Wito fanya ufutaji wa akaunti zako kwenye applications au kompyuta kabla huja uninstall programu husika

BenKaile

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
443
373
Sitakupa maelezo marefu sana ya kupoteza muda wako, ila umakini na faragha ni muhimu sana nyakati hizi za kimageuzi ya mitandao na ukuaji wa teknolojia.

Kwa watumiaji wa vifaa ya kimtandao kama simu na kompyuta iwe ya mezani au mipakato jaribuni sana kuwa na umakini ikiwa utaacha kutumia programu au wavuti fulani iwe ya kimtandao wa jamii, mauzo ya kimtandao, biashara za kibenki n.k ni vyema sana kuwa na tabia ya kufuta au kuondoa maelezo nyeti juu ya akaunti yako/zako kwenye majukwaa tofauti tofauti uliyojiunga awali kabla ya kuondoka na mwisho ukitaka kufuta/kuondoka kabisa, na hii inategemea unataka labda kubadilisha kifaa kipya, kuuza ili upate fedha, kuazima mtu mwingine n.k

Angalizo hapa ni kuwa usipofanya ufutaji wa awali wa taarifa zako nyeti basi itawezesha kuruhusu uepukuzi au ufuatiliwaji wa watu au vifaa vingine kupata data zako kirahisi kwani rekodi haikutunzwa vizuri. Na umuhimu wa zoezi hili itakupunguzia hadha ya kupatwa na spam wengi ambao hushambulia data mitandaoni, itaimarisha safu ya usalama wa taarifa zako (security risks) na kuongeza usiri mkubwa juu ya maelezo yako mtandaoni (privacy concerns).
 
Back
Top Bottom