'o walivokuja tulienda waangalia kwa 5,000 na kiwango cha juu kilikuwa 50,000(kama sikosei)..............Ngoja tusubiri na tuone.............
   
Loading...